11: Ugonjwa Sugu wa Figo: Dalili na Utambuzi

Dalili na utambuzi wake.

Katika hali hii ya ugonjwa sugu wa figo, figo hushindwa kufanya kazi polepole,kwa miezi hata miaka kwa hiyo mwili huzoea hatari za hali hii. Pia, figo huwa na uwezo mkubwa wa kujisaidia katika shida ya kazi zake.kwa sababu hizi mbili, watu walio na ugonjwa huu usiopona huwa hawana dalili zozote hadi wakati figo zimeharibika sana.

Figo huwa na kazi nyingi sana kama kutoa uchafu na maji kwenye mwili, kuzuia shinikizo la damu,kusawazisha kemikali mwilini , uzalishaji wa chembechembe za damu nyekundu mwilini na kadhalika.Hivyo kutegemea matatizo yaliyoko kwenyefigo, dalili huwa tofauti kati ya mtu mmoja na mwingine katika ugonjwa sugu wa figo.

Dalili za ugonjwa sugu wa figo ni zipi?

Dalili hutofautiana kulingana na kiwango cha ugonjwa.Ili kuelewa vyema na kukabiliana na hali hii vizuri,ugonjwa wa figo umegawanywa katika viwango vitano kulingana na kiasi cha utoaji uchafu kwenye figo (Glomerular Filtration Rate- GFR),ambacho ndio kiwango cha kuonyesha jinsi figo zinavyochuja uchafu kutoka kwenye damu.GFR huhesabiwa kulingana na kiasi cha creatinini kwenye kipimo cha damu. Kipimo cha GFR ni kipimo sahihi cha kuonyesha utendaji wa figo: Utendaji mzuri wa figo ni wakati GFR ni zaidi ya mililita tisini kwa kila dakika (90 ml/min).

Mapema katika ugonjwa huu,(CKD) wagonjwa wengi hawana dalili zozote za ugonjwa.

Hatua za ugonjwa wa figo usiopona.

Hatua Hatua Ya kwanza Hatua Ya pili Hatua Ya tatu Hatua Ya nne Hatua Ya tano
  GFR ya Kawaida Kiwango kidogo cha ugonjwa wa figo Ugonjwa kiasi cha figo Ugonjwa mkali wa figo Hatau za za mwisho
GFR Zaidiya 90 ml/dakika 60-89 ml/dakika 30-59 ml/dakika 15-29 ml/dakika kidogo kuliko 15 ml/ dakika

 

Hatua ya kwanza ya ugonjwa wa figo usiopona (kazi ya figo ikiwa 90_-100%)

Hii ni hatua ya mapema ya ugonjwa huu na figo huwa hazijadhurika. Umajimaji (serum creatinini) kwenye damu huwa uko katika kiwango cha kawaida.Katika hatua hii ya kwanza ya CKD tatizo linaweza tu kujulikana mtu anapofanyiwa uchunguzi wa kimatibabu au anapopimwa kwa ugonjwa mwingine.

Ishara za hali hii zinaweza kukosekana. Kwa mfano;kuwepo kwa protini kwenye mkojo, sura yafigo kuonekana zimebadilika kwenye picha za eksirei, ultrasound,MRI au CT,historia ya familia yenye ugonjwa wa uvimbe wa figo (polycystic kidney).

Hatua ya pili ya ugonjwa wa figo usiopona (kazi ya figo ikiwa 60_89%)

Hapa figo zimedhurika kidogo.Wagonjwa wanaweza kuwa hawana dalili, lakini ishara zinaweza kuwa ni kukojoa mara nyingi hasa usiku,shinikizo la damu kuwa juu,mkojo usio wa kawaida na creatinini kwenye damu inaweza kuwa juu ( au hata kawaida).

Shinikizo la damu katika umri mdogo ni ishara kuu ya ugonjwa wa figo.

Hatua ya tatu (kazi ya figo ikiwa 30_59%)

Ugonjwa huwa na kasi,wagonjwa wanaweza kuwa hawana dalili au wana dalili kidogo pamoja na mkojo kuwa si wa kawaida,na creatinini kwenye damu kuongezeka.

Hatua ya nne (Kazi ya figo ikiwa 15_29%)

Katika hatua hii ya ugonjwa, ugonjwa huwa mkali. Kuna dalili nyingi, kutegemea chanzo cha kudhoofika kwa figo na magonjwa mengine yaliyoambatana na hali hii.

Hatua ya tano(kazi ya figo ikiwa kidogo chini ya 15%)

Hii ni hatua ya mwisho na ni ya hatari.Kuna dalili nyingi na nyingine zinazohatarisha hata maisha.Katika hatua hii hata matibabu yakifanywa,dalili za figo kufeli huzidi na wagonjwa wengi huhitaji dayalisisi au kupatiwa figo nyingine.

Ishara kuu za ugonjwa wa figo ni:

  • Kukosa hamu ya chakula,kichefuchefu na kutapika.
  • Kuwa mdhaifu,mwili kuchoka na kupungua uzito.
  • Kuvimba miguu,mikono au/na usoni karibu na macho.
  • Shinikizo la damu lisilozuilika hasa kwa umri mdogo.
  • Kukosa nguvu kunakosababishwa na upungufu wa damu mwilini (anaemia),hali inayosababishwa na figo kutotengeneza homoni ya erithropoyetini inayosaidia kutengeneza chembechembe za damu.
  • Kushindwa kulala,kizunguzungu na kushindwa kuwa makini.
Kukosa nguvu,kukosa hamu ya chakula,kichefuchefu na kuvimba ni dalili za mapema za ugonjwa wa figo.
  • Kujikuna,mkakamao wa misuli ( muscle cramps), kuhisi uchovu kwenye miguu na kushindwa kufikiria kitu kwa makini.
  • Maumivu mgongoni hasa chini ya mbavu.
  • Kuhisi kutaka kukojoa mara kwa mara hasa wakati wa usiku (nocturia).
  • Maumivu, Urahisi wa kuvunjikavunjika mifupa kwa watu wazima na watoto kutokukua kwa sababu ya upungufu wa vitamini D inayotengenezwa na figo.
  • Kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwa wanaume na kukosa hedhi kwa mwanamke.
  • Ugonjwa wa figo huhusishwa na ongezeko la vifo vinavyotokana na ugonjwa wa moyo.
Ni wakati gani ushuku ugonjwa wa figo kwa mtu mwenye matatizo ya shinikizo la damu? Shuku ugonjwa wa figo ikiwa:
  • Umri wa mgonjwa ni nchini ya miaka thelathini (30) au zaidi ya miaka hamsini (50) shida ya shinikizo la damu inapotambuliwa/ inapogundulika.
  • Iwapo shinikizo la damu liko juu sana(zaidi ya 200/120mm /Hg).
  • Shinikizo la damu la juu sana hata baada ya matibabu kuzingatiwa.
  • Kushindwa kuona kwa sababu ya shinikizo la damu.
  • Kuwepo kwa protini kwenye mkojo.
  • Shinikizo la damu kuhusishwa na dalili za ugonjwa wa figo kama vile kuvimba,kukosa hamu ya chakula, kuchoka/kukosa nguvu na kadhalika.
Vipimo vitatu rahisi vinaweza kuokoa figo yako.Pima shinikizo la damu,Pima protini kwenye mkojo na Pima jinsi figo zinavyochuja uchafu kutoka kwenye damu(GFR).

Utambuzi

Matatizo ya ugonjwa wa figo uliokaa kwa muda ni yapi?
Figo zinapozidi kudhoofika yaweza kuleta hathari nyingine hata kuhatarisha maisha.

Matatizo yenyewe ni kama yafuatayo:

  • Kushindwa kupumua na maumivu ya kifua kwa sababu ya ongezeko la maji hasa kwenye mapafu,na shinikizo la damu la juu sana.
  • Kichefuchefu kingi na kutapika.
  • Kuchoka kwingi/ kukosa nguvu mwilini.
  • Matatizo katika mfumo wa neva kwa mfano kuchanganyikiwa, kusinzia, na hata kuzimia.
  • Ongezeko la juu la potasiamu kwenye damu (hyperkalemia),jambo ambalo ni hatari sana kwani linaweza kudhohofisha utendaji kazi wa moyo hata kuleta kifo cha ghafla.
  • Kuvimba kwa utando uzungukao moyo (pericardium).

Utambuzi wa ugonjwa sugu wa figo

Mapema,ugonjwa huu hauna dalili.Ni vipimo vya hospitalini tu vinavyoweza kuonyesha shida hii inapoanza.Iwapo unashuku ugonjwa wa figo ,agiza vipimo vya hospitali vya shinikizo la damu, protini kwenye mkojo na creatinini kwenye damu.

1. Himoglobini
Himoglobini ni protini ya damu inayosaidia damu kusambaza hewa ya oksijeni mwilini. Kwa mtu mwenye ugonjwa wa figo, himoglobini huwa kidogo.Hii ni anemia kwa sababu ya ukosefu wa protini (erythropoitini) inayotengenezwa na figo.

Figo kupooza na kuwa ndogo (kusinyaa) ni ishara kuu ya ugonjwa wa figo.
2. Kipimo cha mkojo

Kupatikana kwa protini kwenye mkojo ( albuminuria au proteinuria) ni dalili ya mapema ya ugonjwa sugu wa figo.Hata kama protini inayopatikana ni kidogo sana,hii inaweza kuashiria ugonjwa huu hasa kwa wale wenye ugonjwa wa kisukari.Protini inaweza kupatikana kwenye mkojo kwa sababu ya homa au mazoezi mazito.Kwa sababu hii,ni muhimu kuhakikisha kwanza kuwa uwepo wa protini kumesababishwa na hali nyingine yoyote kabla ya kusema thahiri kumesababishwa na ugonjwa sugu wa figo. (CKD).

3. Kipimo cha creatinini ya damu, yurea na ki le kinachoonyesha kiwango cha kazi ya figo ya kuchuja uchafu kutoka kwa damu (eGFR)

Hivi ndivyo vipimo vya kawaida vinavyofanywa kuchunguza na kufuatia ugonjwa wa figo.Iwapo figo zinazidi kudhoofika,Kiasi cha creatinini na yurea kwenye damu huongezeka.Kurudia kupimwa mara kwa mara husaidia kujua jinsi ugonjwa unavyoendelea na iwapo dawa zinaleta nafuu au la.

Kiwango cha kreatinini kwenye damu ni ishara muhimu ya kuonyesha jinsi figo inavyo fanya kazi.Hata hivyo kipimo kinachoonyesha jinsi figo zinavyochuja uchafu kutoka kwenye damu (GFR) ndicho huwa sahihi zaidi.Hiki huweza kuonyesha ugonjwa wa figo mapema na kinaweza kutegemewa kuliko kile cha kreatinini ya damu pekee. Kipimo cha kazi ya figo ya kuchuja uchafu huhesabiwa kutokana na umri, jinsia na kiasi cha kreatinini ya damu.

Kipimo hiki (eGFR) ni muhimu kwa kutambua na kufuatia jinsi ugonjwa unavyoendelea na ukali wake.Kwa kuzingatia kipimo hiki,ugonjwa wa figo umegawanywa katika viwango au hatua tano.Hatua hizi ni muhimu katika kujua uchunguzi gani zaidi unahitajika na jinsi ya kukabiliana na ugonjwa.

Homa, Kuzidi kwa dalili au dalili mpya zinazo hashiria utendaji mbaya wa figo, haya yoteyanahitaji kutibiwa/kushughulikiwa mara moja.
4. Picha za figo( Ultrasound)

Kipimo hiki ni rahisi na cha kutegemewa katika kutambua ugonjwa sugu wa figo.Figo zilizosinyaa ni ishara ya ugonjwa.Hata hivyo,figo zinaweza kuonekana kawaida au kubwa zaidi iwapo ugonjwa umesababishwa na uvimbe (polycystic kidneys),kisukari au amyloidosis. Picha hizi huweza pia kuonyesha ugonjwa uliosababishwa na kuziba kwa njia ya mkojo au na mawe ya figo.

5. Vipimo vingine

Ugonjwa sugu wa figo hutatiza kazi kadha za figo.Ili kutathmini matatizo haya,vipimo mbalimbali hufanywa.Vipimo vya damu ambavyo kwa kawaida hufanywa ni vya usawa wa asidi mwilini, (sodium, potasiamu,magnesia, bicarbonate) vipimo vya anemia (hematocrit,ferritin, kiasi cha transferritin na muonekano wa damu – peripheral smear) vipimo vya ugonjwa wa mifupa (calcium,phosphorus,alkaline phosphatase,parathyroid hormone), moyo, kisukari,himoglobini ya damu,na vipimo vingine vya kawaida katika magonjwa haya kama sukari kwenye damu, serum albumin, cholesterol, triglycerides, ECG, echocardiography…..nk.

Mgonjwa wa figo anafaa kumwona daktari lini?

Mgonjwa anafaa kumwona daktari mara moja akipata:

  • Kuongezeka kwa uzito ghafla, kupungua kwa kiasi cha mkojo, kuvimba na kushindwa kupumua hasa anapolala.
  • Maumivu ya kifua na moyo kupiga haraka au polepole sana.
  • Homa, kuharisha sana, kukosa hamu ya chakula, kutapika sana na pengine kuwa na damu kwenye matapishi au kupungua uzito.
  • Misuli kukosa nguvu ghafla.
  • Shinikizo la damu kuzidi hata baada ya juhudi nzuri ya kutibu.
  • Mkojo mwekundu au wenye damu nyingi.