Wakati figo hazifanyi kazi yoyote,dayalisisi ni njia ya bandia ya
kutoa uchafu na maji yasiyohitajika mwilini.Njia bora ya kuokoa
maisha kwa watu ambao figo zao zimedhoofika kabisa.
Dayalisisi huwasaidiaje wagonjwa wenye figo zisizofanya
kazi?
Dayalisisi husaidia mwili kwa kufanya kazi ambazo omit zingalifanywa
na figo ambazo sasa hazifanyi kazi kama ifuatazo:
- Kusafisha damu kwa kutoa uchafu kama kreatinini na yurea
mwilini.
- Kutoa maji yasiyohitajika mwilini na kusawazisha kiwango
kinachofaa mwilini.
- Kurekebisha usawa wa kemikali kama chumvi,potasiamu na
magadi mwilini.
Hata hivyo,dayalisisi haiwezi kufanya kazi za figo za kawaida
kama vile kudumisha himoglobini kwa kutengeneza eraithropoyetini
wala kudumisha mifupa yenye afya.
Dayalisisi huhitajika lini?
Kazi ya figo inapopungua kwa asilimia themanini na tano au
tisini(kipindi cha mwisho cha ugonjwa wa figo - ESKD),figo basi
huwa hazitoi uchafu na maji ya kutosha kutoka mwilini.Hali hii
husababisha dalili kama kichefuchefu,kutapika,kuchoka,kuvimba na
kushindwa kupumua.
Dayalisisi ni njia ya haraka na bora ya kutibu
wagonjwa wenye figo zilizodhoofika zaidi.
Katika kipindi hiki cha ugonjwa sugu wa figo,dawa huwa hazifanyi
kazi na basi dayalisisi huhitajika.Mgonjwa huhitaji dayalisisi, vipimo
vya damu vinapoonyesha kreatinini ya 8.0mg/dl au zaidi kwenye
damu.
Je,dayalisisi inaweza kuponesha ugonjwa sugu wa figo?
La hasha!Ugonjwa sugu wa figo hauponi kwa hiyo mgonjwa aliye
katika kipindi cha mwisho cha ugonjwa huu huhitaji dayalisisi maisha
yake yote,isipokuwa akipatiwa figo nyingine.
Kwa upande mwingine,mtu mwenye ugonjwa wa figo wa muda huhitaji
dayalisisi kwa muda mfupi tu hadi figo zitakapopona / zitakaporudia
kazi yake kama kawaida.
Aina za dayalisisi
Kuna aina mbili kuu ya dayalisisi
- Dayalisisi ya damu.
- Dayalisisi ya tumbo.
Dayalisisi ya damu
Hii ndiyo njia inayotumika sana kutibu wagonjwa walio katika kipindi
cha mwisho cha ugonjwa wa figo.Hufanywa kwa kutumia figo bandia
na mashine ya dayalisisi kutoa uchafu na maji yasiyohitajika kwenye
damu.
Dayalisisi ya tumbo
Dayalisisi ya tumbo pia ni njia bora ya kutibu kipindi cha mwisho cha
ugonjwa wa figo – (ESKD). Hapa,mpira laini unaoitwa katheta
huingizwa katika tumbo.Kupitia katika kimpira hiki au tyubu hii,maji
ya dayalisisi huingizwa kwenye tumbo na hutoa uchafu na maji
Dayalisisi haiponyi figo lakini humsaidia mgonjwa
kuendelea kuishi vyema ingawaje figo hazifanyi kazi.
yasiyohitajika mwilini.Njia hii huweza hutumiwa nyumbani bila ya
mashine.
Ni mambo gani yanayozingatiwa ili kuamua aina ya
dayalisisi itakayotumiwa?
Aina zote mbili za dayalisisi ni bora kwa wagonjwa walio katika
kipindi cha mwisho cha ugonjwa sugu wa figo.Hakuna njia moja
ambayo inaweza kusemekana kuwa inafaa zaidi kwa wagonjwa
wote.Baada ya kuangalia faida na upungufu wa kila aina ya
dayalisisi,uchaguzi hufanywa na mgonjwa pamoja na familia yake na
daktari bingwa wa figo.Mambo muhimu ya kuangalia ni gharama ya
matibabu,umri,magonjwa mengine yaliyoambatana na hali hii,umbali
kutoka hospitali,kiwango cha elimu,mapendekezo ya daktari na
maisha na shughuli za kawaida za mgonjwa.Kwa sababu ya gharama
na kupatikana kwa urahisi,dayalisisi ya damu ndiyo hupendelewa sana
na wagonjwa wengi Bara Hindi (India}.
Je,wagonjwa wanaofanyiwa dayalisisi huhitaji kuzingatia
ushauri wa vyakula vyao?
Ndio,ushauri wa vyakula kwa wagonjwa wa dayalisisi huwa ni kudhibiti
chumvi, potasiamu,fosforasi na vinywaji. Lazima wagonjwa wazingatie
ushauri wa daktari kuhusiana na vitu hivi lakini masharti hupunguzwa
baada ya dayalisisi kuanzishwa kwa wenye ugonjwa sugu wa
figo.Wengi hushauriwa wale vyakula vyenye protini nyingi na vyenye
kuleta nguvu nyingi,vitamini na madini.
Je, ‘Uzito mkavu’ ni upi/ nini?
Maneno ‘uzito mkavu’ hutumika sana kwa wagonjwa wa
dayalisisi.Hunamaanisha uzito wa mtu baada ya umajimaji wote
Hata baada ya dayalisisi kuanzishwa, ushauri
wa vyakula uendelee na lazima uzingatiwa.
usiohitajika umetolewa kwa dayalisisi.‘Uzito mkavu’ unafaa kurekebishwa mara kwa mara kulingana na uzito halisi wa mgonjwa.
Hii ndiyo dayalisisi inayopendwa na kutumika sana.Kwa njia hii damu husafishwa kwa mashine na maji ya dayalisisi.
Dayalisisi ya Damu hufanywaje?
Sana sana dayalisisi ya damu hufanyika katika vituo vya dayalisisi chini ya uangalizi wa daktari,wauguzi na mafundi wa mitambo ya dayalisisi.
- Mashine ya dayalisisi husukuma kama mililita mia tatu ya damu kwa dakika kutoka mwilini hadi kwenye sehemu ya mashine ya kusafisha kupitia tyubu au kifuko chepesi.Dawa ya heparin huendelea kuwekwa ili damu isigande.
- Sehemu ya mashine ya kusafisha ni kama figo bandia ambayo huchuja maji yasiyohitajika mwilini pamoja na uchafu.Husafisha damu kwa kutumia maji maalumu yanayotayarishwa kwa mashine hiyohiyo ya dayalisisi.
- Punde damu inaposafishwa tu, mashine huirudisha mwilini.
- Dayalisisi ya damu hufanywa kwa kawaida mara tatu kwa wiki na huchukua muda wa kama saa nne.
Damu hutolewa na kurudishwa vipi?
Njia tatu za kufikia damu kwa mishipa ni kupitia kwenye katheta iliyounganishwa na mshipa mmoja mkubwa; pili, mshipa mkubwa na mdogo kuunganishwa moja kwa moja na tatu kipandikizi cha plastiki kutumiwa kuunganisha mishipa hii.
Hemodialisis ni usafishaji wa damu unaopendwa sana kwa kutibu figo iliyo katika hatua ya mwisho ya ugonjwa.
1. Njia ya katheta kuunganishwa na mshipa mmoja
mkubwa
- Ili kuanza dayalisisi mara moja,njia ya kuingiza katheta au kifuko
kwenye mshipa wa damu ndiyo njia bora na hutumiwa kwa
wingi.
- Njia hii ni nzuri ya kutumiwa kwa muda mfupi-kabla njia ya
mshipa mdogo kuunganishwa kwenye mshipa mkubwa moja
kwa moja au ile njia ya mishipa kuunganisha na tyubu ya plastiki
kutengenezwa.
- Katheta huingizwa kwenye mshipa mkubwa shingoni,kifuani au
mguuni karibu na kinena. Kwa kutumia katheta hii zaidi ya 300ml za
damu kwa dakika huweza kutolewa ili isafishwe.
- Katheta huwa ni kifuko au tyubu iliyo na midomo miwili.Damu
huingilia mdomo mmoja na kuingia kwenye mashine ya
dayalisisi,kisha hurudishwa mwilini kupitia mdomo wa pili.
- Katheta zinazounganishwa na mishipa haziwezi kutumiwa kwa muda
mrefu kwa sababu ya hatari ya kuchafuka na damu kuganda.
- Kuna aina mbili za katheta:zile zenye upenyo ambazo zinaweza
kutumika kwa miezi kadha na zisizo na upenyo ambazo hutumika
kwa wiki kadha tu.
2. Njia ya mshipa mkubwa(ateri)kuunganishwa kwa mshipa
mdogo(vena)-Nasuri ya AV
- Njia ya Nasuri ya AV ndiyo mara
nyingi hutumika kwa dayalisisi ya
muda mrefu kwani hudumu na ni
vigumu kupata uchafu au damu
kuganda.
- Kwa njia hii ateri na vena hupasuliwa
na kuunganishwa.kwa kawaida njia
hii hutengenezwa kwenye mkono
karibu na kifundo cha mkono.
- Damu nyingi hutoka mshipa mkubwa
wa ateri na kuingia kwenye mshipa
mdogo wa vena,kwa nguvu
nyingi.Baada ya wiki kadhaa au
miezi,mshipa mdogo wa vena
hupanuka na kubeba damu nyingi.Njia
hii ya Nasuri ya AV huchukua muda kupanuka na kuwa tayari
kutumika.Haiwezi kutumiwa kufanya dayalisisi mara moja.
- Sindano kubwa huingizwa kwenye mshipa ili kupeleka damu kwenye
sehemu ya mashine ya kuisafisha na nyingine ya kurudisha damu
iliyosafishwa mwilini.
- Njia hii huweza kudumu kwa miaka mingi ikitunzwa vyema.shughuli
zote za kawaida zinaweza kufanywa kwa mkono ulio na Nasuri ya
AV.
Kwa nini Nasuri ya AV huhitaji utunzaji maalum?
- Maisha ya mtu aliye katika kipindi cha mwisho cha ugonjwa wa figo
hutegemea dayalisisi ya mara kwa mara ili kusafisha damu.Damu ya
kutosha inafaa kuweza kupitia mshipa uliotengenezwa, ili
isafishwe.kwa hivyo,njia ya Nasuri ya AV ni tegemeo la uhai la mtu
anayehitaji dayalisisi wakati wote.Kutunza Nusuri ya AV huhakikisha
kuwa damu ya kutosha inaweza kutolewa na kwa siku nyingi.
- Damu nyingi hupitia kwenye mishipa ya AV kwa kasi / nguvu
nyingi.Mishipa hii ikiumia mtu anaweza kutokwa na damu nyingi sana
na kuhatarisha maisha yake.Kwa hivyo ni muhimu kulinda mishipa
hii.
Njia za kutunza mishipa yenye njia ya kutolea damu( Nasuri
ya AV)
Tahadhari muhimu za kuhakikisha kuwa mishipa inaweza kutoa damu
ya kutosha na kwa muda mrefu.Tahadhari hizi ni kama zifuatazo.
Zuia maambukizi
Linda Nasuri ya AV
- Hakikisha kuwa mkono ulio na Nasuri ni safi wakati wote na kabla
ya kila dayalisisi.
- Tumia Nasuri ya AV kwa dayalisisi pekee.Usikubali yeyote atumie
njia hii kudunga sindano,kutoa damu wala kupima shinikizo la
damu kutumia mkono huu.
- Chunga mishipa iliyo na Nasuri .Usivae bangili,nguo iliyobana mkono
wala saa kwenye mkono huu.Mkono huu ukijeruhiwa , hata kwa
bahati mbaya,damu nyingi itatoka na kuhatarisha maisha. Kudhibiti
kutokwa na damu,bana mahali panapotoka damu kwa nguvu
ukitumia mkono mwingine au bendeji.Damu ikikoma kutoka,Ongea
na/mfahamishe daktari wako mara moja.Usijaribu kukimbia
hospitalini damu inapotoka kwani hii ni hatari.Jaribu mara moja
Nasuri ya AV ndilo tegemeo la uhai la wagonjwa wa figo.Bila
njia hii dayalisisi ya damu haiwezi kufanywa kwa muda mrefu.
kuzuia kupoteza damu nyingi zaidi kwa kufunika na kubana
panapotoka damu.
- Usiinue kitu kizito kwa mkono ulio na Nasuri ya AV wala usiufinye
Tahadhari usiulalie mkono huu.
Hakikisha kwamb a mishipa ya Nasuri ya AV inafanya kazi
- Pima mtiririko wa damu katika Nasuri ya AV kwa kusikiliza mtetemo
wa damu mara tatu kwa siku (kabla ya kiamshakinywa, chakula
cha mchana na chakula cha j ioni).Iwapo mtetemo
hausikiki,mfahamishe daktari wako au kituo cha dayalisisi mara
moja.Kujua mapema kama Nasuri ya AV imeziba na kuitoa damu
iliyoganda kunaweza kuiokoa Nasuri ya AV.
- Shinikizo la damu lililo chini linaweza kukwamisha mishipa ya Nasuri
ya AV kupeleka damu kwa hivyo ni muhimu lizuiwe.
Mazoezi
Mazoezi ya mara kwa mara yanaweza kusaidia njia ya Nasuri ya AV
kukomaa haraka.Hata baada ya kuanza dayalisisi ni muhimu
kuendelea kufanya mazoezi ili kuimarisha mishipa hii.
3. Njia ya Kipandikizi au kiunganishi
- Kiunganishi kati ya mshipa mkubwa wa ateri na mdogo wa vena ni
njia nyingine inayoweza kutumiwa iwapo mishipa midogo haitoshi
kwa Nasuri ya AV au njia ya Nasuri ya AV imeshindwa kufanya
kazi.
- Katika njia hii,mshipa wa ateri huunganishwa na mshipa wa vena
kwa kutumia kifuko au tyubu fupi nyororo inayowekwa chini ya
ngozi.Sindano huingizwa kwa kipandikizi hiki wakati wa matibabu
ya dayalisisi.
Ni muhimu kutunza mishipa ya Nasuri ya AV ili kuhakikisha
inatoa damu ya kutosha na pia inatumika kwa muda mrefu.
- kilinganishwa na ile ya Nasuri ya AV ambapo mshipa mkubwa wa
ateri huunganishwa moja kwa moja na mshipi mdogo wa vena,njia
ya kipandikizi ina hatari zaidi ya damu kuganda,kupata maambukizi
au kuchafuka,na haidumu kama njia ya Nasuri ya AV.
Kazi za mashine ya dayalisisi ni zipi?
Kazi muhimu za mashine ya dayalisisi ni kama zifuatazo:
- Mashine hii husukuma damu na kufuatia mtiririko wa damu kutoka
mwilini hadi kwenye mashine inaposafishwa damu.
- Mashine hutengeneza maji maalumuya kusafisha damu.Mashine
hufuatia na kusawazisha joto,kiasi na kasi ya maji ya dayalisisi
ambayo yanafaa kulinganishwa na mahitaji ya mgonjwa kwa
uangalifu mkubwa. Maji haya hutoa uchafu na maji yasiyohitajika
mwilini.
- Kwa usalama wa mgonjwa,mashine ya dayalisisi ina vifaa tofauti
vinavyoweza kugundua uvujaji wa damu kutoka kwenye mashine
au kuwepo kwa hewa katika mzunguko wa damu.
- Kwa mashine zilizo na kompyuta, mashine hizi huonyesha vipimo
mbalimbali na huonya iwapo kuna kasoro huhakikisha hakuna
matatizo,kuna usahihi, usalama na kufuatiliwa wakati wote dayalisisi
inapofanywa.
Muundo wa sehemu ya mashine inayosafisha damu na
jinsi inavyofanya kazi?
- Katika dayalisisi sehemu hii ni kichungi(figo bandia)ambacho
husafisha damu.
- Kichungi hiki huwa na urefu wa sentimita kama ishirini hivi na
upana wa kama sentimita tano.Ni silinda ya plastiki yenye maelfu
ya nyuzi kama tyubu zenye utando unaoweza kupenyeka.
Mashine ya dalisisi, ikisaidiana na maji ya dialiaza, huchuja
damu na hudumisha ugiligili,kiasi cha madini na asidi mwilini.
- Nyuzi hizi huungana
upande wa juu na wa
nchini wa silinda na
kutengeneza ‘chumba
cha damu’.Damu
huingia chumba hiki
kwa mdomo mmoja
na kutoka kwa
mdomo wa pili baada
ya kusafishwa.
- Maji ya dayalisisi
huingi lia mdomo
mmoja,huzunguka nje
ya nyuzi na
kutengeneza chumba cha maji na kutokea kwa mdomo mwingine.
Usafishaji wa damu katika mashine
- Katika dayalisisi,damu inayosukumwa na mashine huingia kwa
mdomo mmoja na husambazwa kwenye nyuzi zinazofanana na
mishipa midogomidogo kabisa ya damu.
- Kwa kila dakika,karibu mililita mia tatu ya damu na mililita mia sita
ya maji ya dayalisisi hutiririka kutoka pande zote mbili za
mashine.Utando wa nyuzi unaotenga damu na maji hupenyeka (
semi-permeable)na hivyo kuwezesha uchafu na maji yasiyohitajika
kutoka na kuingia kwenye‘chumba cha maji’.
- Damu hutokea mwisho huo mwingine wa mashine baada ya
kusafishwa.Maji yenye uchafu uliotolewa kwenye damu nayo
hutokea kwenye upande wa mashine ambao damu huingilia.
- Kwa njia hii damu yote ya mwili husafishwa mara kumi na mbili
hivi.Mwishoni mwa kazi hii ya saa nne,yurea ya damu,maji
yasiyohitajika, kreatinini na chumvichunvi (electrolytes) hupungua
sana.
Je,maji ya dayalisisi ni nini na kazi yake ni ipi?
- Maji haya ni maalum na hutumika kutoa uchafu na umajimaji
usiohitajika kwenye damu.
- Maji haya kwa kawaida hufanana na maji ya kawaida yaliyoko mwilini
lakini huweza kubadilishwa kulingana na mahitaji ya mgonjwa.
- Maji hutengenezwa na mashine ya dayalisisi kwa kuchanganya
sehemu thelathini za maji yaliyosafishwa kwa hali ya juu na sehemu
moja ya dawa ya dayalisisi(30.1).
- Dawa hii ni maji maalum yanayouzwa kwenye chupa na huwa
yamekolea chumvichumvi (electrolytes), madini na bikabonati.
- Ili kutayarisha maji ya dayalisisi,maji ya kawaida yanayoingia kwenye
mashine husafishwa kwa njia kadha kwa kutumia kichungi cha
changarawe na cha makaa,kutoa chumvi chumvi na njia zingine za
kisayansi kama vile reverse osmosis, deionization, na kuchuja kwa
miale ya ultra violet.(ultra violet filtration).
- Maji yaliyosafishwa kiasi hiki huwa hayana vumbi,uchafu mwingine
unaoelea,uchafu wa kikemikali,madini, bacteria au sumu za ndani
(endo-toxins) .
- Maji yaliyosafishwa kwa hali ya juu ni muhimu kwa usalama wa
dayalisisi kwani karibu lita mia moja na hamsini hutumiwa kwa kila
dayalisisi.
- Ili kumkinga mgonjwa na hatari ya uchafu wa maji,lazima maji
yasafishwe kwa umakini mkubwa na pia yaendelee kuangaliwa
yanapotumiwa.
Dayalisisi ya damu hufanywa wapi?
Kwa kawaida,dayalisisi ya damu hufanywa hospitalini au kwenye kituo
cha dayalisisi chini ya wahudumu waliohitimu wakiongozwa na
daktari.Kwa wagonjwa wachache,dayalisisi huweza kufanywa
nyumbani.Hii huwezekana tu kwa wagonjwa ambao hali yao imeimarika
na huhitaji mafunzo mazuri,usaidizi wa familia, nafasi ya kutosha na
fedha za kutosha.
Je, dayalisisi ina uchungu/maumivu? Mgonjwa hufanya nini
wakati wa dayalisisi?
Hapana.Dayalisisi haina uchungu isipokuwa wakati sindano
inapoingizwa.Mgonjwa anayefanyiwa dayalisisi ya kawaida huenda
hospitalini na kurudi nyumbani baada ya dayalisisi.
Kwa kawaida wagonjwa hupumzika au hulala wakati wa saa nne za
dayalisisi.Wanaweza pia kusoma,kusikiliza muziki, au hata kutazama
runinga.Wakati wa dayalisisi wagonjwa hupendelea kupewa
viburindisho vyepesi au vinywaji baridi.
Dayalisisi ina matatizo yapi?
Matatizo ya kawaida wakati wa dayalisisi huwa kama shinikizo la
Maji ya dialisi hurekebisha na kuleta usawa wa madini mwilini kwa
kuondoa uchafu wakati wa kusafisha damu kwa hemo dialisisi.
damu kwenda chini (hypotension),kichefuchefu au kutapika,mkakamao
wa misuli (cramps), uchovu na kuumwa na kichwa.
Faida na kasoro za dayalisisi ya damu:
Faida za dayalisisi ya damu
- Hufanywa na wauguzi waliohitimu au mafundi wa dayalisisi,kwa hiyo
huwa salama na isiyo na usumbufu kwa wagonjwa.
- Dayalisisi ya damu ni haraka na yenye utendaji bora kwa hiyo
huchukua muda mfupi kuliko dayalisisi ya tumbo.
- Dayalisisi ya damu huwezesha wagonjwa kukutana na wengine walio
na shida kama zao.Utangamano huu hupunguza mfadhaiko na
mgonjwa anaweza kufurahia uwepo wa wagonjwa wenzake.
- Humpa mgonjwa uhuru zaidi kwani hufanywa kwa siku tatu tu kwa
wiki.
- Hatari ya maambukizo ni kidogo.
- Dayalisisi ya damu ni rahisi ukilnganisha na ya tumbo katika vituo
vingi.
Matatizo Ya Dayalisisi Ya Damu
- Usumbufu wa mgonjwa kwenda mara kwa mara kwenye kituo cha
dayalisisi na hasa kama kituo hicho kipo mbali.
- Mgonjwa lazima apange ili atimize mahitaji / matakwa ya mpango
mzima wa dayalisisi.
- Udungwaji wa sindano una maumivu.
- Mgonjwa hana uhuru wa vyakula- Mgonjwa aliye kwenye dayalisisi
ya damu lazima afuate maelekezo ya maji (fluids), chumvi,potasiam,
na pia vyakula vilivyo na fosfarasi nyingi.
Faida kuu za dayalisisi ya damu ni usalama,ubora na
haina usumbufu.
- Wagonjwa wanaofanyiwa dayalisisi ya damu wana hatari zaidi ya
kupata /kuambukizwa homa ya maini.
Vitu Gani Wagonjwa Wa Dayalisisi Wafanye Na Vipi
Wasifanye
- Wagonjwa walio na ugonjwa sugu wa figo (ESKD)na ambao
wanatibiwa kwa dayalisisi, wanahitaji kwenda kufanyiwa dayalisisi
mara tatu kwa juma bila kukosa. Kwenda kufanyiwa dayalisisi ni
muhimu kwa afya njema kwa muda mrefu, kutokufuata maelekezo
ya kufanyiwa dayalisisi ni hatari na kunaweza kusababisha hata kifo.
- Kutokunywa maji mengi (fluids) na kula chumvi ni muhimu ili kuzuia
ongezeko la uzito hasa katikati ya miula ya dayalisisi. Mgonjwa asile
vyakula vilivyo na potasiam na fosforasi nyingi. Ale protini zaidi.
- Utapiamlo hutokea mara nyingi kwa wagonjwa walio kwenye
dayalisisi na ikitokea hivyo maendeleo yao hayawi mazuri : wanaweza
hata kupoteza maisha. Kutokula protini yakutosha na upotevu wa
protini wakati wa dayalisisi, upelekea mgonjwa kuwa na utapiamlo.
Kwa hiyo mgonjwa aliye kwenye dayalisisi ale chakula chenye protini
na chakula kinacholeta nguvu barabara.
- Wagonjwa wa dayalisisi wanafaa kupewa vitamini zinazoweza
kuyeyuka kwenye maji kama vile B na C. Wasishauriwe kununua
dawa za vitamini madukani kwani zinaweza kuwa hazina ubora,
hazina vitamini zote zinazohitajika au iwe vitamini zilizomo si za
kutosha kwa mgonjwa wa dayalisisi,au pengine ziwe na vitamini
zenye madhara kama vile A, E na K au madini.
- Madini ya kalsiamu (iliyo kwenye mifupa na meno) na vitamini ya D
vinaweza kupatiwa mgonjwa kutegemea viwango vya madini alivyo
Kizuizi/ugumu mkubwa wa hemodialisisi ni mgonjwa
kuhitajika kwenda hospitali mara tatu kila juma.
navyo (ikiwa pamoja na kiasi cha kalsiam,fosfarasi, na kiwango
cha parathairoid homoni).
- Lazima mgonjwa azingatie ushauri kama kuzuia kunywa
pombe,kutovuta sigara,kudumisha uzito unaofaa,kufanya mazoezi
na kadhalika.
Ni wakati gani mgonjwa inafaa amwone muuguzi au
daktari?
Mgonjwa aliye kwenye dayalisisi inafaa amwone muuguzi wa dayalisisi
au daktari wake mara moja iwapo:
- Anatokwa na damu kwenye mkononi wenye Nasuri ya AV au mahali
katheta imewekwa.
- Mtetemo wa mtiririko wa damu hausikiki kwenye mkono ulio na
Nasuri ya AV.
-
- Uzito ukiongezeka ghafla,kuvimba au akiwa na shida ya kupumua.
- Maumivu ya kifua na mdundo wa moyo usio wa kawaida.
- Shinikizo la damu kuwa juu zaidi au chini zaidi.
- Mgonjwa kuchanganyikiwa,kuzimia au kusinzia.
- Mgonjwa anahisi baridi sana na kutetemeka,kutapika sana au
kutapika damu au/na kukosa nguvu kwa ujumla.
Dayalisisi Ya Tumbo
Dayalisisi ya tumbo,hii ni njia nyingine ya dayalisisi kwa wagonjwa
walio katika kipindi cha mwisho cha ugonjwa wa figo
(ESKD).Hutumika sana nyumbani.
Dayalisisi ya tumbo ni nini?
- Dayalisisi hii hufanywa kupitia utando(membrane) unaozunguka
tumbo,matumbo na sehemu zingine za tumbo.
Kwa wagonjwa wa hemodialisisi uzuiaji wa maji na chimvi
ni muhimu ili uzito usiongezeke hasa kati ya dialisisi.
- Utando huu wa tumbo una ruhusu kupenyeza uchafu na sumu ulio kwenye damu kupitia kwake na kuutoa.
- Dayalisisi ya tumbo ni njia ya kusafisha damu kupitia kwenye utando huu.
Aina za dayalisisi ya tumbo
1. Dayalisisi ya vipindi vifupi vifupi.(IPD)
2. Dayalisisi ya wakati wote.(CAPD)
3. Dayalisisi inayojiendesha.(CCPD)
1. Dayalisisi ya vipindi vifupi vifupi (Intermittent Peritoneal Dialysis - IPD)
Aina hii ya dayalisisi ya tumbo ni bora kwa wagonjwa walio hospitalini wanaohitaji dayalisisi kwa muda mfupi tu.Hutumika sana kwa watu wenye ugonjwa wa figo wa muda,kwa watoto na katika hali ya dharura kwa wagonjwa walio katika kipindi cha mwisho cha ugonjwa wa figo.
- Katika njia hii,katheta ya plastiki yenye vishimo vingi huwekwa kwenye tumbo pamoja na maji maalum ya dayalisisi.
- Dayalisisi hii hufanywa kwa muda wa saa 24 hadi saa 36 na takriban lita thelathini au arobaini za maji maalum ya dayalisisi hutumika kwa kila kipindi cha matibabu.
- Dayalisisi aina hii hurudiwa baada ya kati ya siku moja hadi tatu kulingana na mahitaji ya mgonjwa .
CAPD ni aina ya dialisisi inayoweza kufanywa na mgonjwa mwenyewe nyumbani akitumia maji maalumu (special fluid).
2. Dayal isisi ya wakati wote.(Continous Ambulatory Peritoneal Dialysis - CAPD)
- Dayalisisi hii hufanywa kwa mfululizo,saa ishirini na nne za siku na siku saba za wiki.
- Mgonjwa anaweza kutembea na kufanya shughuli za kawaida.
- Utando wa tumbo ndio hutumika kama kichungi.
Njia hii inaweza kutumiwa na mgonjwa nyumbani bila ya kutumia mashine.kwa sababu njia hii inampa mgonjwa uhuru wa kuendelea na shughuli zake. Hutumiwa sana katika nchi zilizoendelea.
Hufanywaje?
Njia hii ya dayalisisi hutumia katheta nyepesi na laini yenye vishimo vingi . Katheta hii huingizwa kwa njia ya upasuaji kwenye tumbo la mgonjwa. Katheta hii ni njia ya kudumu ya dayalisisi.Huingizwa kwenye tumbo kama inchi moja (1") chini na kwa upande wa kitovu.Katheta huwekwa siku kumi hadi kumi na nne kabla ya dayalisisi kuanza.kama vile Nasuri ya AV, katheta hii ndiyo ‘tegemeo la uhai’ la mgonjwa.
Hatua za dayalisisi ya wakati wote
Njia hii ya dialisisi ina hatua tatu: kujaza,kukaa na kutoa maji.
Kujaza: kupitia katheta,lita mbili za maji ya dayalisisi ya tumbo yaliyowekwa kwenye mfuko safi kabisa hutiririshwa tumboni.Maji haya yakishawekwa tumboni huwa yanagusana na utando wa tumboni (peritoneum). Mfuko wake mtupu hukunjwa na kuwekwa kwenye nguo ya ndani ya mgonjwa hadi wakati mwingine wa matibabu.
Kukaa: Maji ya dayalisisi hukaa tumboni kwa saa nne hadi sita wakati wa mchana na saa sita hadi nane wakati wa usiku. Wakati ambapo maji yaliyowekwa kwenye hatua ya kujaza na yapo tumboni, huitwa wakati waKUKAA. Huu ndio wakati damu inasafishwa .Utando wa tumbo ndio huwa kama kichungi kinachoruhusu uchafu kupita kutoka
CAPD iendeshwe kwa uangalifu na usafi mkubwa kila siku kwa wakati uleule hata wakati wa sikukuu.
kwenye damu na kuingia kwenye maji . Wakati haya
yanapoendelea,mgonjwa yuko huru kutembea.
Kutoa maji:
Baada ya kukaa,maji ya dayalisisi yaliyo na uchafu
hutolewa kupitia katheta na kuingia kwenye mfuko uliowekwa kwenye
nguo ya ndani ya mgonjwa. Mfuko uliokusanya maji hupimwa uzito
na baadae kutupwa Maji yaliyokusanywa yanapaswa yasiwe na rangi
yoyote.
Kutoa maji tumboni na kujaza maji mapya huitwa kubadilisha.
Kunawezwa kufanywa mara tatu hadi tano wakati wa mchana na
mara moja wakati wa usiku.Wakati wa usiku,kubadilisha hufanywa
kabla ya mgonjwa hajalala na maji huachwa tumboni usiku
kucha.Shughuli hii lazima ifanywe kwa mazingira na njia ya usafi kabisa.
3. Dayalisisi inayojiendesha.
Hii ni dayalisisi inayoendelea wakati wote kwa kutumia
mashine.Hufanyw anyumbani.Mashine
Dialisisi inayojiendesha hujaza na kutoa maji ya dayalisisi tumboni.kila
mzunguko wa kujaza na kutoa huchukua kama saa moja hadi mbili na
kubadilisha hufanyika mara nne au tano.kazi hii yote huchukua muda
wa kama saa nane hadi kumi mgonjwa alalapo usiku.Mashine
inapotolewa asubuhi,lita mbili hadi tatu za maji ya dayalisisi huachwa
tumboni.Maji haya hubaki tumboni hadi jioni yanapotolewa na
mashine kuwekwa tena.
Faida kuu za njia hii ni kuwa na uhuru wa kufanya shughuli za
kawaida za mchana na kwamba mashine huwekwa mara moja na
kutolewa mara moja tu kwa siku.Hii humwezesha mgonjwa kupumzika
na hupunguza hatari ya utando wa tumbo kupata maambukizi
Dialisisi ya peritoni hufanyika nyumbani kwa kutumia mashine
maalumu inayojiendesha, (automated cycler machine).
yanayosababisha kuvimba.(peritonitis). Lakini ikumbukwe njia hii ni
ghali.
Maji yanayotumika katika dayalisisi ya kudumu au wakati
wote ni yapi?
Maji yanayotumika huwa ni maji safi kabisa yenye madini na sukari(
glukosi) yanayotumika katika dayalisisi.Kutegemea kiwango cha
Sukari,maji haya huwa yana nguvu tofauti.kuna yenye kiwango cha
asilimia 1.5% ,2.5 % na 4.5%. Glukosi iliyo kwenye maji haya ndiyo
huwezesha maji kutolewa mwilini.Maji yenye nguvu tofauti hutumiwa
kulingana na kiwango cha maji yanayohitajika kutolewa mwilini.Iwapo
maji mengi yanahitajika kutolewa mwilini basi maji ya dayalisisi yenye
nguvu zaidi hutumiwa.
Sasa kuna aina mpya ya maji ya dayalisisi yenye nguvu zaidi
yanayotumika. Maji haya huitwa icodextrin na hutumika badala ya
dextrose. Faida ya maji haya mapya ni kuwa huweza kutoa maji
yasiyohitajika mwilini polepole. Maji haya mapya ya dayalisisi pia ni
mazuri hasa/hata kwa watu wenye kisukari au wenye uzito mkubwa.
Matumizi yake huwa ni ya mzunguko mmoja tu kwa siku. Hupatikana
kwenye mifuko ya mililita elfu moja hadi elfu mbili mia tano.
Matatizo ya dayalisisi ya wakati wote au ya kudumu.
1. Maambukizi
Tatizo kubwa sana kwa mgonjwa anayefanyiwa dayalisisi hii huwa ni
ugonjwa wa uvimbe wa utando uliozunguka sehemu za ndani za
tumbo(fumbatio),maumivu ya tumbo,dalili za homa,kibaridi na maji ya
dayalisisi kuonekana machafu yanapotoka mwilini zote huwa ni dalili
za ugonjwa huu wa uvimbe wa fumbatio. Ili kuzuia ugonjwa huu,lazima
dayalisisi ifanywe kwenye mazingira safi kabisa na kuhakikisha kuwa
mgonjwa hafungi choo.Matibabu yake huwa ni pamoja na dawa za
antibayotiki.Maji ya Dayalisisi yanayotoka mwilini yapimwe ili kujua
dawa sahihi zitakazofaa kutumiwa na kwa wagonjwa wengine katheta
hutolewa, kwani mahali katheta ilipoingizwa panaweza kuwa ndiyo
chanzo cha maambukizi.
Matatizo mengine
Kuvimba tumbo,kudhoofika kwa misuli ya tumbo na kusababisha
ngiri,maji kuzidi mwilini,mfuko wa korodani kuvimba/kujaa maji,kufunga
choo,kuumwa na mgogo,maji kutotoka vizuri,maji ya dayalisisi kuvuja
na mgonjwa kuongeza uzito.
Faida za dayalisisi ya wakati wote
- Masharti ya vyakula na vinywaji huwa si makali sana.
Uangalifu mkubwa unahitajika ili kuzuia maambukizi
kuwapata wagonjwa wanaofanyiwa dayalisisi ya kudumu.
- Mgonjwa huwa huru zaidi kwani dayalisisi inaweza kufanyika
nyumbani,kazini na hata anaposafiri. Shughuli za kawaida huweza
kuendelea wakati dayalisisi inapofanyika.Mgonjwa anaweza
kujifanyia dayalisisi kwani hahitaji mashine, wala daktari,wala jamaa.
- Mgonjwa hana haja ya kwenda hospitalini mara tatu kama
kawaida,wala kusafiri wala kudungwa sindano.
- Shinikizo la damu na anemia huzuilika kwa njia bora zaidi.
- Njia hii huwezesha damu kuendelea kusafishwa wakati wote kwa
hivyo hakuna usumbufu.
Mapungufu wa dayalisisi ya kudumu
- Hatari ya maambukizi kwenye utando wa tumboni au panapopitia
katheta.
- Mgonjwa anatakiwa kubadilisha mara tatu hadi tano kila siku ya
maisha yake(exchange) Kuzingatia maagizo na usafi wa hali ya juu
kila wakati, hii si kazi rahisi.
- Kuwa na katheta na maji tumboni kila wakati haina raha na pia,wengi
huwa hawapendi jinsi mwili unavyoonekana.
- Sukari iliyo katika maji ya dayalisisi inaweza kumfanya mgonjwa
aongeze uzito au kuwa na sukari zaidi mwilini.
- Kuiweka mifuko mizito ya dayalisisi nyumbani si rahisi.
Mashauri ya mlo
Ushauri wa vyakula kwa mgonjwa anayefanyiwa dayalisisi kwa
mashine inayojiendesha huwa muhimu sana.pia, huwa tofauti na ule wa
anayefanyiwa dayalisisi ya damu kupitia kwenye mishipa.
- Vyakula vyenye protini nyingi ni muhimu ili kuzuia ukosefu wa
Faida kubwa ya CAPD ni uhuru wa mahali na wakati na pia
makatazo ya vyakula ni kidogo.
protini mwilini kwa sababu ya kupoteza protini nyingi katika
dayalisisi ya tumbo.
- Zuia vyakula vyenye joto jingi ili kuzuia kuongeza uzito ,maji ya
dayalisisi huwa na sukari ya glukosi ambayo huzidi kuongeza
kabohaidriti kwa mwili wa mgonjwa.
- Masharti ya matumizi ya chumvi na vinywaji ni mepesi hapa kuliko
kwa wagonjwa wanaofanyiwa dayalisisi kwenye mishipa ya damu.
- Kuzuia vyakula vyenye potasiamu na fosfati.
- Ale zaidi vyakula vyenye nyuzinyuzi ili kuzuia kufunga choo.
Ni wakati gani mgonjwa aende kwa daktari au muuguzi
wake wa dayalisisi?
- Akipata maumivu ya tumbo,dalili za homa au kutetemeka.
- Iwapo maji ya dayalisisi yanayotoka mwilini yanaonekana machafu
au yana damudamu.
- Uchungu,usaha,wekundu,kuvimba au joto mahali ambapo katheta
inatokea.
- Mtiririko wa maji (fluid) ndani au nje ya tumbo umeziba au mgonjwa
hapati choo (constipation).
- Kuongeza uzito ghafla, kuvimba mwili,kushindwa kupumua au
shinikizo la damu kuwa juu sana (inahashiria kuongezeka ghafla kwa
maji mwilini).
- Shinikizo la damu la chini,kupungua uzito, mkakamao wa misuli
(cramps) au kizunguzungu. (kunahashiria upungufu wa maji –fluid).
Wagonjwa wa dayalisisi ya wakati wote sharti wale vyakula
vyenye protini nyingi ili kuzuia maambukizi na utapiamlo.