Magonjwa ya figo huua kimya kimya. Yanaweza kusababisha kuendelea kwa kupotea  kwa kazi ya figo na kuelekea kwa hitilafu ya figo na hatimae  kuhitaji dayalisisi au kubadilisha kwa figo ili kudumisha maisha. Kwa sababu ya  gharama kubwa na shida za  kupatikana katika nchi zinazoendelea asili mia 5-10% ya  wagonjwa  wa hitilafu  ya figo  hupata matibabu kama dayalisisi na kubadilisha figo, wakati waliobaki hufa bila kupata  tiba.  Ugonjwa sugu wa figo ni tatizo kubwa sana na hauna tiba, kwa hiyo kinga ndio njia pekee. Ugunduzi na matibabu ya mapema huweza kuzuia hali ya ugonjwa sugu wa figo kuwa mbaya sana, na huweza kuzuia au kuchelewesha hata haja ya dayalisisi au kubadilisha/ kupandikizwa  figo.
Ni vipi  tunaweza kuzuia magonjwa ya figo? 
Usipuuze figo zako. Mambo  muhimu  kuhusu kinga na  utunzaji  wa figo lenye ugonjwa  wa figo yamejadiliwa  katika sehemu mbili:
    - Tahadhari kwa mtu mwenye afya.
 
    - Tahadhari kwa mtu mwenye ugonjwa wa figo.
 
Tahadhari kwa mtu mwenye afya
Njia  saba zinazofaa  za  kuweka  figo kuwa  zenye  afya  ni :
1. Kuwa mtu mwenye afya na mwenye kufanya mazoezi (Be fit and active)
Mazoezi ya kila mara  na shughuli  za  kimwili za  kila siku  hudumisha msukumo  wa kawaida wa damu na  hudhibiti kisukari. Shughuli za kimwili huondoa  hatari ya  kisukari, na  msukumo wa juu  wa damu hivyo  basi  kupunguza  hatari ya  ugonjwa  sugu  wa figo.
                         
                    
                       
                            
                            2. Lishe bora
Kula lishe yenye afya, matunda na mboga mboga. Punguza  ulaji  wa vyakula vilivyosagwa, sukari , mafuta na nyama, chumvi  kidogo hasa baada ya umri  wa miaka  40 itasaidia  kuzuia  msukumo  wa juu wa damu  na kuwepo kwa mawe ya figo.
3. Chunga  uzito wako 
Dumisha uzito wako na lishe bora na mazoezi stahiki. Hii inaweza kuzuia kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa sugu ya figo na hali nyingine zinazohusishwa na ugonjwa sugu wa figo.
4. Acha  uvutaji   wa  tumbaku  na matumizi  ya mazao  ya tumbaku 
Uvutaji wa tumbaku na matumizi mengine ya tumbaku yanaweza kusababisha atherosclerosis. Hii inaweza kupunguza mtiririko wa  damu hadi kwenye figo na hivyo  kupunguza  uwezo  wa figo kufanya kazi vyema.
5. Jihadhari na OTCs 
Jihadhari na usizidishe matumizi ya dawa  za  kupunguza /kutuliza maumivu zinazonunuliwa bila karatasi ya Daktari (Prescription) kwenye kaunta. Dawa za kawaida  kama non-steroidal anti-inflammatory kama ibuprofen zinajulikana kusababiaha uharibifu wa figo na hitilafu ya figo, zikitumiwa mara kwa mara. Pata ushauri wa daktari jinsi ya kudhibiti maumivu yako bila kuhatarisha figo zako.
6. Kunywa maji mengi 
Unywaji wa maji ya  kutosha ( Kiasi cha lita  3 kila  siku ) husaidia kuzimua mkojo, kutoa uchafu wote wa  sumu  kutoka mwilini na  kuzuia mawe kwenye  figo.
7. Uchunguzi wa figo wa kila mwaka 
Magonjwa ya figo huwa magonjwa yanayoingia mwilini kimya kimya na hayatoi dalili zozote hadi yafikie  hatua  ya  kuimarika. Mbinu sahihi na bora lakini inayotumika kwa nadra sana ni uchunguzi wa mara kwa mara.  Utambuzi wa mapema na kuzuia magonjwa ya figo inaweza kufanyika tu kwa uchunguzi wa kila mwaka. Watu walio kwenye hatari zaidi, kwa mfano wenye kisukari, unene kupita  kiasi au walio na  historia ya familia  ya magonjwa haya ya figo ni vema wakafanya uchunguzi wa kila mwaka wa afya na hasa figo.
Ukipenda figo zako (Na hii ni muhimu zaidi kwako wewe mwenyewe) usisahau kupata uchunguzi wa mara kwa mara na hasa baada ya umri wa miaka 40. Njia rahisi  ya ugunduzi  wa mapema  wa  ugonjwa  wa figo ni upimaji wa  msukumo wa damu kila mwaka, upimaji wa  mkojo na upimaji wa kreatinini  kwenye  damu.
                         
                    
                       
                            
                            Tahadhari  Kwa Wagonjwa Wa Figo
1. Uhamasishaji kuhusu magonjwa ya figo na utambuzi wa mapema
Kuwa macho na makini ili utambue dalili za ugonjwa wa figo. Dalili  za kawaida  ni kuvimba  kwa uso na miguu, kukosa hamu ya chakula, homa, kutapika, udhalifu, kukojoa kila mara, damu kwenye mkojo au kuwepo  kwa protini  kwenye mkojo. Wakati wa matatizo kama hayo, inashauriwa  kupata ushauri  wa daktari ili upate upimaji wa figo.
2. Tahadhari za  kisukari 
Kwa kila mgonjwa wa kisukari, tahadhari za  kuzuia ugonjwa wa figo ni muhimu kwa  sababu kisukari  ndio sababu kuu  ya  ugonjwa  sugu wa figo(CKD) na  hitilafu  ya figo  kote duniani. Takriban asili mia 45% ya wagonjwa wapya wa hatua ya mwisho ya ugonjwa wa figo hutokana na kisukari. Kwa utambuzi wa mapema wa ugonjwa wa figo utokanao na kisukari njia rahisi na sahihi ni upimaji wa  mkojo ili kubaini kuwepo kwa protini na msukumo wa damu kwa kila miezi mitatu. Upimaji bora zaidi wa utambuzi wa mapema  kwenye kisukari  ni upimaji wa maikroalbuminuria (MA) kwenye mkojo, ambao unafaa kufanywa kila mwaka. Aidha pima  kreatinini  ya damu (  na e GFR) ili kuchunguza kazi  ya  figo angalau  mara moja  kila mwaka.
                         
                    
                       
                            
                            Msukumo wa juu wa damu, kuwepo kwa protini kwenye mkojo, kuvimba, upungufu wa sukari kwenye  damu wa kila mara  na  kuonekana kwa dalili za kisukari kwenye jicho(diabetic retinopathy) ni vidokezo muhimu kwa figo kuhusishwa na  kisukari. Jihadhari  na ishara  hizi hatari  na  upate  ushauri wa daktari  wako mapema.
Ili kujikinga na ugonjwa wa kisukari ya figo, wagonjwa wote wa kisukari wana wajibu wa kudhibiti kwa uangalifu sana kisukari, kudumisha msukumo wa  damu uwe chini ya 130/80 mm ya Hg(ace. Inhibitor au ARB ni dawa zinazopendekezwa kwa kudhibiti msukumo wa juu wa damu) punguza kiwango cha protini kwa lishe na dhibiti mafuta.
3. Tahadhari kwa wagonjwa wenye msukumo wa juu wa damu 
Msukumo wa juu wa damu ndio chanzo cha pili muhimu cha ugonjwa sugu wa figo ambacho kinazuilika. Na kwa kuwa wagonjwa wengi wenye tatizo la msukumo wa damu hawaonyeshi dalili zozote, wengi husitisha matibabu kwa muda na wachache husitisha matibabu kabisa kwa kuwa wao huhisi vyema bila dawa. Lakini hii ni hatari. Msukomo usiodhibitiwa kwa muda mrefu huweza kusababisha shida na  hatari kama ugonjwa  sugu  wa figo , moyo kusimama ghafla na kupooza.
Ili kukinga ugonjwa wa figo, wagonjwa wote  wa msukumo wa juu wa damu , wanatakiwa kunywa dawa zao kila mara/kila siku, kuchunguzwa msukumo wa damu na kuwa na lishe/mlo bora  na kuepuka  mlo wenye chumvi. Madhumuni yawe kuweka presha /msukumo wa damu kuwa chini ya 130/80mm ya Hg. Ili kutambuwa mapema uharibifu wa figo wagonjwa wote wenye msukumo wa damu wachunguzwe mkojo na kreatinini ya damu kila mwaka.
4. Tahadhari kwa ugonjwa sugu wa figo 
Ugonjwa sugu wa figo hautibiki. Lakini  utambuzi wa mapema na udhibiti wa mlo,na kufuatia maelekezo ya matibabu bora itapunguza mwendelezo wa ugonjwa na kuchelewesha hatua ya matumizi ya dayalisisi au kubadilisha figo.
                         
                    
                       
                            
                            Udhibiti thabiti wa  msukumo wa  juu wa  damu ni hatua muhimu ya kuzuia  kwendelea  kwa ugonjwa  sugu wa figo. Inapendekezwa sana kuweka msukumo wa damu kuwa 130/80 mm Hg au chini. Njia nzuri ya kuthibiti msukumo wa damu ni kupima mara kwa mara hata nyumbani na kuandika sehemu ili kumsaidia daktari wako kuamua kiasi gani cha dawa akupe.
Kwa wagonjwa wenye CKD, vidokezo kama msukumo wa chini wa damu (hypotension),kupungua maji mwilini (dehydration), kuwa na kizuizi kwenye mfumo wa mkojo (obstruction), maambukizi kwenye damu (sepsis), dawa zinazoumiza figo……nk lazima zitambuliwe. Kuchukuliwa hatua za haraka katika vidokezo hivi kunaweza kuleta nafuu kwa figo hata katika hali ya CKD.
5. Utambuzi na matibabu ya ugonjwa wa polisistiki ya figo (PKD) 
Ugonjwa huu (ADPKD) ni hitilafu ya figo ambayo hurithiwa na hujumuisha asili mia 6-8 % ya wagonjwa walio katika dayalisisi. Mtu mzima ambaye ana historia ya ugonjwa huu wa figo yuko katika hatari kubwa sana na anastahili kuchunguzwa mapema  na  picha  ya ultrasound ili ugonjwa ugundulike mapema. PKD haina tiba, lakini hatua kama kudhibiti msukumo wa juu wa damu, matibabu  ya maambukizi ya mfumo  wa mkojo, kuthibiti lishe na  usaidizi  wa matibabu(supportive treatment)  husaidia kudhibiti   dalili,  kuzuia matatizo makubwa (complications), na kupunguza kasi ya utendaji kazi wa figo.
6. Utambuzi  na matibabu  ya mapema  ya maambukizi  ya mfumo wa mkojo kwa watoto
Maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI) lazima uhisiwe wakati mtoto anapata baridi isiyoelezeka, kukojoa kila mara, kuchomwa wakati wa kukojoa, ukosefu wa hamu ya kula na ongezeko mbaya wa uzito.
                         
                    
                       
                            
                            Ni muhimu kukumbuka kuwa kila maambukizi ya mfumo wa mkojo yanapotokea (UTI), hasa yenye homa husababisha uharibifu wa figo hasa isipotambuliwa, tiba ikiwa imechelewa au kutomaliza matibabu. Uharibifu unaoweza kutokea ni pamoja na figo kuwa na makovu, figo kutokukua, msukumo wa juu wa damu, na figo kushindwa kufanya kazi baadae katika maisha. Kwa sababu hii maambukizi haya kwa watoto hayahitaji tu utambuzi wa mapema au matibabu ya haraka, bali pia tathmini makini ili kubaini vihashiria vingine, hatari au athari nyingine. Vesicoureteral reflux (VUR) ndiyo chanzo  kikuu cha maambukizi haya na huleta karibu asili mia 50%  ya jumla ya maambukizi yote wakati wa utoto. Ufuatiliaji ni muhimu sana kwa watoto waliopatwa  na UTI.
7. Maambukizi ya mfumo wa mkojo unaojirudia  rudia kwa watu wazima 
Wagonjwa wote wenye maambukizi ya mfumo wa mkojo yenye kujirudia rudia wanahitaji kujua sababu zake. Baadhi ya sababu ni uzibaji wa mkondo wa mkojo, tiba isiyo kamili, ugonjwa wa mawe n.k) Matatizo haya yasipotibiwa vizuri huweza kuharibu figo. Kwa hiyo utambuzi wa mapema na matibabu ya vyanzo vya tatizo kujirudia rudia ni muhimu.
8. Matibabu sahihi ya ugonjwa wa mawe Na kuvimba kwa tezi dume (BPH) 
Wagonjwa wengi wanaouguza ugonjwa wa mawe hawana dalili zozote kwa hivyo wanakosa kugundua ugonjwa na kukosa utambuzi na matibabu yake kwa wakati/ mapema. Wanaume wengi wazee walio na tezi dume (BPH) hawatambui dalili zake kwa muda mrefu. Tatizo la mawe na tezi dume kama hayakutibiwa mapema na kwa wakati huweza kuleta uharibifu kwenye figo. Ufuatiliaji sahihi na tiba ya wakati husaidia sana kulinda figo.
9. Usipuuze msukumo wa damu katika umri mdogo 
Msukumo wa damu katika umri mdogo si kitu cha kawaida na kwa hiyo huhitaji uchunguzi kamili wa chanzo chake. Magonjwa ya figo ndiyo yanaweza kusababisha msukumo wa juu wa damu kwa vijana. Kwa kila kijana mwenye msukumo wa juu wa damu anahitaji kufanyiwa utambuzi wa magonjwa ya figo na matibabu sahihi ili kulinda figo ya mgonjwa huyu.
                         
                    
                       
                            
                            10. Matibabu ya mapema ya hitilafu kali ya figo 
Vyanzo muhimu vya hitilafu kali ya figo ni kushuka ghafla kwa utendaji wa figo. Hii utokea katika matatizo yafuatayo: kuhara, kutapika, malaria (hasa aina ya falsiparumu), maaambukizo katika damu (sepsis), madawa mengine (ACE inhibitor, NSAID’s) n.k matibabu ya mapema na bora ya vyanzo  hivi  huweza kuzuia hitilafu ya figo.
11. Tahadhari kuhusu matumizi ya dawa 
Kuwa mwangalifu. Dawa nyingi zinazonunuliwa dukani hasa za kutuliza maumivu, zina hatari ya kusababisha uharibifu wa figo hasa kwa wazee. Dawa kama hizo zinatangazwa bila kueleza hatari zinazobainishwa kwa wanunuzi. Acha matumizi ya dawa hizi kwa mauimivu ya kichwa na mwili. Pia usijitibu mwenyewe na dawa zisizofaa. Ni vyema kupata maelezo na maelekezo ya daktari kuhusu  matumizi salama ya dawa. Ni vibaya kuamini kuwa dawa zote za asili na badala (Ayurvedic medicines, Chinese herbs….nk) pamoja na virutubisho vya vyakula (dietary supplements) si hatari.
Vyuma vizito vilivyo kwenye dawa za Ayurvedic vinaweza kusababisha uharibifu wa figo.
12. Tahadhari kwa figo moja 
Watu walio na figo moja huishi maisha sawa na yenye afya. Kwa kuwa watu hawa hawana figo nyingine, tahadhari lazima zichukuliwe. Mgonjwa adhibiti msukumo wa damu, anywe maji mengi, awe na lishe bora, apunguze /adhibiti ulaji wa chumvi, asile vyakula vyenye viwango vya juu vya protini, na kwa namna yoyote ile azuie jeraha la hiyo figo moja. Tahadhari muhimu zaidi ni uchunguzi wa kiafya wa mara kwa mara. Inafaa amuone daktari mara moja  kwa mwaka  ili kuchunguza kazi  ya  figo kwa  kuangalia msukumo wa  damu, upimaji wa mkojo na damu,  pia upimaaji wa ultra sonogramu ,iwapo inahitajika.