14: Kupandikiza figo

Kuhamisha/ Kupandikiza Figo
Uhamishaji /Kupandikiza figo ni mazao ya hatua kubwa sana katika sayansi ya matibabu.Hii ndiyo njia bora kuliko zote ya kutibu ugonjwa wa figo uliofikia kipindi chake cha mwisho (ESKD).Baada ya mgonjwa kuhamishiwa /kupandikizwa figo,maisha hurudi karibu kama kawaida.

Kuhamisha /Kupandikiza figo kumeelezwa katika sehemu nne.

 1. Kabla ya kuhamisha / kupandikiza figo
 2. Kuhamisha / kupandikiza figo
 3. Baada ya kuhamisha / kupandikiza figo
 4. Kuhamisha / kupandikiza figo ya marehemu

Kabla ya kuhamisha/ Kupandikiza figo

Maana ya kuhamisha/ kupandikiza figo
Kuhamisha / kupandikiza figo ni kutoa figo yenye afya kutoka kwa mtu aliye hai au hata marehemu na kumwekea mtu mwingine anayeugua ugonjwa wa figo,kwa njia ya upasuaji.

Ni lini kuhamisha kupandikiza figo huhitajika?
Huhitajika kwa mtu mwenye figo zilizodhoofika kabisa na katika kipindi cha mwisho cha ugonjwa wa figo.

Uvumbuzi wa kuhamisha figo ni baraka kubwa kwa wagonjwa wenye ugonjwa sugu wa figo.

Ni lini kuhamisha / kupandikiza figo hakuhitajiki?

Kuhamisha / kupandikiza figo hakuhitajiki katika ugonjwa wa figo wa muda au wakati ni figo moja tu imefeli.

Kwa nini huwa muhimu kuhamishiwa figo?

Dayalisisi pamoja na dawa humsaidia mtu mwenye ugonjwa wa figo uliozidi (ESKD)lakini hazimponyi.Njia ya kuponya hali hii huwa ni tu kuwekwa figo nyingine.Huokoa maisha na mtu huweza kuendelea na maisha kama yale ya kawaida.Huwa ni zawadi ya maisha.

Faida za kuhamishiwa figo?
Faida kuu ni:

 • Mgonjwa aliye hamishiwa/pandikizwa figo hupona kiasi kwamba huishi maisha bora.Wagonjwa hawa huishi maisha karibu ya kawaida yenye shughuli na nguvu ya kufanya kazi karibu kama kawaida.
 • Mgonjwa huondokewa na maumivu na matatizo yanayoambatana na dayalisisi pia muda mwingi unaotumika pale.
 • Maisha marefu.Wanaohamishiwa figo huishi maisha marefu kuliko wanaofanyiwa dayalisisi.
 • Mgonjwa aliyehamishiwa/pandikizwa figo hana masharti mengi ya maji (fluids) au vyakula.
 • Matatizo ya kuhamishiwa /kupandikizwa figo si mengi yakilinganishwa na yale ya dayalisisi.
 • Ingawaje gharama ya kuhamishiwa /kupandikizwa figo ni kubwa,baada ya miaka miwili au mitatu gharama ya matibabu hupungua kwa waliohamishiwa figo ikilinganishwa na ya wale wanaofanyiwa dayalisisi.
 • Maisha ya kimapenzi huboreka kwa mwanaume na mwanamke naye anaweza kupata mimba.uja uzitonk.
Figo likipandikizwa salama ni tiba bora kwa wagonjwa wenye CKD – ESKD kwani huwarudishia maisha ya kaaida.

Kubadilisha Figo

Je kuna Kasoro/matatizo ya kuhamishiwa/ kupandikizwa figo?

Kuna faida nyingi za kuhamishiwa/kupandikizwa figo; lakini vile vile yapo matatizo yake. Baadhi ya matatizo hayo ni:

 • Upasuaji mkubwa.Uhamishaji /upandikizaji wa figo hufanywa kwa njia ya upasuaji na mgonjwa akiwa katika hali ya nusu- kaputi.Upasuaji huu mkubwa unaweza kuwa wa hatari wakati unapofanywa na hata baadaye.
 • Mwili kukataa figo. Hakuna uhakika kuwa mwili utaikubali figo iliyohamishiwa / iliyopandikizwa. Hata hivyo, siku hizi kuna dawa zinazosaidia hali hii ya kukataliwa ni nadra sana kwa figo kukataliwa na mwili kabisa siku hizi.
 • Dawa.Kuna haja ya kunywa dawa kila siku bila kukosa ili figo iendelee kufanya kazi.La sivyo, figo hiyo inaweza kushindwa kufanya kazi na mwili ukaikataa.
 • Hatari nyingine: Kuna hatari ya maambukizi,athari za dawa na kuzizoea. Aidha mfadhaiko unao ambatana na kungojea kupata mtu wa kutoa figo, iwapo figo itafanya kazi, iwapo itadumu,haya yote yanaweza kumfanya mtu kuwa na wasiwasi.
 • Gharama kubwa ya kuhamishiwa figo.
 • Wagonjwa wasiofaa kuhamishiwa figo Mtu ambaye amefikisha kipindi cha mwisho cha ugonjwa wa figo hafai kuhamishiwa figo iwapo ana maambukizi makali, ana saratani ,amedhurika na magonjwa ya akili pamoja na mtindio wa akili,ugonjwa wa moyo na hali zingine za kiafya.
Figo haiwezi kuhamishiwa/ kupandikizwa kwa mgonjwa mwenye ukimwi,saratani au magonjwa mengine makubwa.

Umri wa kuhamishiwa/ kupandikizwa figo ni upi?

Hakuna umri mahususi uliotengwa wa kuhamishiwa/kupandikizwa figo, lakini hupendekezwa zaidi kwa watu wa umri kati ya miaka mitano na sitini na tano.

Figo zinazohamishwa/zinazopandikizwa hutolewa wapi?
Watoa figo ni wa aina tatu:

 • Walio hai na ni wanafamilia
 • Walio hai na sio jamaa
 • Marehemu

Jamaa walio hai huwa wana uhusiano wa damu na mgonjwa- mzazi,kaka,mtoto,shangazi,mjomba au binamu.Walio hai na si jamaa wanaweza kuwa mke au mme au rafiki.Watoaji marehemu huwa ni wale waliofariki kifo cha ubongo ( brain damage na alitoa wosia afanyiwe hivyo kama hali yake itakuwa hivyo).

Nani anayefaa zaidi kumpatia mtu figo?

Mapacha (identical) ndio bora zaidi kupatiana figo.Uwezekano wa wote wawili kuendelea kuishi vyema baada ya kupeana figo huwa ni mkubwa.

Nani anaweza kuwa mtoaji figo?

Mtu mwenye afya nzuri na figo mbili anaweza kutoa figo iwapo aina ya damu na tishu za mwili za mtoaji na mpokeaji zinalingana kwa jumla (compatible),watoaji wanafaa kuwa kati ya miaka 18 - 65.

Figo illiyotolewa na jamaa huwa na matokeo mazuri zaidi kuliko zingine.

Aina ya damu hutumiwa vipi kuchagua mtoaji figo?

Ni lazima damu zilingane.Mtoaji na mpokeaji figo wawe na aina moja ya damu au wawe na aina zinazopatana kama ifuatavyo.

Aina ya damu ya mpokeaji Aina ya damu ya mtoaji.
O O
A A au O
B B au O
A B AB,A,B au O

Nani hawezi kutoa figo?

Mtoaji wa figo lazima achunguzwe hali yake ya afya, ya mwili na ya akili ili kudhibitisha kuwa ni salama kwake kutoa figo. Wafuatao hawawezi kutoa figo: mtu mwenye kisukari, saratani, UKIMWI, mtoaji ana ugonjwa wa figo, shinikizo la damu au ugonjwa wowote mkubwa wa kawaida au ugonjwa wa akili.

Watoaji wengi huendelea na maisha ya kawaida na yenye afya, wakiwa na figo moja.Maisha yao ya kimapenzi hayabadiliki na wanawake wanaweza kupata watoto na wanaume kuwa baba ya watoto kama kawaida.

Watoaji Wanaoshirikiana

Mtoaji aliye hai anafaa zaidi kulikofigo toka kwa marehemu au kufanyiziwa dayalisisi.Wagonjwa wengi walio katika kipindi cha mwisho cha ugonjwa wa figo hupata watoaji wanaojitolea na wenye afya.Tatizo lililopo huwa ni aina ya damu au kutolingana kwake( incompatibility).

Kuhamishiwa /kupandikizwa figo huwa salama na huokoa maisha ya mgonjwa Wa CKD.

Kutoa figo kwa kushirikiana au kubadilishana huwezesha jozi mbili za mtoaji na mpokeaji ambao damu zao hazipatikani,kushirikiana na kuunda jozi mbili za mtoaji na mpokeaji wanaopatana.Hii inaweza kufanyika iwapo mtoaji figo wa jozi ya kwanza ana damu inayopatana na ya mpokeaji wa jozi ya pili, na mtoaji wa jozi ya pili. Ana damu inayopatana na ile ya mpokeaji wa jozi ya pili kama ilivyoonyeshwa kwenye mchoro.Kwa kubadilishana figo zilizotolewa na watu wawili wanaweza kupata figo zinazowafaa.

Kuhamisha/kupandikizwa figo kabla ya dayalisisi

Mara nyingi wagonjwa hupatiwa au uhamishiwa /hupandikizwa figo baada ya muda fulani wa dayalisisi.Hata hivyo kwa walio na ugonjwa wa figo uliozidi au unaosemekana kuwa katika kipindi chake cha mwisho,inafaa kuhamishiwa /kupandikizwa figo kabla ya dayalisisi.Hii ni kwa sababu huzuia hatari, gharama na mfadhaiko wa dayalisisi,na pia uhamisho/kupandikizwa figo huwa na uwezekano wa kufaulu kuliko kwa yule aliyekwisha fanyiwa dayalisisi kwa sababu ya faida zake basi,mgonjwa anashauriwa kufanyiwa uhamisho /upandikizwaji figo kabla ya dayalisisi iwapo ana mtu wa kumtolea figo.

Upasuaji wa kuhamisha/kupandikiza figo

Upasuaji wa kuhamisha/kupandikiza figo

Kabla ya upasuaji,hali ya mgonjwa ya kimwili ,kiakili na ushirikiano lazima ichunguzwe na kutathminiwa.Hii hufanywa ili kuhakikisha afya njema na usalama wa mtoaji figo na mpokeaji. Vipimo vya kitabibu huhakikisha kuwa aina ya damu ya mtoaji na mpokeaji zinapatana.

 • Kazi ya kuhamisha figo hufanywa na timu ya daktari bingwa wa figo,mpasuaji, daktari bingwa wa patholojia, mtaalamu wa nusu kaputi,wauguzi na pia waratibu wa uhamishaji.
 • Baada ya kuelezwa kwa makini kuhusu utaratibu wote,mtoaji na mpokeaji (aliyehai) hutoa ruhusa.(consent)na upasuaji wa mtoaji na mpokeaji figo hufanyika pamoja.
 • Upasuaji huu huchukua kama saa tatu hadi tano wakiwa wamepewa dawa ya nusukaputi.
 • Iwapo mtoaji yu hai,kwa kawaida,figo ya kushoto ndiyo hutolewa kisha inaoshwa kwa dawa maalumu baridi na kuwekwa kwa upande wa kulia na wa chini ya tumbo ya mpokeaji.
 • Mara nyingi,figo nzee zilizodhoofika hazitolewi.
 • Iwapo mtoaji yu hai,figo iliyohamishwa/iliyopandikizwa huanza kufanya kazi mara moja.Lakini iwapo mtoaji alikuwa amekufa figo iliyohamishwa/iliyopandikizwa huchukua siku kadha au hata wiki kabla ya kuanza kufanya kazi.Mpokeaji ambaye figo yake inachukua muda kufanya kazi huhitaji dayalisisi hadi wakati figo itafanya kazi vyema.
 • Baada ya kupata figo,daktari bingwa wa figo ndiye humwangalia mgonjwa.

Matunzo Ya Mgonjwa Baada Ya Kupandikizwa Figo

Matunzo Ya Mgonjwa Baada Ya Kupandikizwa Figo Je Athari Gani Zinaweza Kutokea?

Matatizo yanayoweza kutokea baada ya kupandikiza figo ni figo kukataliwa(rejection), maambukizi, madhara yasiyotegemewa ya madawa na matatizo yanayo ambatana na upasuaji.

Vitu muhimu vya kuviangalia baada ya kupandikiza figo ni:

 • Dawa zinazotolewa baada ya kupandikiza na kukataliwa kwa figo lililopandikizwa.

Tahadhari zote baada ya kupandikiza figo na kuhakikisha kuwa figo lililopandikizwa lina afya na halipati maambukizi.

Figo huwekwa upande wa chini wa tumbo bila kugusa figo nzee.

Dawa baada ya figo kupandikizwa na Figo kukataliwa

Kwa nini wagonjwa wa upasuaji wa figo hutunzwa tofauti na upasuaji mwingine?

Mara nyingi upasuaji wa kawaida huhitaji dawa na kutunzwa kwa siku 7 hadi 10 pekee,lakini baada ya kuhamisha figo dawa na uangalizi mkubwa lazima uzingatiwe/ufanyike maisha yote.

Figo kukataliwa

Mfumo wa kinga ya mwili huwa umeundwa kwamba unaweza kutambua na kuharibu chochote kilicho kigeni kama bakteria na virusi ambavyo vinaweza kuwa na madhara mwilini. Mwili wa mpokeaji unapogundua kwamba figo iliyowekwa si sehemu ya mwili wake,kinga ya mwili huishambulia figo hiyo ili kuiangamiza.Huku kushambuliwa kwa figo hii geni na kinga ya mwili wa mpokeaji ndiko kunakoitwa ‘Figo kukataliwa’ .

Figo hukataliwa lini na athari zake ni zipi?

Figo inaweza kukataliwa wakati wowote baada ya kuhamishiwa/ kupandikizwa,lakini mara nyingi hutokea katika miezi sita ya kwanza. Ukali wa hali hii ya kukataliwa huwa tofauti kwa kila mgonjwa.Mara nyingi huwa kiasi tu na hali hii huweza kutibiwa kwa dawa zinazobadilisha kinga ya mwili kwa namna fulani. Hata hivyo, kwa wagonjwa wachache ,hali hii inaweza kuwa mbaya kiasi kwamba dawa haziwezi kusaidia.Katika hali hii figo huharibika.

Ni Dawa zipi zinafaa baada ya figo kuhamishiwa / kupandikizwa ili kuzuia kukataliwa?
 • Kwa sababu ya kinga ya mwili, wakati wote kuna hatari ya figo iliyohamishiwa / iliyopandikizwa kukataliwa.
Matatizo makuu baada ya figo kuhamishiwa/ kupandikizwa huwa ni figo kukataliwa, maambukizi na athari za dawa.
 • Kama kinga ya mwili ingezimwa kabisa hakungekuwa na hatari hii.Lakini mgonjwa anaweza kuwa hatarini na maambukizi(hata ya kuhatarisha maisha) kama mwili hauna kinga.
 • Dawa maalum hutumiwa ambazo hubadili kinga kwa njia fulani ili kuzuia figo kukataliwa Dawa hizi kwa kiasi fulani huathiri uwezo wa mgonjwa wa kupigana na maambukizi.
 • Dawa za aina hii zinazotumika mara nyingi huwa ni prednisolone, cydosporine, azathioprine, mycophenolate mofetil(MMF), tacrolimus na sirolimus.
Mgonjwa anafaa kuendelea na dawa hizi kwa muda gani baada ya kuhamishiwa / kupandikizwa figo?

Ili kuzuia figo kukataliwa,mtu hunywa dawa hizi maisha yake yote.Mwanzoni dawa kadhaa hutumiwa lakini kadri muda unavyo pita huendelea kupunguzwa kwa idadi na kiasi.

Je, mgonjwa huhitaji dawa zingine baada ya kuwekewa/ kupandikizwa figo?

Ndio.Baada ya kuwekewa/kupandikizwa figo nyingine,mgonjwa huhitaji dawa nyingine pamoja na zile za kubadili kinga ya mwili. Dawa hizi zingine ni kama zile za kudhibiti shinikizo la damu,za kukojoa,za nguvu ya mifupa,za kuzuia au kutibu maambukizi,vitamini na zile za kuzuia vidonda vya tumbo.

Dawa zinazobadili mfumo wa kinga ya mwili zina hatari gani?

Madhara ya dawa hizi yameelezwa hapa chini:

Lazima mgonjwa aendelee kunywa dawa ili kuzuia figo kukataliwa na mwili.

Nini kinachofanyika figo iliyohamishwa/iliyopandikizwa ikishindwa kufanya kazi?

Huwa kuna njia mbili za kukabiliana na hali hii :-

Kupatiwa figo nyingine au dayalisisi

Tahadhari Baada ya kuhamishiwa /kupandikizwa figo

Iwapo uhamisho wa figo umefaulu,mtu hupata maisha ya kawaida,yenye afya na uhuru.Hata hivyo,ni muhimu kuchunga figo iliyohamishiwa/pandikizwa na kuzuia maambukizo.

Kama figo iliyopandikizwa imeshindwa kufanya kazi, lazima moja ya haya mawili yafanyike: kuanzishwa dialisisi au hatua za kupandikizwa figo jingine.

Mwongozo wa jumla wa kuhifadhi afya ya figo iliyohamishiwa/Pandikizwa:

 • Usisimamishe wala kubadilisha dozi ya dawa zako.Kumbuka ya kwamba kukosa kunywa dawa,kubadilisha au kuacha kabisa ndicho chanzo cha figo iliyohamishiwa/kupandikizwa Kufeli/ kukataliwa.
 • Kuwa na orodha ya dawa zako na uwe nazo za kutosha kila wakati.Usinunue dawa ovyo madukani wala kutumia mitishamba.
 • Upime shinikizo la damu, kiasi cha mkojo,uzito na sukari(iwapo umeshauriwa hivyo na daktari)kila siku na uandike rekodi ya vipimo hivi.
 • Mwone daktari wako na kapimwe kama ulivyoshauriwa. Hii ni muhimu sana.
 • Upimwe damu katika maabara iliyopendekezwa tu.Iwapo matokeo hayaridhishi,badala ya kwenda kwenye maabara nyingine,mwone daktari wako haraka iwezekanavyo.
 • Katika hali ya dharura, na unahitaji kumwona daktari mwingine ambaye hafahamu shida yako, usisite kumeleza kuwa umepandikizwa figo. Kumbuka kumweleza pia dawa unazotumia.
 • Masharti juu ya vyakula hupungua baada ya kupata figo jipya, lakini ni vyema kuzingatia ushauri wa vyakula bora vyenye protini na nguvu ya mwili na pia kula kwa wakati ufaao kila siku. Kula sukari, chumvi na mafuta kidogo, pia vyakula vyenye nyuzi nyingi ili kuepuka uzito.
Kupata ushauri wa daktari mara moja na kwa shida yoyote pia kutibiwa kwa shida mpya au isiyo ya kawaida hii ni njia ya lazima ya kutunza figo.
 • Unywe zaidi ya lita tatu za maji kila siku.
 • Fanye mazoezi mara kwa mara na kuzuia uzito.Usifanye kazi nzito wala michezo yenye mpambano kama vile ndondi au mpira wa miguu.
 • Unaweza kuendelea na maisha ya mahusiano ya ndoa baada ya miezi miwili hivi na kama utakavyoshauriwa na daktari wako.
 • Usivute sigara wala kunywa pombe.
Tahadhari za kuzuia maambukizo
 • Epuka mahali penye watu wengi kama vile majumba ya sinema, maduka makubwa(malls) magari yenye watu wengi na watu wenye maambukizo.
 • Vaa kichuja hewa (masks)kila ukiwa kwenye watu wengi kwa miezi mitatu ya kwanza.
 • Nawa mikono yako kwa maji na sabuni kabla ya kula, kabla ya kunywa dawa zako na baada ya kwenda msalani.
 • Kunywa maji yaliyochemshwa na kuchujwa.
 • Kula vyakula vilivyopikwa nyumbani kwa vyombo safi.Usile matunda, mboga mbichi na kamwe usile nje na chakula kisichopikwa kwa miezi mitatu ya kwanza.
 • Dumisha usafi nyumbani.
 • Piga msuaki mara mbili kwa siku kutunza meno yako.
 • Chunga kidonda au jeraha lolote kwa kukisafisha sehemu iliyoumia mara moja kwa sabuni na maji na funika kwa kitambaa safi.
Pata ushauri wa daktari au kituo cha kuhamisha /kupandikiza figo kama:
 • Una homa zaidi ya 100F au dalili za homa kama vile kuhisi baridi,kuumwa na mwili au kuumwa na kichwa.
Daktari atafutwe mara moja na tiba ianzishwe mara pale ambapo kuna dalili mpya auzisizo za kawaida ili kulilinda figo.

 • Uchungu au wekundu karibu na sehemu yenye figo ngeni.
 • Mkojo kupunguka,kuvimba mwili au uzito kuongezeka ghafla(zaidi ya kilo moja kwa siku).
 • Mkojo wenye damu au kuwashwa unapokojoa.
 • Kikohozi, kukosa pumzi, kutapika au kuharisha.
 • Ishara zozote mpya, zisizo za kawaida au ngeni zikionekana.

Kwa nini wagonjwa wachache tu huweza kupata figo?

Kuhamishiwa au kupatiwa figo ndio njia ya pekee ya kutibu ugonjwa sugu wa figo.Wengi wangetaka kupata figo. Sababu kuu tatu za ukosefu wa figo ni:

1. Kukosa mtoaji wa figo: Si watu wengi huweza kupata watu wa kuwapatia figo.Watoaji walio hai huwa hawapatikani na wanaongoja figo za walioaga pia ni wengi sana.
2. Gharama: gharama ya kuhamisha figo na ya dawa za baadaye huwa juu sana.Hiki huwa kikwazo kikubwa hasa kwa wananchi maskini wa nchi zinazoendelea.
3. Ukosefu wa vifaa: Katika nchi zinazoendelea au maskini ,vituo vya kuhamisha /kupandikiza figo ni nadra/vichache sana.

Kukosa watoaji ni kikwazo kikubwa kinachowanyima wagonjwa faida za kupatiwa figo.

Kuhamisha figo ya marehemu

Kuhamisha figo ya marehemu

Hapa ,figo zenye afya nzuri hutolewa kwa upasuaji kutoka kwa mtu ambaye amekufa ubongo au moyo,na hupachikwa /hupandikizwa kwa mgonjwa wa figo.Hutolewakwa mtu ambaye amekufa tu na mwenyewe au jamii yake wangetaka kutoa sehemu zake kwa wengine.

Kwa nini mtu awekewe figo ya marehemu

Watu wengi wenye ugonjwa sugu wa figo na wanaongoja kupatiwa figo,wanaendelea kufanyiwa dayalisisi kwa sababu wamekosa kabisa mtoaji aliye hai wa kuwapatia figo.Tumaini lao tu ni kupata figo la mtu aliyeaga.Kama mtu anaweza kumuokoa mwingine kwa kumtolea figo anapoaga,ni wema mkubwa mno.Huku kuhamisha figo ya marehemu pia huzuia biashara haramu ya viungo vya mwili.

Kifo cha ubongo ni kipi?

Kifo hujulikana kama moyo kusimama na kuvuta pumzi kuisha kabisa na hakuna namna ya kuvirejesha. Kifo cha ubongo ni kusimama kwa kazi zote za ubongo na hivyo kufa.

Utambuzi wa kifo cha ubongo hufanywa na madaktari kwa wagonjwa hospitalini wakiwa wamepoteza fahamu na kupumua kwa mashine.

Madaktari hutambua vipi kifo cha ubongo?

1. Lazima mgonjwa awe amepoteza fahamu na kuwa katika hali ya kupoteza fahamu,na chanzo cha hali hii kujulikana kupitia historia ya mgonjwa,vipimo na picha.Chanzo kinaweza kuwa kugongwa kichwa au damu kwenye ubongo na kadhalika.Kuna dawa zingine,kama zile za kumfanya mtu alale, za kuzuia kuzimia katika kifafa ,za kunyoosha misuli na kuzuia usumbufu wa kiakili .Zinaweza kumfanya mtu azimie na kuonekana kama mwenye ubongo uliokufa.

Kama kifo cha ubongo kimetokea,hali hii haiwezi kugeuzwa, na kwa hiyo hakuna njia ya matibabu wala upasuaji inayoweza kuleta nafuu.

2. Mgonjwa kuwa amepoteza fahamu na hajitambui kabisa (deep coma) licha ya tiba ya wataalamu kwa muda na wataalamu hao kuona hakuna uwezekano wa kuamka.
3. Mgonjwa kutoamka kutoka kwenye hali ya kupoteza fahamu hata baada ya matibabu yanayofaa kufanywa na wataalamu wake.
4. Mgonjwa kuwa hawezi kupumua mwenyewe ila kwa kusaidiwa na mashine.

Ubongo kufa inamaanisha nini?

Kama ijulikanavyo,kifo humaanisha roho imesimama na mtu hawezi kupumua tena.Ubongo unapokufa kazi zote zake husimama milele na hivyo kufa.Madaktari ndio hutambua kifo cha ubongo kwa mgonjwa aliyelazwa hospitalini na kupumua kwa mashine.

Hatua za utambuzi wa kifo cha ubongo

1. Lazima mgonjwa awe katika hali ya kupoteza fahamu yaani hajisikii na chanzo cha hali hii kiwe kinajulikana vyema.Kinaweza kuwa ni kugongwa kichwa au damu kwenye ubongo,n.k. Mgonjwa lazima awe amepimwa,akapigwa picha na historia yake kufuatiliwa.Kuna dawa fulani kama vile zile za kumfanya mtu alale,za kuzuia kuzimia,za kunyoosha misuli,za kuzuia usumbufu wa kiakili na nyinginezo,zinaweza kumfanya mtu awe katika hali ya kutojihisi hadi aonekane kama aliyekufa.Sababu kama hizi lazima ziondolewe kabla ya daktari kusema ubongo wa mtu umekufa kwa kweli.
2. Kupumua, kusukuma na kuzunguka kwa damu mwilini kunaendeshwa kwa mashine.

Ubongo ukishakufa, mashine huendelea kusaidia mwili kupumua na damu kuzunguka.
Tofauti za kuzimia na ubongo kufa ni zipi?

Mtu ambaye amezimia na hajisikii anaweza kupumua bila ya kusaidiwa na mashine na anawea kupona baada ya kutibiwa.Kwa upande ule mwingine ,mtu aliyekufa ubongo hawezi kupona hata akipewa dawa au afanyiwe upasuaji.Mara tu mashine ya kupumua inapozimwa, roho husimama.Kumbuka ya kwamba mtu huwa amekufa tayari na kuzima mashine hizi siyo sababu ya kifo.Wagonjwa hawawezi kuishi kwa mashine kwani roho husimama mwishowe.

Je,mtu yeyote anaweza kujitolea figo yake ?

La! Kama vile jicho,figo haziwezi kutolewa kwa mtu aliyekwisha kufa.Mtu anapokufa roho husimama na damu haiendi kwenye figo tena.Kwa sababu hii,figo huharibika na haiwezi kutumika tena.

Nini husababisha ubongo kufa?

Kujeruhiwa kichwa,damu kwenye ubongo, ubongo kufa au uvimbe(tumour).

Utambuzi wa kifo cha ubongo hufanywa lini, na nani na kwa njia gani?

Iwapo mtu aliyewekwa kwenye mashine ya kupumua kwa muda haonyeshi mabadiliko,basi uchunguzi hufanywa na kundi la madaktari wasiohusika na uhamishaji wa figo.Miongoni mwao huwa daktari aliyekuwa anamtibu mgonjwa yule,daktari wa ubongo,na daktari mpasuaji wa ubongo.

Iwapo uchunguzi hauonyeshi dalili zozote za mgonjwa kuamka, pamoja na kufanyiwa EEG (KAMA IPO)basi huwa kumethibitishwa kuwa ubongo umekwisha kufa.

Mtu aliyekufa anaweza kuokoa uhai wa watu wawili figo zake zote mbili zikitolewa kwa watu hao.
Mambo yafuatayo ndiyo tu yanaweza kufanya figo ya mtu mwenye ubongo uliokufa isipatiwe mtu mwingine

1. Mgonjwa mwenye maambukizi.
2. Mgonjwa mwenye virusi vya ukimwi au ugonjwa wa ini wa hepatitis B.
3. Mgonjwa ambaye amekuwa na shinikizo la damu kwa muda mrefu, kisukari, ugonjwa wa figo na ugonjwa sugu wa figo.
4. Mgonjwa wa saratani(isipokuwa saratani ya ubongo).
5. Mgonjwa mwenye umri wa chini ya miaka kumi au zaidi ya sabini.

Je, ni viungo vingine vipi vya mwili vinavyoweza kutolewa kwa mtu aliyekufa ubongo?

Figo mbili zinaweza kutolewa na hivyo kuokoa maisha ya wagonjwa wawili . Viungo vingine ni macho, moyo, ini, ngozi na pia kongosho.

Je uhamishaji figo wa mtu aliyekufa hufanywa na nani?
Kundi hili huwa ni la:
 • Jamaa za aliyeaga ili kuhalalisha utoaji wa figo zake.
 • Daktari wa aliyeaga.
 • Mratibu wa uhamishaji anayeisaidia jamii ya mgonjwa.
 • Daktari wa ubongo anayethibitisha kifo cha ubongo.
 • Daktari bingwa wa mfumo wa mkojo na daktari bingwa mpasuaji wa figo.
Baada ya kupandikizwa figo, mgonjwa hufu rurahia maisha ya kawaida kabisa.

Figo ya mtu aliyeaga huhamishwa vipi?
Mambo muhimu.

 • Lazima kuhakikisha kuwa ubongo umekufa.
 • Kuhakikisha kuwa figo zote mbili hazina tatizo lolote na aliyeaga hana ugonjwa unaoweza kuambukiza.
 • Ruhusa ya kutoa kutoka kwa jamaa za aliyeaga.
 • Aliyeaga lazima awe kwenye mashine ya kuendeleza moyo kupiga,kuzungusha damu mwilini na kupumua hadi figo zote zimetolewa.
 • Baada ya kutolewa, figo huoshwa kwa maji maalum baridi na kuhifadhiwa kwenye barafu.
 • Mtu mmoja anaweza kuwapatia figo zake zote mbili,hivyo watu wawili tofauti wanaweza kupatiwa kila mmoja figo moja.
 • Kuzingatia vipimo mbalimbali vya kulinganisha aina ya damu na mambo mengine watakaopewa figo za mtu fulani huchaguliwa kwa orodha ya wanaongoja.
 • Baada tu ya matayarisho, upasuaji hufanywa kwa mtoaji na mpokeaji na figo huhamishwa.
 • Upasuaji anaofanyiwa mtoaji aliye hai ndio huo huo anaofanyiwa aliyeaga,na hata mpokeaji.
 • Kwa sababu ya kuhifadhiwa kwenye barafu na pia kukosa oksijeni, kwani damu haizunguki ,figo huwa haziwezi kufanya kazi mara moja zinapowekwa.kwa hiyo,dayalisisi ya muda mfupi huhitajika kwa wagonjwa wengi.

Kujitolea sehemu ya mwili ni jambo la faraja, kujitolea sehemu ya mwili ni jambo la kutukuzwa sana hata zaidi ya kuepusha ajali kwa kawaida.
Je kuna malipo yoyote yanayotolewa kwa mtoaji wa figo hapana

Hakuna malipo yanayotolewa kwa familia ya mtoaji figo; wala mpokeaji wa figo halipii figo hilo. Kutoa figo na mtu akaishi ni thawabu kubwa.Kumfanya mtu ambaye angali kufa kuishi tena ni jambo la wewe unayetoa kuwa na faraja kubwa.