Utangulizi na Yaliyomo

Kidney Failure

Mwongozo Kamili Kwa Wagonjwa Wa Figo

OKOA FIGO LAKO

Ujumbe Kamili Juu ya Kukinga na Kuponya Magonjwa ya Figo





Dr Gabriel L. Upunda
Dar es Salaam, Tanzania

Dr Bashir Admani
Nairobi, Kenya

Dr Sanjay Pandya
Rajkot, India

OKOA FIGO LAKO

Mchapishaji
TMJ Hospital,Mikocheni, Dar es Salaam, Tanzania



© Samarpan Kidney Foundation
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kukitoa kitabu hiki kwa namna yoyote ile: iwe kwa mfumo wa elektroni ikiwa pamoja na mfumo wowote wa kuhifadhi na kutoa taarifa, bila idhini ya mchapishaji. Kitabu hiki huchapishwa India na kwa hiyo kisifanyiwe biasharanje (exported), bila kupata ruhusa kwanza kwa maandishi kutoka kwa mchapishaji. Kama kutatokea utata wowote wa kisheria, utata huo utasuluhishwa tu chini ya sheria ya Rajkot, India.




Toleo la kwanza : 2015

bei:TZS


Mwandishi
Dr Gabriel L Upunda
Mganga Mkuu Wa Serikali (Mstaafu) Wizara Ya Afya Na Ustawi wa Jamii SLP 5720
Dar es Salaam, Tanzania.






Kitabu Hiki Kimetolewa Kwa
Ukumbusho Wa Wagonjwa Wote Wa Figo






Hebu tujikinge na magonjwa ya figo

Kitabu hiki “Okoa Figo Lako” ni jitihada ya makusudi ya kutoa maelezo ya msingi ya jinsi ya kujikinga na magonjwa ya kawaida ya figo.

Kwa miongo kadha iliopita kumekuwa na mlipuko wa kuogofya na wa kuongezeka kwa maradhi ya figo. Magonjwa ya figo yaliyozidi na yasiyotibika yamekua kwa wingi. Kwa sababu hiyo kuwaeleza watu sababu, dalili na mbinu za kujikinga na magonjwa haya ni mbinu bora ya kupambana na ongezeko hili la kusumbua. Kitabu hiki ni mchango wetu wa kujaribu kumpa mtu wa kawaida ujumbe muhimu kwa maneno rahisi.

Uchunguzi, utambuzi na matibabu ya mapema ya ugonjwa huu ni muhimu kwa vile humpa mgonjwa manufaa ya gharama ndogo ya matibabu. Kwa kutokujua watu wachache kabisa hutambua ishara na dalili zinazoonyesha uwezekano wa kuwa na ugonjwa wa figo, nao pia hucheleweshwa kwa uchunguzi na kupewa matibabu kama dialysis au kubadilisha figo ambayo ni ghali mno na hata katika nchi kama india ni wachache tu, kama asilimia kumi (10%) ya wagonjwa wote, huweza kumudu gharama hizo. Kwa hiyo uchunguzi na utibabu wa mapema zinabaki kuwa njia pekee inayoweza kupunguza mlipuko wa ugonjwa wa figo uliokomaa katika nchi yetu.

Uchunguzi unaonyesha kuwa mtu akigundulika anaugua ugonjwa wa figo, mgonjwa na familia yake huwa na mawazo mazito na wasiwasi. Wagonjwa wa figo na familia zao hupenda kujua kila kitu juu ya ugonjwa. Lakini si rahisi kwa daktari anayetibu kuwapa maelezo mengi. Tunatumaini kitabu hiki kitajenga daraja kati ya daktari na mgonjwa. Hata hivyo ni msaada kuwa na kitabu cha maelezo ili husome kwa wakati wako na kukipitia mara nyingi unavyohitaji. Kukupa ujumbe

wote wa msingi juu ya dalili, uchunguzi na matibabu ya magonjwa mbalimbali ya figo kwa lugha rahisi na nyepesi. Maelezo ya kuchagua na jinsi ya kujikinga kwa vyakula vinavyopendekezwa kwa magonjwa mbalimbali ya figo yote yametolewa hapa. Tunahitaji kusisitiza na kulenga kwa kusema hapa kuwa ujumbe unaopatikana katika kitabu hiki si usaidizi wa kimatibabu; ni kwa kukupa ujumbe pekee. Matibabu binafsi au kubadilisha vyakula kwa kusoma kitabu hiki, bila ushauri wa daktari yaweza kuwa hatari, hatushauri na haikubaliki kabisa.

Mwongozo huu wa figo utakuwa muhimu si tu kwa wagonjwa wa figo na famila zao tu bali hata kwa wale waliohatarini kupata ugonjwa wa figo. Na utatoa mafunzo kwa wale watu ambao hupenda kujua.. Madaktari, wanafunzi wa matibabu, matabibu waliofunzwa kusaidia kutibu, wanahaki ya kupata kitabu hiki ili kiwe msaada wa karibu.

Tunamshukuru sana Mr. Pravin V. Pindoriya na Timu yake (Nairobi – Kenya) kwa msaada wao mkubwa wa kutafsiri kitabu hiki kutoka kiingereza kwenda Kiswahili. Tunapenda kuwashukuru pia Dr T. M Jafferji, Mkurugenzi Mtendaji, Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam, na Mrs. Parul Chayya, Mtendaji Mkuu, TMJ Hospital, kwa kuunga mkono kwa hali na mali na ushauri katika shughuli hii.

Natumaini wasomaji watakaopata kitabu hiki wataona umuhimu wake na chenye kuelimisha. Mapendekezo yanakaribiswa ya kuboresha kitabu hiki.

Tunawatakia wote afya njema.

Dr Gabriel L. Upunda
Dr Bashir Admani
Dr Sanjay Pandya

Kuhusu waandishi

Dr Gabriel L. Upunda MD, M. Med; MPH
Dr G. L. Upunda alisomea Udaktari katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (1972), Alimaliza masomo ya uzamili katika Kutibu (Internal Medicine) mwaka 1978) katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na mwaka 1993 alimaliza mafunzo ya uzamili (Masters in Pubic Health) huko Johns Hopkins School of Public Health, USA.

Amekuwa Mganga wa Wilaya, Mganga wa Mkoa (mara mbili), na kwa zaidi ya miaka kumi na tano amekuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kama kiongozi wa Afya Ya Msingi, Mkurugenzi wa Tiba na hatimae alikuwa Mganga Mkuu Wa Serikali kwa takriban miaka kumi. Dr G L Upunda amefanya kazi pia Shirika La Afya Ulimwenguni (WHO - AFRO).

Dr. Bashir Admani M.B.Ch.B, M. Med ((Paediatrics), C. Neph. (Paed)
Dr Bashir Admani alimaliza mafunzo yake ya Udaktari (1998) na kufanya mafunzo ya uzamili katika fani ya watoto (2004) kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya. Alipata mafunzo maalumu ya ubingwa wa juu katika magonjwa ya figo kwa watoto katika Red Cross Memorial Childrens’ ospital, Cape Town, Afrika ya Kusini. Sasa hivi anafanya kazi ya Udaktari Bingwa wa Figo kwa Watoto katika Hospitali ya Chuo Kikuu Cha Aga Khan. Nairobi, Kenya. Yeye ni Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Figo kwa Watoto, Hospitali ya Nairobi. Wakati tunapoandika Dr Bashir Admani ni Katibu wa African Paediatric Nephrology Association (AFPNA).Aidha anatoa huduma zake pia kama Mweka Hazina wa Kenya Renal Association.

Dr Sanjay Pandya

Dr Sanjay Panya ni Daktari Bingwa Mwandamizi wa Figo ambaye anafanya kazi Rajkot ( Gujarat – India). “Kidney Education Foundation” imeanzishwa naye ikiwa na kazi maalumu ya kusambaza ujumbe kwa watu wengi ili kuzuia na kutibu magonjwa ya figo.Kitabu cha FIGO kwa wagonjwa katika lugha za kiingereza, Hindi, Gujarat na Kutchi kimeandikwa naye. Kwa kushirikiana na timu ya madaktari bingwa kutoka sehemu mbalimbali duniani, vitabu vya kuelimisha wagonjwa wa figo vimetayarishwa katika lugha zaidi ya 20.

Ili kuwasaidia watu na wagonjwa wa figo wengi zaidi sehemu mbalimbali duniani, Dr Pandya na timu yake wameanzisha mtandao www.KidneyEducation.com. Kupitia mtandao huu unaweza kuvipata vitabu zaidi ya 230 katika zaidi ya lugha 20. Aidha katika miezi 60 watu wameingia kwenye tuvuti hii zaidi ya mara milioni 20.

Kwa hivi sasa kitabu hiki kwa wagonjwa kinapatikana katika kiingereza, kichina, kihispania, kijapani, kiitalia, kihindi, kiarabu, kireno, kibangla, kiurdu na lugha nyingine kumi za kihindi.

Yaliyomo

Sehemu 1: Mambo ya misingi kuhusu figo

Sura ya 1 Utangulizi 1
Sura ya 2 Figo na Kazi Yake 3
Sura ya 3 Dalili za Magonjwa ya Figo 10
Sura ya 4 Utambuzi wa Magonjwa ya Figo 13
Sura ya 5 Magonjwa Makuu ya Figo 21
Sura ya 6 Nadharia Potofu na Ukweli Juu ya Magonjwa ya Figo 27
Sura ya 7 Kuzuia Magonjwa ya Figo 32

Sehemu 2: magonjwa makuu ya figo na matibabu

figo Kushindwa

Sura ya 8 Kushindwa kwa Figo ni Nini? 39
Sura ya 9 Kushindwa Ghafla kwa Figo 41
Sura ya 10 Ugonjwa Sugu wa Figo: Chanzo 46
Sura ya 11 Ugonjwa Sugu wa Figo: Dalili na Utambuzi48
Sura ya 12 Ugonjwa Sugu wa Figo: Matibabu 55
Sura ya 13 Dayalisisi 64
Sura ya 14 Kubadilisha Figo86

Magonjwa mengine makuu ya figo

Sura ya 15 Ugonjwa wa Kisukari wa Figo 106
Sura ya 16 Ugonjwa wa Figo wa Polisitiki(Polycystic) 115
Sura ya 17 Kuishi na Figo Moja 121
Sura ya 18 Maambukizi ya Mfumo wa Mkojo 124
Sura ya 19 Ugonjwa wa Mawe Katika Figo 131
Sura ya 20 Uvimbe Usio wa Saratani kwenye Tezi Dume(BPH) 145
Sura ya 21 Dawa ya Matatizo ya Figo 157
Sura ya 22 Nephrotic Syndrome 162
Sura ya 23 Maambukizi ya Mfumo wa Mkojo kwa Watoto 176
Sura ya 24 Ugonjwa wa Kukojoa Kitandani 188

Lishe katika magonjwa ya figo

Sura ya 25 Lishe katika Ugonjwa Sugu wa Figo193
Maelezo 210
Vifupisho 218
Vipimo vya Kawaida vya Damu Kwa Wagonjwa wa Figo 220
Ripoti 222

Jinsi ya kutumia kitabu hiki

Kitabu hiki kimo katika sehemu mbili

Sehemu ya 1:

Katika sehemu hii, ujumbe wa msingi juu ya figo na kujikinga na magonjwa ya figo yameelezwa. Kila mtu anashauriwa kusoma sehemu hii ya kitabu hiki.. Ujumbe uliotolewa waweza kukuletea mabadiliko kwa msomaji, kwa vile hunamuandaa msomaji wa kawaida kutambua na kujikinga na magonjwa ya figo.

Sehemu ya 2:

Msomaji anaweza kusoma sehemu hii kwa kutaka tu kujua au ikiwa inabidi/ lazima.

Katika sehemu hii
  • Ujumbe kuhusu magonjwa makuu ya figo, dalili, uchunguzi, kinga na matibabu yameshughulikiwa.
  • Magonjwa yanayoharibu figo kama kisukari, kupanda kwa damu / shinikizo la damu, polycystic kidney……nk) na tahadhari za kujikinga na ujumbe mwingi muhimu umeelezwa.
  • Maelezo ya ndani/maksusi kuhusu lishe bora kwa ugonjwa wa figo uliozidi.
Ujumbe katika kitabu hiki sio matibabu Ya daktari; tiba bila ushauri wa Daktari huenda ikawa hatari.