Kuwa na figo moja ni jambo la wasiwasi.Hata hivyo mtu akijitunza vyema na kuishi maisha bora,anaweza kuishi maisha ya kawaida na figo moja .
Matatizo ambayo mtu mwenye figo moja anaweza kukumbana nayo katika maisha ya kawaida.
Karibu kila binadamu huzaliwa na figo mbili.Hata hivyo,hata figo moja lina uwezo wa kufanya kazi ambazo hufanywa na figo zote mbili.Kwa hivyo mtu mwenye figo moja hapati matatizo ya maisha ya kawaida ya kufanya kazi nzito wala mahusiano yake ya ndoa.
Figo moja inatosha maisha yote.Kwa mtu aliyezaliwa na figo moja,hali hii hugunduliwa anapofanyiwa vipimo kwa sababu tofauti kabisa.Kwa watu wachache wenye figo moja shida tu inayoweza kutokea baada ya miaka mingi ni shinikizo la damu au protini kwenye mkojo.Hata hivyo uwezo wa figo Haupungui.
Nini kinachosababisha figo moja?
Kwa kawaida kuna sababu tatu za mtu kuwa na figo moja
- Mtu kuzaliwa na figo moja.
- Figo moja kutolewa kwa sababu ya ugonjwa wa mawe kwenye figo,saratani,kuzibika,usaha kwenye figo au kujeruhiwa.
- Kumpatia mgonjwa figo moja.
Mtu mwenye figo moja huweza kuishi maisha yenye shughuli za kawaida kabisa.
Je, kuna uwezekano wa kuzaliwa na figo moji?
Watu wengi huzaliwa na figo moja. Uwezekano wa hali hii ni kama mtu mmoja kwa watu mia saba na hamsini. Wanaume ndio sana sana huzaliwa na figo moja na mara nyingi figo la kushoto ndilo huwa halipo.
Kwa nini mtu mwenye figo moja anahitaji tahadhari?
Hata kama mtu hana tatizo lolote akiwa na figi moja,anaweza kulinganishwa na gari la miguu miwili ambalo halina mguu wa akiba au wa spea.Bila figo ya pili,kudhurika kwa figo moja tu iliyopo husababisha kazi zote za figo kuzorota haraka sana.Figo zinaposhindwa kufanya kazi ghafla matatizo mengi hufuatia na huhitaji kushungulikiwa mara moja.Matatizo yanapotokea yanaweza kuzidi katika muda mfupi na kuhatarisha maisha.Wagonjwa kama hawa huhitaji dayalisisi mara moja.Ili kuzuia figo kudhurika,ni muhimu mtu mwenye figo moja kujilinda vyema.
Ni jambo gani linayoweza kusababisha kudhurika kwa ghafla kwa figo moja?
1. Mkojo kuzuiliwa ghafla na jiwe au damu iliyoganda kwenye mfumo wa mkojo (hasa ureta)na hivyo mkojo hukosa kutoka kwenye figo.
2. kufunga njia ya mkojo ya yureta kwa bahati mbaya wakati wa upasuaji wa tumbo,mkojo uliotengenezwa kwenye figo hupitia kwenye mshipa(njia ya mkojo) na kuingia kwenye kibofu cha mkojo.
3. Kujeruhiwa.Figo inaweza kujeruhiwa kwa michezo kama ndondi,magongo,kandanda,karate au miereka.Figo ambayo ni moja huwa kubwa na nzito kuliko figo ya kawaida ili kuweza kufanya kazi inayohitajika.Kwa sababu ya ukubwa wake,ni rahisi kujeruhiwa.
Watu wengi huzaliwa na figo moja.
Hatua za kuilinda figo ya kipekee
Wenye figo moja hawahitaji matibabu,lakini ni vyema kuzingatia hatua za kulinda figo waliyonayo. Hatua hizi ni kama:
- Kunywa maji mengi (kama lita tatu kwa siku).
- Kutohusika kwa michezo hatari.kama ndondi, karate, mielekank.
- Kuzuia na kutibu haraka mawe na maambukizi ya njia ya mkojo.
- Kabla ya kuanza matibabu yoyote au kufanyiwa upasuaji wa tumbo, umjulishe daktari ya kwamba una figo moja.
- Kuzuia shinikizo la damu, fanya mazoezi ya kawaida, chakula bora na usinywe ovyo dawa za maumivu, Epuka vyakula vyenye protini nyingi na chumvi kama daktari atakavyoshauri.
- Kupimwa mara kwa mara ili kujua kiasi cha uwezo wa figo, shinikizo la damu na hali ya mkojo, kupimwa angalau mara moja kwa mwaka kunaweza kutambua dalili zozote za matatizo ya figo au figo kushindwa kufanya kazi yake na unaweza kupewa matibabu mapema.
Mgonjwa mwenye figo moja amwone daktari lini?
- Kukosa kabisa mkojo kwa ghafla.
- Figo ya pekee kujeruhiwa.
- Haja ya dawa za maumivu au za x ray katika kipimo fulani.
- Homa, kuwashwa anapokojoa au mkojo wenye rangi nyekundu.
Watu wenye figo moja haifai wawe na wasi wasi bali wajifunze vizuri na kupimwa mara kwa mara.