1: Utangulizi

Figo ni kuingo cha kushangaza ambacho hufanya kazi muhimu kwa kuweka miili yetu safi na yenye afya kutokana na uwezo wa figo kutoa uchafu na sumu.

Ingawa kazi ya msingi ni kutoa uchafu katika mwili, hii sio kazi pekee. Figo pia hufanya kazi muhimu ya kusawazisha presha ya damu, kuweka ujazo wa majimaji na viini vingine sawa katika mwili (balanced fluid and electrolytes).

Ingawa wengi wetu huzaliwa na figo mbili, lakini figo moja tu huweza kujitosheleza kufanya vyema kazi zote.

Kwa miaka ya hivi karibuni kumejitokeza wagonjwa wengi wa kisukari na shinikizo la damu ambayo imeleta idadi kubwa ya wagonjwa wanaougua ugonjwa sugu wa figo. Hii inatutaka tuwe na msukumo mkubwa zaidi wa kuwajulisha watu na kuwafanya waelewe magonjwa ya figo, kinga yake na matibabu ya mapema. Kitabu hiki kinajaribu kuwasaidia wagonjwa kuelewa magojnwa yanayohusiana na figo na kuwa tayari kujiandaa kupambana nayo. Kinajaribu pia kutoa majibu ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara.

Mwanzo wa kitabu kimetanguliza kuwaeleza wasomaji kuhusu figo, kiungo muhimu katika mwili wa binadamu na kupendekeza mbinu za kujikinga na magonjwa yanayohusiana na figo. Hata hivyo, sehemu kubwa ya kitabu imelenga hasa mambo ya wagonjwa wa figo na familia zao. Kitabu kinashughulika na vyanzo, dalili na uchunguzi wa magonjwa yanayoogopwa, na pia kujulisha wasomaji juu ya matibabu mbadala yaliyopo.

Sura maalum inalenga juu ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa mwanzoni mwa ugonjwa sugu wa figo na jinsi unavyoweza kuuepuka.

Kuchelewesha matibabu ya kusafisha damu (dialysis) na hata kuwekewa figo nyingine. Ujumbe mwingine juu ya matibabu, kuamisha figo na figo la “mfu” pia umetolewa tofauti.

Ili kufanya kitabu hiki kiwe mwongozo kamili kwa wagonjwa wa figo kimejumuisha ujumbe juu ya shida za kawaida za figo (kando na kushindwa kwa figo): imani potofu (myths), Nadharia na ukweli juu ya ugonjwa wa figo, sheria muhimu za kuepuka na kukinga magonjwa ya figo, hoja muhimu juu ya dawa za kawaida zinazotumiwa na wagonjwa wa figo na mambo mengi menginei.

Kwa kuwa lishe ni sehemu muhimu ya kushughulikia na inayoleta kuchanganyikiwa kwa wagonjwa wa ugonjwa sugu wa figo (CKD), sura tofauti imetengwa kwa sehemu hii. Inawashauri wagonjwa kuchukua tahadhari ya kuchagua lishe sawa na inayotosha. Maelezo (glossary) yaliyo mwisho, yanaeleza vifupisho vyote na kufafanua ujumbe na maneno ili kufanya usomaji wa kitabu hiki uwe rahisi.

Tanbihi: Ujumbe uliotolewa katika mwongozo huu wa figo ni wa kuelimisha pekee. Tafadhali, usijihusishe katika hali yoyote ile ya kujichunguza ama kujitibu kwa kutumia maarifa uliyopata kutokana na kitabu hiki. Lazima kila mara ushauriane na daktari ama mhudumu yeyote wa tiba kwa matibabu ya kitaalamu.

Elewa figo yako – kinga magonjwa ya figo.