6: Nadharia Potofu na Ukweli Juu ya Magonjwa ya Figo

Wazo Potofu:Magonjwa yote ya figo ni hatari.

Ukweli: La, magonjwa yote ya figo si hatari. Yakitambuliwa na kutibiwa mapema, magonjwa mengi ya figo yanaweza kuponywa. Kwa mengi, utambuzi na matibabu hupunguza au kusimamisha kuendelea kwa magonjwa hayo.

Wazo Potofu: Hitilafu ya figo huweza kutokea iwapo figo moja linahitilafu.

Ukweli: La, hitilafu ya figo hutokea iwapo figo zote mbili zimefeli. Watu hawahisi shida yoyote ikiwa figo moja imefeli kabisa,na kwa hali kama hiyo, kiwango cha yurea na kreatinini ya serami katika damu huwa kawaida. Lakini ikiwa figo zote zimefeli,uchafu hukusanyika mwilini na ongezeko la kiwango cha yurea na kreatinini ya serami katika damu huonyesha kiwango cha juu. Kuongezeka kwa kiwango cha yurea na kreatinini katika damu huonyesha kufeli kwa figo.

Wazo Potofu: Katika magonjwa ya figo, kuwepo kwa edema huonyesha kufeli kwa figo.

Ukweli: La, katika magonjwa ya figo mengine, kuna edema, lakini kazi ya figo ni kawaida (K.m uvimbe wa figo – Nephrotic Syndrome).

Wazo Potofu: Edema hupatikana kwa wagonjwa wote wenye hitilafu ya figo.

Ukweli : La, edema hupatikana kwa wagonjwa wengi wenye hitilafu ya figo, lakini si kwa wote . Wagonjwa wachache huwa hawana edema hata katika hatua ya mwisho ya hitilafu ya figo kwa hiyo ukosefu wa edema si uthibitisho kuwa mgonjwa unayemwona hana hitilafu ya figo.

Wazo Potofu: Wagonja wote wa ugonjwa wa figo wanapaswa kunywa maji mengi.

Ukweli: La, upungufu wa utoaji wa mkojo hupelekea kwa mgonjwa kuvimba. Hii ni sifa muhimu kwa magonjwa mengi ya figo. Kwa hiyo kudhibiti kunywa maji ni muhimu/ lazima ili kudhibiti usawazishaji wa maji kwa wagonjwa kama hao. Hata hivyo, wagonjwa wanaoumwa ugonjwa wa mawe na maambukizi ya mfumo wa mkojo, wenye figo zinazofanya kazi sawa sawa wanashauriwa kunywa maji mengi.

Wazo Potofu: Najiona niko mzima, kwa hiyo sidhani nina shida ya figo.

Ukweli: Wagonjwa wengi hawaonyeshi dalili zozote katika hatua za mwanzo za ugonjwa sugu wa figo. Uchunguzi wa kimaabara ndio thibitisho pekee la kuwepo kwa shida ya figo.

Wazo Potofu: Ninajihisi vyema, kwa hiyo sihitaji kuendelea na matibabu ya tatizo langu la figo.

Ukweli: Wagonjwa wengi wenye ugonjwa sugu wa figo (CKD) hujihisi vyema, kwa hiyo huacha kuendelea na matibabu na lishe maalumu. Kutoendelea na matibabu ya CKD huweza kuwa hatari. Inaweza kusababisha kuzorota ghafla kwa hitilafu ya figo na kwa muda mfupi wagonjwa kama hao wanaweza kufika hatua inayohitaji dayalisisi au kubadilisha figo.

Wazo Potofu: Kreatinini ya serami yangu iko juu kidogo tu ya ile ya kawaida .Lakini niko salama kwa hiyo sina haja ya kuwa na wasi wasi.

Ukweli: Hata ongezeko dogo tu ya kreatinini ya serami ni ishara ya kulemaa kwa figo na uhitaji uchunguzi. Magonjwa mengi ya figo yanaweza kuharibu figo, kwa hivyo mwone mtaalamu wa nefrolojia bila kuchelewa. Hebu tuelewe umuhimu wa ongezeko la kiwango cha kreatinini ya serami (hata kidogo) katika hatua na wakati tofauti wa ugonjwa sugu wa figo.

Hatua za mwanzo za ugonjwa sugu wa figo huwa hazina dalili na ongezeko la kiwango cha kreatinini ya serami linaweza kuwa kidokezo/ kithibitisho cha pekee la ugonjwa. Kiwango cha kreatinini ya serami

cha 1.6 mg/dl kina maana kuwa zaidi ya asili mia 50% ya kazi ya figo imepotea tayari, taarifa hii ni muhimu sana. Ugunduzi wa ugonjwa sugu wa figo na kuanzisha tiba sahihi katika hatua hii hutoa matokeo mazuri. Matibabu chini ya mtaalamu wa nefrolojia katika hatua hii husaidia kuhifadhi kazi ya figo kwa muda mrefu sana.

Ikiwa kiwango cha kreatinini ya serami ni 5.0 mg/dl, hii ina maana asili mia 80% ya kazi ya figo imepotea. Kiwango hiki kinaonyesha kulemaa sana kwa kazi za figo. Uchunguzi na matibabu sahihi katika hatua hii ni ya manufaa ili kuhifadhi kazi za figo. Lakini ni muhimu kukumbuka kuwa hatua hii ni ya mwisho ya ugonjwa sugu wa figo na nafasi pekee ya kupata matokeo bora ya matibabu huwa imekwishapotea.

Ikiwa kiwango cha kreatinini ya serami ni 10.0 mg/dl ina maana asili mia 90% ya kazi ya figo imepotea na kiwango hiki kinaonyesha hatua ya mwisho ya ugonjwa wa figo. Katika hatua hii nafasi ya kumtibu mgonjwa kwa kutumia dawa haupo tena. Wengi wa wagonjwa huhitaji dayalisisi katika hatua hii.

Wazo Potofu: Wagonjwa wenye hitilafu ya figo, wakifanyiwa dayalisisi mara moja ina maana dayalisisi inakuwa hitaji la kudumu.

Ukweli: La, muda anaohitaji mgonjwa wa hitilafu ya figo kufanyiwa dayalisisi hutegemea aina ya hitilafu ya figo.

Hitilafu kali ya figo hudumu kwa muda na ni aina inayoweza kurekebishwa kwenye hali yake ya awali. (reversible). Wagonjwa wachache wenye hitilafu kali ya figo huitaji usaidizi wa dayalisisi kwa kipindi kifupi. Kwa matibabu machache ya dayalisisi (few dialysis sessions),figo hupona kabisa katika hitilafu hii. Kuchelewa kumfanyia dialysis mgonjwa, kwa woga kwamba mgonjwa atahitaji dayalisisi ya muda mrefu/ya kudumu kunaweza kuhatarisha maisha ya mgonjwa.

Hitilafu sugu ya figo huwa mbaya zaidi kila kukicha na hairudi nyuma. Hitilafu sugu ya figo, ikifikia hatua ya mwisho (End Stage Kidney Disease), mgonjwa huyu atahitaji dayalisisi maisha yake yote.

Wazo Potofu: Dayalisisi hutibu hitilafu ya figo.

Ukweli: La, dayalisisi haitibu hitilafu ya figo. Dayalisisi ni tiba maalumu ya kuokoa maisha katika hitilafu ya figo ambalo limeshindwa kutoa uchafu, maji mengi na kusahihisha elektro- laiti na pia usumbufu wa acid base.Dayalisisi hufanya kazi ambayo figo haiwezi tena kufanya. Dayalisisi huweka mgonjwa kutokuwa na dalili, sawa na mtu mwenye afya hata akiwa na hitilafu kubwa ya figo.

Wazo Potofu: Katika kubadilisha figo, mtu jinsi ya kiume na wa kike hawawezi kuchangia figo zao kwa jinsia tofauti.

Ukweli: Wanaume na wanawake wanaweza kuchangia figo zao kwa jinsia tofauti kwa kuwa muundo na kazi ya figo zao ni sawa.

Wazo Potofu: Mchango wa figo huathiri afya na kazi ya uzazi.

Ukweli: Kuchangia figo ni salama sana na haina athari kwa afya na kazi ya uzazi. Wachangiaji wa figo huishi maisha ya kawaida yanayo jumuisha ndoa na kuzalisha watoto.

Wazo Potofu: Kwa kubadilisha figo, inawezekana kununua figo.

Ukweli: Kununua au kuuza figo ni hatia. Kumbuka kuwa figo linalopandikizwa hutoka kwa figo hai isiyo na uhusiano na figo ya mchangiaji. Figo inayopandikizwa huwa na hatari ya kukataliwa ikilinganishwa na figo yenye uhusiano.

Wazo Potofu Sasa, msukumo wangu wa damu ni kawaida kwa hiyo sihitaji tembe za kurekebisha msukumo wa juu wa damu yangu..Mimi huhisi vyema hata nisipomeza tembe hizi kwa hiyo kwa nini niendelee kuzitumia?

Ukweli : Wagonjwa wengi wa msukumo wa damu husita kutumia dawa baada ya hali hii kudhibitiwa ,kwa kuwa hawana dalili zozote tena, wanahisi kuwa sawa,bila dawa. Lakini msukumo wa damu usiodhibitiwa huuwa kimya kimya. Baada ya muda mrefu, huweza kusababisha shida kubwa kama shambulio la moyo, hitilafu ya figo na kupooza . Kwa hiyo ili kulinda viungo muhimu vya mwili, ni vyema kumeza dawa hata

kama hakuna dalili za msukumo wa damu ambao umetambulika na mtu kuhisi vyema.

Wazo Potofu: Wanaume pekee ndio wana figo ambazo zimo kwenye mfuko kati ya miguu.

Ukweli : Kwa wanaume na wanawake wote figo zao zipo kwenye sehemu ya juu na nyuma ya tumbo na ni za ukubwa, umbo na kazi sawa.

Kwa wanaume, kiungo muhimu cha uzalishaji, kende, kipo kwenye kifuko kati ya miguu.