19: Ugonjwa wa mawe kwenye figo

Ugonjwa wa figo wamawe umeenea sana.Husababisha maumivu makali sana.Wakati mwingine mawe ya figo hayaonyeshi dalili zozote.Ugonjwa huu husababisha maambukizi na hudhuru figo kwa wagonjwa wengine,iwapo hautibiwi haraka.Mawe yatokeapo huwa ni rahisi kurudia tena kwa hiyo ni muhimu kuelewa , jinsi ya kuzuia na kukabiliana na ugonjwa huu.

Jiwe la figo ni nini?

Jiwe la figo ni fuwele kigumu kinachofanana na jiwe kilicho ndani ya sehemu za mfumo wa mkojo(njia za mkojo na kibofu)au kwenye figo.Fuwele hii hutokana na chembe za kalsiumu, oxalale, urate, fospati na nyinginezo zilizo kwenye mkojo.Mamilioni ya chembe hizi hujikusanya na huendelea kukua na mwishowe huwa kama jiwe.

Kwa kawaida ,mkojo huwa na kitu kinachozuia chembe kugandamana na kitu hiki kinapopungua ndipo mawe hutokea.Ni muhimu kuelewa kuwa mawe ya figo ni tofauti na yale ya kibofu cha mkojo, na ni tofauti na mawe ya ini.

Je,mawe ya figo huwa ya kiasi,na umbo gani na hutokea wapi?

Mawe ya figo huwa na umbo na kiasi tofauti.Yanaweza kuwa madogo kuliko changarawe au kubwa kama mpira wa tenisi. Umbo la jiwe la figo linaweza kuwa la mviringo au umbo la yai. Linaweza kuwa laini, ambapo halisababishi maumivu makali na huweza kutoka lenyewe.I wapo umbo lake ni laini, na umbo lake si laini (irregular/jagged) uleta maumivu na huwa mengi na ni vigumu kutoka lenyewe. Jiwe linaweza kutokea popote katika sehemu za njia ya mkojo lakini mara nyingi hutokea kwenye figo kisha huteremka hadi kwenye njia ya mkojo iliyo katikati ya figo na kibofu cha mkojo, kwenye ureta.

Jiwe kwenye mfumo wa mkojo ni chanzo muhimu cha maumivu makali na yasiyovumilika ya tumbo.

Aina

Aina za mawe ya figo

Kuna aina nne ya mawe ya figo:

1. Aina ya kwanza ni yale mawe hutokea wakati mkojo una asidi nyingi. Haya ndiyo mawe ambayo hutokea mara nyingi kuliko mengine yote.Asilimia sabini hadi themanini huwa ni ya aina hii. Mawe haya huwa na asili ya calcium oxalate au calcium phosphate.(Calcium stones ).

2. Mawe yanayotokana na maambukizi kwenye figo.Huwa nadra (hutokea kama kwa asilimia kumi hadi kumi na tano),hupatikana sana /zaidi kwa wanawake (Struvite stones ).

3. Mawe ambayo hutokea mkojo unapokuwa na asidi nyingi ya aina ya yuriki,inayotokana na kula nyama nyingi,kuishiwa na maji au kutibiwa saratani.Aina hii ya mawe huwa haiwezi kuonekana kwa picha za ekserei.Asilimia kama tano hadi kumi ya mawe huwa ya aina hii (Uric Acid Stones ).

4. Aina ya mawe ambayo hutokana na kurithi.Hali hii hupitishwa kutoka kwa wazazi hadi vizazi vyao.Mawe haya huambatana na ugonjwa wa cystinuria. Kiasi cha “cystine”kwenye mkojo huwa juu(cystine stones ).

Jiwe la pembe za kulungu

Jiwe hili huwa kubwa sana na huchukua nafasi kubwa kwenye figo.Hufanana na pembe za kulungu. Halisababishi maumivu na mara nyingi halitambuliki na hivyo mwishowe huharibu figo.

Mawe ya kwenye mfumo wa mkojo hutokea zaidi kwenye figo na mshipa wa ureta.

Nini husababisha mawe ya figo?

Kila mtu anaweza kupata mawe kwenye figo.Hata hivyo, kuna mambo kadha yanayochangia hali hii:

  • Kutokunywa maji ya kutosha.
  • Historia ya familia kupata mawe ya figo.
  • Kula vyakula vyenye nyama, sodiam, oxalate na maziwa mengi na kukosa mboga na matunda.
  • Asili mia 75% ya mawe kwenye figo na asili mia 95% ya mawe kwenye kibofu cha mkojo huwapata wanaume kati ya umri wa miaka ishirini na sabini na sanasana walio na uzito mkubwa.
  • Watu wanaoishi sehemu kavu/kame zenye joto jingi.
  • Watu ambao hawajiwezi na muda mwingi wamelala (bed ridden/ immobile).
  • Maambukizi ya njia ya mkojo ya mara kwa mara,au kuzibika kwa njia ya mkojo.
  • Magonjwa kama ya tezi dundundio(thyroid), jongo, na mengineyo yanayotokana na kasoro katika uvunjajivunjaji wa kemikali mwilini.
  • Matumizi ya dawa fulani fulani kama vile za kukojoa au za kuzuia asidi(diuretics na antiacids).
Kutokunywa maji mengi na historia ya familia ya kuwa na mawe kwenye figo ni viashiria viwili vikuu vya uwezekano wa kutengeneza mawe.

Dalili

Dalili za mawe katika mfumo wa mkojo ni nini?

Dalili zinazojitokeza hutofautiana kulingana na ukubwa wa jiwe,umbo na mahali lilipo.Dalili zenyewe huwa ni kama zifuatavyo:

  • Maumivu ya tumbo.
  • Kukosa dalili zozote na hali hii Hujulikana mtu anapopimwa kwa sababu nyingine. Haya mawe huitwa ‘mawe kimya’.
  • Kukojoa na kuhisi kutaka kukojoa kila mara.
  • Kichefuchefu na kutapika.
  • Kukojoa damu(haematuria).
  • Uchungu au kuwashwa unapokojoa.
  • Kama jiwe likikwama kwenye njia ya mkojo,mkojo hukatika ghafla wakati wa kukojoa.
  • Kukojoa jiwe.
  • Wakati mwingine jiwe husababisha matatizo kama maambukizi yanayo jirudia rudia kwenye njia ya mkojo, kufunga njia ya mkojo na hivyo kuleta madhara ya muda au ya kudumu kwenye figo ambayo yakakosa kurekebishika.

Maumivu ya tumbo yanayosababishwa na jiwe katika mfumo wa mkojo

  • Ukali ya maumivu huwa tofauti kati ya mtu mmoja na mwingine ikitegemea aina,ukubwa na mahali jiwe lilipo.Kumbuka maumivu hayalingani na ukubwa wa jiwe . Jiwe dogo lisilo laini husababisha maumivu makali kuliko jiwe kubwa ambalo ni laini.
  • Maumivu yanaweza kuwa si makali sana.Maumivu huzidi mtu anapogeuka na yanaweza kukaa kwa dakika au hata saa kadhaa kIsha yakaisha.Huja yakipotea.
  • Maumivu hutokea upande ulio na jiwe.Maumivu huanzia kwenye kiuno hadi kwenye kinena, yakiambatana na kichefuchefu na kutapika.
  • Jiwe kwenye kibofu pia husababisha maumivu kwa upande wa chini wa tumbo na maumivu wakati wa kukojoa sanasana kwenye uume.
  • Watu wengi wanapohisi maumivu ya ghafla hukimbilia suluhisho la tiba ya haraka.
Maumivu ya upande wa chini wa tumbo na kukojoa damu ni dalili kuu za mawe kwenye mfumo wa sehemu za mkojo.

Utambuzi

Je,mawe ya figo yanaweza kuharibu figo?

Ndio. Mawe kwenye figo au kwenye njia ya mkojo yanaweza kuzuia mkojo kutoka na basi kusababisha figo kupanuka (dilatation) .Figo ikipanuka kwa muda mrefu huishia kuharibika. Utambuzi wa mawe kwenye mfumo wa mkojo Uchunguzi hufanywe ili kutambua uwepo wa mawe, matatizo yanayoambatana na hali hii na pia kujua chanzo cha kuwepo kwa mawe haya.

Uchunguzi wa picha za eksirei : Picha za ultrasound huwa rahisi kupatikana, si ghali na hufanywa kwa njia rahisi.Ndizo mara nyingi hutumika kutambua mawe yaliyo kwenye mfumo wa mkojo na kujua kuwepo kwa kuziba.

Eksrei Ya KUB - Eksirei kutoka kwenye figo, njia ya mkojo hadi kwenye kibofu cha mkojo-ndio njia bora zaidi ya kufuatilia uwepo wa jiwe na ukubwa wake kabla na baada ya matibabu.

Picha za CT-ndio njia yenye matokeo sahihi zaidi yanayoonyesha mawe ya viwango/ ukubwa wake na huonyesha iwapo njia imeziba.

Mashine inayoangalia ndani ya mfumo wa mkojo.(IVU) : Njia hii ambayo ni nadra kutumika huwa sahihi sana kutambua mawe na kuziba kwa njia ya mkojo.Faida yake kubwa ni kwamba hutathimini uwezo wa figo kufanya kazi zake.Maumbile ya figo na iwapo njia ya mkojo imepanuka huweza kuonekana vyema kwa kutumia kipimo hiki.

Uchunguzi wa maabara

Vipimo vya mkojo: Vipimo hivi hutambua maambukizi na uasidi(pH) kwenye mkojo.Mkojo wa saa ishirini na nne huchukuliwa ili kupima kiasi chake,uwepo wa madini ya kalsimu ,fusfori,aina ya asidi ya yurik,magnesia,chumvi na aina ya protini ya kreatinini.

Vipimo vya damu: vipimo vya msingi kama vile vya chembechembe za damu, kreatinini, sukari na kutambua kemikali ambazo husababisha mawe kama vile kalsiamu,fosfori na asidi.Aidha kuna maabara zinazoweza kupima kiasi cha hormone ya parathyroid.

Uchambuzi wa jiwe: jiwe lililotolewa au kutoka lenyewe,uchambuz i hufanywa ilii kujua aina za kemikali zilizo kwenye jiwe , husaidia kujua matibabu yatakayotolewa na hatua za kuzuia mawe haya kutokea tena.

Jihadhari na‘mawe kimya’ ambayo hayana maumivu na huweza kudhuru figo.

Kuzuia

Kuzuia mawe kutokea. : Mtu akishapata mawe ya figo,huwa yumo hatarini ya kuyapata tena.Wagonjwa kama asilimia hamsini hadi sabini huyapata mara nyingine.Kwa upande mwingine,matibabu sahihi na ushauri ukizingatiwa hatari hii hupungua hadi asilimia kumi au hata kidogo zaidi.Kwa hiyo ni muhimu wagonjwa waliopata mawe kwenye figo kuzingatia ushauri wa njia za kuzuia.

Njia za jumla za kuzuia mawe ya figo

Vyakula ni muhimu katika kuzuia na pia kuongeza hatari ya mawe kutokea.Mambo muhimu ya jumla ya kuzingatiwa ni kama yafuatayo:

1. Vinywaji vingi
Kunywa maji mengi ni jambo muhimu sana katika kuzuia mawe kwenye figo.Kunywa kati ya gilasi kumi na mbili hadi kumi na nne (zaidi ya lita tatu)kila siku.Ili kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha, beba chupa ya maji popote uendapo.

  • Wengi hushindwa kuchagua aina ya maji ambayo ni bora lakini kumbuka ya kwamba aina ya maji si muhimu kama kiasi cha maji unachokunywa, kwa ajili ya kuzuia mawe kuwepokwenye figo.
Kwa utambuzi wa jiwe kwenye mfumo wa mkojo, vipimo vya CT, sonografia,na X ray ni muhimu sana katika uchunguzi.

  • Ili kuzuia mawe, mkojo wa kutosha ndio muhimu kuliko maji ya kutosha .Ili kujua kama unakunywa maji ya kutosha,pima kiasi cha mkojo kwa siku.Inafaa mkojo uwe zaidi ya lita mbili au mbili na nusu kila siku.
  • Rangi ya mkojo ndiyo husema iwapo unakunywa maji ya kutosha. Ukinywa maji ya kutosha,mkojo hauna rangi nzito.Hii huonyesha mkojo hauna madini mengi ambayo husababisha mawe.Mkojo wenye rangi nzito/njano huonyesha kutokunywa maji ya kutosha.
  • Ili kuzuia mawe, uwe na mazoea ya kunywa gilasi mbili za maji baada ya kula.Ni muhimu kunywa gilasi mbili kabla ya kulala na gilasi moja kila uamkapo usiku. Kunywa maji kila SIKUusiku wa manane ni muhimu sana kwa kuzuia mawe.Unaweza kuweka saa ya kengele ili ikuamshe kunywa maji.
  • Vinywaji vingi vinapendekezwa kwa watu wenye shughuli nyingi hasa katika siku zenye joto jingi kwani maji mengi hupotezwa jasho linapomwagika.
  • Ni vinywaji vipi bora zaidi?
    Kunywa maji kama yale ya nazi/dafu,ya nyanya au ya matunda kama malimau,au mananasi haya husaidia kuzuia mawe. Hata hivyo kumbuka kuwa ni muhimu asilimia hamsini ya vinywaji iwe maji.
  • Ni vinywaji vipi ambavyo havifai?
    Usinywe maji ya zabibu,au tufaha;chai ya turungi,kahawa,chokoleti na soda;na aina yoyote ya pombe.
Kunywa maji mengi huwezesha kutoa mawe kupitia kwenye mkojo.

2. Jizuie na chumvi

Usile chumvi nyingi, chumvi nyingi katika chakula inaweza kufanya kalsiumu zaidi itoke mwilini kwa njia ya mkojo na hivyo kuongeza hatari ya mawe kutokea. Kwa hiyo chumvi unayoila isizidi gramu sita kwa siku.

3. Punguza vyakula vitokanavyo na wanyama
Vyakula hivi ni kama nyama ya mbuzi, kuku, samaki, ng’ombe na hata mayai. Hivi huwa na asidi nyingi ya aina ya yurik ambayo huleta mawe.

4. Vyakula bora
Kula vyakula vyenye mboga mboga na matunda mengi ambayo hupunguza asidi kwa ujumla na kwenye mkojo.Kula matunda kama ndizi, mananasi,cheri na machungwa.Mboga mboga kama karoti,malenge na pilipili hoho pia maharagwe na shayari.Usile vyakula vilivyokobolewa sana kama mkate mweupe,pasta na sukari.Mawe ya figo huhusishwa na kula sukari nyingi.

5. Mawaidha mengine
Usile zaidi ya gramu elfu moja ya vitamini ya C inayopatikana kwenye matunda.Chunga uzito usizidi kwani pia husababisha mawe. Lazima ule vyakula bora ili uzito usizidi.

Hatua Maalum
1. Kuzuia mawe ya aina ya kalsiamu

  • Usizuie vyakula vyenye kalsiamu kama vile maziwa, bali ule vyakula bora vyenye kalsiamu. Kalsiamu iliyo kwenye chakula kwa kawaida hushikana na madini mengine yanayoitwa oxalate, na kwa pamoja yaweza kutoka mwilini,lakini iwapo madini ya kalsiamu ni kidogo mwilini,madini haya mengine ya oxalate hukosa kalsiamu ya kushikamana nayo ili iweze kutolewa mwilini, na hivyo basi hutengeneza jiwe. Usimezetembe za kalsiamu, iwapo ni lazima zitumiwe,basi zitumiwe pamoja na vyakula ili kupunguza hatari.
  • Dawa za kuzuia mawe ya kalsiamu zinaweza kutumiwa (Thiazide diuretics).
Mkojo ambao ni safi, hauna rangi rangi,unaonekana kama maji inahashiria muhusika anakunywa maji yakutosha.

2. Kuzuia mawe ya aina ya oksaleti

Watu walio na aina hii ya mawe wanafaa kuzuwia kula vyakula vyenye wingi wa madini haya ya okslaleti, kama;mboga-majugwa,viazi vitamu,bamia na viazisukari.

  • Matunda na matunda makavu-Forosadi (stroberi), zabibu, casiberi, matomoko, njugu karanga, korosho, lozi na tini.
  • Vyakula vingine-pil ipil i hoho, keki yenye matunda,chokoleti,koko,soya na siagi ya njugu.

3. Kuzuia mawe ya asidi ya yurik

  • Epuka vileo vyote.
  • Jiepushe na nyama ya maini,figo,ubongo,pia samaki,nyama ya nguruwe,kuku,ng‘ombe,na hata mayai.
  • Jiepushe pia na maharagwe, spinechi, dhania, koliflawa na mkate mfamu.
  • Jiepushe na vyakula vyenye mafuta kama aiskrimu na vilivyokaangwa.
  • Tumia dawa kama zile za kuzuia aside ya yurik.
  • Zuia uzito usizidi.
Kuzuia ulaji wa chumvi na kula kalisi yakutosha katika chakula ni muhimu katika kuzuia uundwaji wa mawe yenye asili ya kalisi.

Matibabu

Matibabu ya mawe kwenye njia ya mkojo

Matibabu hutegemea dalili, ukubwa wa jiwe,mahali lilipo katika mfumo wa mkojo na chanzo chake.Pia hutegemea iwapo mgonjwa ana maambukizi au njia ya mkojo imeziba.

Njia mbili za matibabu ni:
A Njia ya kuhifadhi (conservative).
B. Njia ya upasuaji.

A. Njia ya Matibabu (conservative treatment)

Mara nyingi mawe ya figo huwa madogo, yenye ukubwa usiozidi milimita tano.Haya huweza kutoka yenyewe baada ya wiki tatu hadi sita. Matibabu hulenga kupunguza makali /maumivu na kuwezesha jiwe kutoka bila upasuaji.

Matibabu ya kwanza

Ili kupunguza maumivu makali, mgonjwa huenda akahitaji sindano au kuwekewa dawa ya maumivu kwa njia ya mshipa.Iwapo maumivu si makali sana, vidonge vinamezwa na husaidia.

Maji mengi.
Kwa walio na maumivu makali,mgonjwa haifai kunywa maji mengi sana kwani yanaweza kuzidisha maumivu.Wakati mgonjwa hana maumivu basi anashauriwa anywe maji mengi na vinywaji vingine, lita mbili au tatu kwa siku huwezesha mawe kutoka.Pombe hairuhusiwi.Iwapo mgonjwa anatapika basi anafaa kuwekewa maji .Mgonjwa anafaa kuliweka jiwe lililotoka ili lipimwe.Njia rahisi ya kulipata ni kukojoa kwenye chombo kilicho na kichungi.

Hatua nyingine

Ni muhimu mkojo uwe na pH inayotakiwa. Dawa kama calcium channel blockers na alpha-blockers hupunguza maumivu kwa kuzuia kubana katika ureta na kuruhusu jiwe/mawe kutoka. Tibu pia kichefuchefu, kutapika na maambukizi ya mfumo wa mkojo kama yapo.

Kunywa maji mengi kutaosha kiasi kikubwa cha mawe madogo madogo katika mkojo.

B. Njia ya upasuaji.

Njia kadhaa za upasuaji zipo kwa kuondoa mawe kwenye figo baada ya kushindwa kutoka kwa matibabu. Njia hizi hazishindani bali hukamilishana. Madaktari bingwa huamua ipi ni njia bora. Baadhi ya njia zinazotumika sana ni pamoja na: (i) Njia ya kutovunjavunja mawe kwa njia ya mashine. (ii) Njia ya kuyatoa mawe kwa kutengeneza njia hadi kwenye figo kupitia mgongoni. (iii) Njia ya kutoa jiwe/mawe kupitia kwenye njia ya mkojo na. (iv) Upasuaji wa kawaida.

Ni mgonjwa yupi huhitaji upasuaji?

Wengi huweza kutolewa mawe bila upasuaji lakini kuna wale lazima wapitie upasuaji kwa mfano:

  • Jiwe likikataa kutoka baada ya muda wa kutosha /mwingi na kusababisha maumivu makali.
  • Jiwe ni kubwa sana na linashindikana kutoka/kuteremka lenyewe.
  • Jiwe linapozuia mkojo na kwa hiyo kudhuru figo.
  • Jiwe linaposababisha maambukizo ya njia ya mkojo au kutokwa na damu.

Upasuaji wa dharura unaweza kuhitajika iwapo jiwe limeziba njia ya mkojo ya mtu mwenye figo moja au figo zote mbili zimeziba kwa wakati mmoja.

Karibu asilimia hamsini ya mawe hujirudia kwa hiyo ni muhimu kuzuia.

1. Njia ya kuvunjavunja mawe kwa mashine (ESWL)

Extra-Corporeal Shock wave Lithotripsy- ESWL - Hii ndiyo njia ya kisasa ambayo ni bora na hutumika mara nyingi kutoa mawe ya figo.Ni nzuri kwa kutoa mawe yenye ukubwa usiozidi sentimita moja na nusu,au mawe yaliyo katika njia ya mkojo katikati ya kibofu na figo (ureta).

Mawe huvunjwa kwa mawimbi yanayotoka kwenye mashine na huyavunja katika vipande vidogo vidogo ili yaweze kutoka kwenye mkojo kirahisi.Mgonjwa hutakiwa kunywa maji mengi wakati mwingine baada ya tiba hii. Tyubu ya plastiki nyororo huwekwa ndani ya njia ya mkojo ili kuzuia kuziba kwa njia hiyo.

Kwa ujumla njia hii huwa salama na matatizo yake ni kama damu kwenye mkojo,maambukizi,mawe kubaki na hivyo kuhitaji marudio ya matibabu haya,kudhuru figo na shinikizo la damu.Uzuri wake ni huwa ni njia salama ambayo haihitaji kulazwa hospitalini,dawa ya nusukaputi wala kukatwa.Uchungu si mwingi na inafaa kwa umri wowote ule.

Njia hii haifai kwa mawe makubwa na kwa watu wanene.Pia si nzuri kwa wajawazito na watu wenye maambukizo makali, shinikizo la damu au matatizo ya kutokwa na damu.Baada ya kutolewa mawe,lazima mgonjwa aangaliwe na daktari mara kwa mara na pia azingatie njia za kuzuia mawe kutokea tena.

2. Njia ya kupitia mgongoni

Njia hii ni bora kwa mawe makubwa namakubwa kadri yenye Ukubwa zaidi ya sentimita moja na nusu.Hutumiwa mara nyingi wakati njia nyingine zimeshindwa.

Katika njia hii mgonjwa hudugwa sindano ya nusukaputi na daktari hukata shimo dogo mgongoni na kutengeneza njia kutoka kwenye ngozi hadi kwenye figo.Hutumia mashine inayoonyesha viungo vya ndani pia.Huku akitumia mashine nyingine, daktari hulipata na kulitoa jiwe.Iwapo ni kubwa,jiwe huvunjavunja kwa mawimbi yenye nguvu na kisha vipande hivyo hutolewa.

Kwa ujumla,njia hii huwa salama ingawaje kuna hatari na matatizo yanayoweza kutokea, jambo ambalo ni la kawaida kwa upasuaji wowote ufanywapo.Matatizo haya yanaweza kuwa kutokwa na damu,maambukizo,kujeruhi viungo vilivyo karibu au mkojo kumwagika.Uzuri wake ni kuwa ni sehemu ndogo tu hukatwa(kama sentimita moja).Njia hii ni nzuri kwa mawe yoyote.Mgonjwa huwa hospitalini kwa muda mfupi tu na hupona haraka.

Upasuaji wa mawe (Lithotripsy) ni njia inayofaa itoayo matokeo yanayotarajiwa na inayotumika mara nyingi kwa matibabu yasiyohitaji upasuaji.

3. Kupitia njia ya mkojo

Njia hii ni bora ya kutoa mawe yaliyo katikati na upande wa chini wa njia ya mkojo.Mgonjwa hudugwa sindano ya nusukaputi kisha tyubu yenye kamera huingizwa hadi kwenye kibofu cha mkojo na kuingia kwenye yureta.Jiwe huweza kuonekana na hutolewa zima zima au huvunjwavunjwa kutegemea na ukubwa wake.Kama jiwe ni dogo ,hushikwa na kutolewa kwa mashine hii,kama ni kubwa, huvunjwavunjwa na hivyo basi vipande hivi vidogovidogo hutoka na mkojo.Mgonjwa hurudi nyumbani siku hiyo hiyo na huweza kuendelea na shughuli za kawaida baada ya siku mbili au tatu.

Faida za njia hii ni kuwa hata mawe magumu yanaweza kuvunjwa na haihitaji kukatwa/kupasuliwa (Incision).Ni salama kwa mama wajawazito,watu wanene na wenye matatizo ya kutokwa na damu.Matat izo yanayoweza kutokea ni damu kwenye mkojo,maambukizi,kujeruhiwa/kutoboa ureta na kuwa kovu baada ya kupona ambalo hupunguza upana wa yureta.

PCNL ni njia inayofaa ya kuondoa mawe kwenye figo yenye ukubwa wa kati hadi makubwa.

4. Njia ya upasuaji

Hii ni njia yenye uchungu na huhitaji siku tano hadi saba za kulazwa hospitalini.Kwa sababu ya kuwepo kwa teknolojia mpya,njia hii ni nadra sana sasa kutumika.Kwa sasa hutumika kutibu wagonjwa wenye matatizo ya mawe mengi na makubwa .Faida kuu ya upasuaji huu ni uwezo wa kutoa zaidi ya jiwe moja na yale makubwa kabisa.Ni njia ambayo si ghali sana hivyo hutumika sana katika nchi zinazoendelea ambako watu hawana pesa nyingi.

Mgonjwa wa mawe ya figo inafaa amwone daktari lini?

  • Anapopata maumivu tumboni ambayo hayaishi hata akinywa dawa.
  • Kichefuchefu kingi na kutapika ambapo mgonjwa hawezi kunywa maji wala dawa.
  • Homa, kibaridi, kuwashwa na maumivu tumboni.
  • Damu kwenye mkojo.
  • Kukosa kukojoa kabisa.
Mawe yaliyo sehemu ya kati au chini kwenye ureta yanaweza kutibiwa kwa ufanisi kwa kutumia mashine ya “ureteroscope” bila upasuaji wa kawaida.