25: Lishe katika Ugonjwa Sugu wa Figo

Lishe Katika Ugonjwa Sugu wa Figo

Wajibu mkuu wa figo ni kutoa uchafu na kusafisha damu. Pamoja na kazi hii, figo huwa na wajibu wa kutoa maji ya ziada , madini na kemikal i na husawazisha maj i na madini kama sodiamu,potassium,kalsiamu,fosfera na biocarbonate mwilini.

Kwa wagonjwa wanougua ugonjwa sugu wa figo (CKD), udhibiti wa maji na elektrolaiti unaweza kuvurugika. Kwa sababu hii, hata unywaji wa kawaida wa maji, chumvi ya kawaida au potassium inaweza kusababisha usumbufu mkubwa wa usawazishaji wa maji na elektrolaiti.

Ili kupunguza mzigo kwenye figo iliyodhohofika na kuzuia usumbufu wa usawazishaji wa maji na elektrolaiti, wagonjwa wenye ugonjwa sugu wa figo wanafaa kurekebisha lishe yao kulingana na maelekezo ya daktari au mtaalamu wa lishe. Hakuna lishe maalumu kwa wagonjwa wa CKD. Kila mgonjwa hupewa ushauri tofauti wa lishe kulingana na hali yake ya afya, na hatua ya hitilafu ya figo au shida nyingine za kiafya. Ushuri wa lishe unaweza kubadilishwa hata kwa mgonjwa yule yule kwa wakati tofauti.

Malengo ya matibabu ya lishe kwa wagonjwa wa CKD ni:

  1. Kupunguza ukuaji wa ugonjwa sugu wa figo na kuahirisha hitaji la dayalisisi.
  2. Kupunguza mathara ya yurea nyingi kwenye damu.
  3. Kudumisha hali halisi ya lishe na kuzuia kupotea kwa uzito wa kawaida wa mwili.
  4. Kupunguza hatari ya usumbufu wa maji na elektrolaiti.
  5. Kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo

Kanuni za jumla za matibabu ya lishe kwa wagonjwa wa CKD ni:

  • Zuia ulaji wa protini hadi 0.8 gm/kg ya uzito wa mwili kwa siku.
  • Toa kabohaidreti ya kutosha ili kuleta nguvu.
  • Toa kiwango cha wastani cha mafuta. Punguza ulaji wa siagi, samli na mafuta.
  • Zuia unywaji wa maji iwapo kuna uvimbe wa mwili.
  • Zuia kiwango cha sodiamu, potasiumu, na fosferasi kwenye chakula.
  • Wagonjwa wapewe vitamin na elementi ndogo ndogo kwa kiwango cha kutosha na vyakula vyenye nyuzi nyuzi (high fiber diet) vinapendekezwa.

Zuia ulaji wa protini

Ufafanuzi wa uchaguzi na ubadilishaji wa lishe ya wagojwa wenye CKD :
1. Zuia ulaji wa protini

Protini ni muhimu kwa kutengeneza na udumishaji wa mwili pia husaidia kuponyesha vidonda na kupigana na maambukizi .

Kabla ya dayalisisi, zuia vyakula vyenye viwango vikubwa vya protini. Zuia ulaji wa protini hadi 0.8 gm/Kg ya uzito wa mwili kwa siku. Protini yenye thamani ya juu au asili inapendekezwa.

Uzuiaji wa protini hupunguza kasi ya kazi za figo, hivyo basi huchelewesha hitaji la dayalisisi na kubadilisha figo. Uzuiaji wa protini hupunguza utoaji wa yurea na hupunguza dalili zinazohusishwa na kiwango cha juu cha yurea. Lakini jihadhari na kusitisha protini kabisa. Kukosa hamu ya kula hutokea sana kwa wagonjwa wa CKD.

Kabla ya wakati wa dayalisisi, uzuiaji wa ulaji protini ni wa manufaa, lakini komesha uzuaji usiofaa.

Ukosefu wa hamu ya kula ni kawaida kwa wagonjwa wa CKD. Ukosefu huu na uzuiaji wa moja kwa moja wa protini huweza kusababisha lishe duni, kupoteza uzito, ukosefu wa nguvu na kupungua kwa kinga mwilini ambayo huongeza hatari ya kifo.

Baada ya uanzishaji wa dayalisisi, kiwango cha juu cha protini kinapendekezwa. Hasa wagonjwa kwa CAPD lazima wale kiwango cha juu cha protini ili kurudisha protini inayopotea kwenye maji wakati wa dayalisisi.

Ulaji wa kiwango cha juu cha kalori

2. Ulaji wa kiwango cha juu cha kalori
Mwili huhitaji kalori kwa shughuli za kila siku na pia kudumisha halijoto, ukuaji na uzito wa kutosha wa mwili. Kalori hupatikana hasa kwenye kabohaidreti na mafuta. Mahitaji ya kalori kwa wagonjwa wa CKD ni 35-40 kcals/kg kwa uzio wa mwili kwa siku. Iwapo ulaji wa kalori hautoshi, protini husaidia kutoa kalori. Huu usagaji wa protini unaweza kusababisha athari kama utapiamlo na uzalishaji mkubwa wa uchafu. Kwa hiyo, ni muhimu sana kumpa mgojwa kiwango cha kutosha cha kalori kulingana na uzito wake wa zamani na siyo uzito wake anapopimwa. Uzito unaweza kubadilika kwa sababu ya shida alizokuwa nazo awali kama utapiamlo au kisukari na ugonjwa sugu wa figo (CKD).

Kabohaidreti (carbohydrates)
Kabohaidreti ndiyo chanzo cha msingi cha kalori mwilini. Kabohaidreti hupatikana kwenye ngano (mkate), nafaka, mchele, viazi, matunda na mboga, sukari, asali, keki, perimende na vinywaji . Wagonjwa wa kisukari na wanene kupita kiasi wanatakiwa kujizuia kiwango cha kabohaidreti. Ni vema wakatumia kabohaidreti zisizo kobolewa kama ni lazima wale: Kwa namna yoyote ile isizidi asilimia 20% ya kabohaidreti yote.

Mafuta
Mafuta ni chanzo muhimu cha kalori kwenye mwili na hutoa kalori nyingi mara dufu kuliko kabohaidreti au protini. Mafuta hujumuisha vyakula mafuta kama mafuta ya zeituni, sunflower, mafuta ya karangank. Punguza/jihadhari na ulaji wa nyama nyekundu, siagi, samli, mafuta ya nazink. kwani mafuta yenye kolesterol yanaweza kusababisha ugonjwa wa moyo na uharibifu wa figo.

Unywaji wa maji

3. Unywaji wa maji

Ni kwa nini wagonjwa wa CKD wachukue tahadhari ya unywaji wa maji?

Figo huwa na wajibu kwa kudumisha kiwango kamili cha maji mwilini kwa kutoa maji mengi kama mkojo. Kwa wagonjwa wa CKD, Kazi za figo zinapoharibika zaidi, kiwango cha mkojo hupungua.

Kupungua kwa mkojo husababisha kuwepo kwa maji mengi mwilini, na kusababisha kuvimba kwa uso, miguu na mikono na shinikizo la juu la damu. Kuwepo kwa maji mengi kwenye mapafu husababisha ugumu wa kupumua. Hali hii isipodhibitiwa huweza kutishia maisha.

Zipi dalili (vidokezo) vya kuwepo kwa maji mengi mwilini Maji mengi mwilini huitwa fluid overload. Kuvimba, maji tumboni (ascites), ugumu wa kupumua, na ongezeko la uzito kwa muda mfupi ndizo dalili za kuwa na maji mengi mwilini.

Ni tahadhari zipi wagonjwa wa CKD lazima wachukue ili kudhibiti unywajii wa maji?

Ili kuzuia au kutokuwa na kiasi cha maji ya kutosha mwilini, lazima maji yanywewe kulingana na mapendekezo ya daktari. Kiasi cha maji hulingana na mahitaji ya kila mgonjwa wa CKD na hupatiwa kulingana na utoaji wa mkojo na hali ya maji ya kila mgonjwa.

Ni kiwango kipi mgonjwa wa CKD anashauriwa kunywa?

  • Kwa wagonjwa ambao hawana uvimbe na wenye utoaji mkojo wa kutosha, kutodhibiti kiwango cha unywaji wa maji kunaruhusiwa, lakini dhana kwamba wagonjwa wa CKD wanafaa kunywa kiwango cha juu cha maji kulinda figo, hii si kweli.

  • Wagonjwa wenye uvimbe na upungufu wa utoaji wa mkojo wanaelekezwa kudhibiti unywaji maji. Ili kupunguza kuvimba, kwa saa 24, maji yanayoruhusiwa yafaa kuwa chini ya kiwango cha mkojo wa siku moja.
  • Ili kuzuia wingi au upungufu, kiwango cha maji kinachoruhusiwa kwa siku ni sawa na kiwango cha mkojo wa siku iliyotangulia kikijumuishwa na mililita 500. Ongezeko la mililita 500 ya maji hufidia maji yaliyopotezwa kupitia jasho na kupumua/ punzi.

Kwa nini wagonjwa wa CKD hujipima kila siku na kudumisha rekodi?
Ili kusimamia kiwango cha maji kwenye mwili na kugundua mapema ongezeko au upungufu wa maji, wagonjwa wanafaa kujipima kila siku na kuweka rekodi. Uzito wa mwili hubaki kuwa sawa iwapo masharti ya unywaji wa maji yanazingatiwa. Ongezeko la ghafla la uzito unatokana na kuongezeka kwa unywaji wa maji mengi. Kama kuna ongezeko la ghafla la uzito mgonjwa aonywe kuhusu kudhibiti kiwango cha unywaji wa maji. Upungufu wa uzito hutokana na kudhibiti unywaji wa maji na ni matokeo mazuri ya dawa zinazoleta kukojoa.

Vidokezo muhimu vya kupunguza unywaji wa maji
Kudhibiti unywaji wa maji ni mgumu, lakini vidokezo hivi vitakusaidia.

  1. Jipime kwa wakati maalum kila siku na kunywa maji ipasavyo.
  2. Daktari atakushauri kuhusu kiwango cha matumizi/unywaji wa maji kinachoruhusiwa kwa siku moja. Pima na unywe kiwango kifaacho kila siku. Kumbuka fluidi (ugiligili) haihusu maji tu bali pia inajumuisha chai, kahawa, maziwa, maziwa ya mgando (mtindi), maji ya matunda, barafu, vinywaji baridi, supu…. n.k. Ukipima unywaji wa maji inafaa pia kupima maji yaliyomo kwenye chakula. Kumbuka pia kwamba vyakula vifuatavyo vina viwango vya juu vya maji kama tikiti maji, zabbibu, saladi, nyanya, mchuzin.k.

  1. Punguza chumvi ,vyakula vyenye viungo vingi vya kukaangwa kwenye lishe kwani vinaongeza kiu , na kusababisha unywaji mwingi wa maji.
  2. Kunywa tu ukiwa na kiu. Isiwe tabia eti kwa sababu kila mtu anakunywa, basi na wewe lazima unywe.
  3. Ukiwa na kiu, kunywa kiwango kidogo cha maji au barafu. Mumunya barafu kidogo. Barafu hukaa sana kwenye kinywa kuliko kitu chochote cha maji maji, kwa hiyo inaridhisha zaidi kuliko kiwango sawa cha maji. Usisahau kuweka barafu iliyoliwa katika kipimo cha maji.
  4. Kuchunga ukaukaji wa kinywa, unaweza kusukutua na maji bila kuyanywa. Kukauka kwa kinywa kunaweza kupunguzwa kwa kumung’unya vitu mbali mbali na kusukutua.
  5. Kila mara tumia kikombe kidogo au gilasi kwa vinywaji vyako ili kupunguza kiwango cha maji.
  6. Meza dawa baada ya kula ukinywa maji. Hii itapunguza unywaji wa maji mengi zaidi wakati wa kunywa dawa.
  7. Mgonjwa lazima ajishughulishe na kazi. Mgonjwa asiye na la kufanya huwa na tamaa ya kunywa maji kila mara.
  8. Kiwango cha juu cha sukari kwa wagonjwa wa kisukari huongeza kiu. Kwa hiyo kudhibiti kiwango cha sukari ni muhimu ili kupunguza kiu.
  9. Hali ya joto (hewa) huongeza kiu. Ni bora kujaribu kuishi kwenye baridi ili kupunguza kiu(kama inawezekana).

Ni vipi unapima na kunywa kiwango kami li cha maji kinachoshauriwa kila siku?

  • Kila siku jaza kwenye chombo kiasi cha maji kilichoshauriwa na daktari.
  • Usisahau kuwa hakuna zaidi ya kiwango hicho kitaruhusiwa kwa siku hiyo.
  • Kila mara mtu akinywa, kiwango kinachojazwa kwenye kikombe au gilasi inafaa kiasi hicho kiangaliwe kwa makini. Tia kiwango sawa na hicho kwenye gilasi au kikombe kutoka kwenye chombo kilichojazwa asubuhi, kisha ukamwage.
  • Kama chombo kilichojazwa maji hakikubaki na maji yoyote, basi mgonjwa afahamu kuwa ametimiza kiwango kifaacho na hakuna haja ya kuongeza.
  • Mbinu hii ya udhibiti inafaa na inaweza kurudiwa kila siku.
  • Kwa mbinu hii rahisi kiwango kinachoshauriwa cha maji kinaweza kutolewa na kudhibitiwa na mgonjwa.

Kudhibiti chumvi (sodium) kwenye lishe

4. Kudhibiti chumvi (sodium) kwenye lishe

Kwa nini wagonjwa wa CKD hushauriwa kupata lishe yenye kiwango cha chini cha chumvi?
Chumvi kwenye chakula ni muhimu kwa kuwezesha mwili kudumisha kiwango cha damu na kudhibiti shinikizo la damu. Figo hudhibiti ukadiriaji wa sodiamu kwa wagonjwa wa CKD. Kwa wagonjwa wa CKD, figo haziwezi kutoa sodiamu na maji ya ziada kutoka mwilini. Kwa hiyo sodiamu na maji hubaki mwilini .

Ongezeko la sodiamu mwilini husababisha ongezeko la kiu, kuvimba, ugumu wa kupumua, na shinikizo la damu. Ili kupunguza shida hizi, wagonjwa wa CKD lazima wapunguze ulaji wa chumvi (sodiamu).

Je, ni tofauti gani baina ya sodiamu na chumvi?
Maneno haya hutumiwa kila mara kama maneno yenye maana moja..Chumvi tuitumiayo kwenye chakula ni sodium chloride ambayo ina asilimia arobaini (40%) sodiamu. Chumvi ndiyo chanzo kikubwa cha sodiam kwenye chakula chetu. Lakini chumvi si chanzo pekee cha sodiamu, vipo virutubisho vingine vyenye sodiamu kwenye vyakula vyetu kama:

  • Sodiamu alginate- Hutumiwa kwa aiskrimu na maziwa ya chocoleti.
  • Sodiamu bicarbonate- Hutumiwa kama hamira na soda.
  • Sodiamu benzoate – Hutumiwa kuhifadhi sosi (sauce).
  • Sodium citrate – Hutumiwa kuleta ladha kwenye jelatini, kitindamlo na vinywaji.
  • Sodiamu nitrate - Hutumiwa kuhifadhi na kuipa rangi nyama ya viwanda.
  • Sodiamu saccharide – Hutumiwa kuongeza utamu (Hutumiwa kama sukari).
  • Sodiam sulfite - Hutumiwa kuzuia kupoteza rangi kwa matunda yaliyokauka.
Vitu hivi vyote vilivyotajwa vina sodiamu lakini havina ladha ya chumvi.Sodiamu imejificha katika kila mchanganyiko uliotajwa hapo juu.

Ni kiwango kipi cha chumvi mtu anafaa kula?
Kiwango cha kawaida cha ulaji wa chumvi kwa Wahindi wengi ni takriban gramu 6-8 kwa siku.

Wagonjwa wa CKD wanatakiwa kufuata maagizo ya daktari. Wale wenye kuvimba na shinikizo la juu la damu wanashauriwa kula kama gramu tatu ya chumvi kila siku.

Vyakula vipi vinabeba viwango vya juu vya sodiamu?
Vyakula vyenye sodium nyingi ni :

  1. Chumvi ya kawaida, hamira.
  2. Vyakula vya kuokwa kama biskuti, keki, pizza,na mikate.
  3. Vyakula vya kubeba, hamira au poda ya kupika k.m vyakula vya kihindi kama vile ganthiyos, pakodar,, dhoklas, handwa, sambusa, ragdapettis, dahi vadas n.k.

  1. Achana na njugu iliyo na chumvi, matunda yaliyo kaushwa na chumvi n.k.
  2. Vyakula vya haraka/papo hapo kama vile noodles, spaghetti, macaroni, paste, cornflakes.
  3. Vyakula vilivyotengenezwa tayari k.m siagi yenye chumvi.
  4. Mboga kama kabeji, cauliflower, spinach, fenugreek, radish, beetroot, coriander n.k.
  5. Lassi yenye chumvi, soda ya masala na maji ya nazi/madafu.
  6. Tembe kama za sodium bicarbonate, antacid, laxative n.k.
  7. Vyakula visivyo vya mboga kama nyama, kuku, viungo vya mwili kama vile figo,ini na ubongo.
  8. Vyakula vya bahari kama vile kaa, lobster, oyster na shrimp na samaki wenye mafuta kama columbi kurang, kekda, bangada n.k na samaki waliokaushwa.

Vidokezo vya kupunguza sodiamu kwenye chakula

  1. Jizuie matumizi ya chumvi kwenye chakula. Pika chakula bila chumvi na uongeze kiwango kinachoshauriwa. Hii ndio njia sahihi ya kupunguza ulaji wa chumvi kwa lishe ya kila siku.
  2. Jizuie vyakula vyenye viwango vya juu vya sodiamu (kama vilivyotajwa hapo juu).
  3. Usilete chumvi au viungo vyenye chumvi mezani na ondoa mkebe wa chumvi kutoka meza ya kula. Usiongeze chumvi kwenye vyakula kama maziwa ya siagi,wali, chapati, bhakhary, parathas n.k.
  4. Soma kwa uangalifu vibandiko kwenye vifurushi vya vyakula vya kuuzwa. Tazama pia virutubisho vingine ambavyo havina au vina kiasi kidogo cha sodiamu.
  5. Tazama kiwango cha sodiamu kwenye dawa.
  6. Chemsha mboga zenye viwango vya juu vya sodiamu. Mwaga maji ya kwanza upunguze chumvi.
  7. Ili kuongeza ladha kwenye vyakula vya chumvi, kidogo ongeza kitunguu,tangawizi, ndimu, amchur,bay leaf,tamarind pulp, siki, mdalasini(cinnamon),curdamon, saffron, nutmey n.k.
  8. Tahadhari Jizuie matumizi ya vibadala vya chumvi, kwani mara nyingi vinabeba kiwango cha juu cha potasiam,ambayo inaweza kuongeza kiwango chake kwenye damu na ni hatari kwa wagonjwa wa CKD.
  9. Usinywe maji yaliyolainishwa, kwa sababu kwa kulainisha, sodium huchukua nafasi ya kalisi.
  10. Ukila kwenye mikahawa, chagua vyakula vyenye viwango vya chini vya sodiamu.

Kudhibiti potasi kwenye lishe

5. Kudhibiti potasi kwenye lishe

Kwa nini wagonjwa wa CKD wanashauriwa kudhibiti potasi kwenye lishe?
Potasi ni madini muhimu mwilini. Huwezesha utendaji kazi bora wa misuli na mishipa ya fahamu na kuweka mapigo ya moyo kuwa kawaida.

Kwa kawaida kiwango cha potasi mwilini husawazishwa kwa kula vyakula vyenye potasi na kutoa potasi nyingi kwenye mkojo. Utoaji huu hunaweza kuwa hautoshi kwa wagonjwa wa CKD na inaweza kusababisha potasi nyingi kuwa kwenye damu. (Hali ijulikanayo kama hyperkalemia). Kati ya aina mbili ya dayalisisi, hatari ya hyperkalemia ni chini kwa dayalisisi ya peritonia kuliko ilivyo kwenye himo - dayalisisi. Kiwango cha juu cha potasi chaweza kusababisha udhaifu wa misuli na mapigo ya moyo yasio ya kawaida, ambao huweza kuwa hatari. Kiwango cha potasi kikiwa juu sana, mapigo ya moyo yanaweza kusimama na kusababisha kifo cha ghafla.

Ili kuzuia athari za viwango vya potasi wagonjwa wa CKD wanashauriwa kudhibiti potasi kwenye lishe.

Ni kiwango kipi cha kawaida cha potasi kwenye damu? Ni kipi kipo juu?

  • Viwango vya kawaida potasi kwenye damu ni 3.5m Eq/l hadi 5.0M Eq/l.
  • Iwapo kiwango hiki kimefika 5.0 hadi 6.0m Eq/l kinahitaji kurekebishwa kwenye lishe.
  • Iwapo kiwango hiki ni zaidi ya 6.0m Eq/l, ni hatari na kinahitaji kuingiliwa upesi kupunguzwa.
  • Iwapo kiwango hiki ni zaidi ya 7.0 mEq/l kinatishia maisha na kinahitaji matibabu ya dharura.

Uainishaji wa vyakula kulingana na viwango vya potasi
Ili kudumisha udhibiti bora wa potasi kwenye damu, ulaji wa vyakula lazima urekebishwe kulingana na ushauri wa daktari. Kulingana na virutubisho vya potasi, vyakula vimegawika katika makundi matatu tofauti( vyakula vinavyobeba potasi kwa wingi ,wastani na chini).

Potasi ya juu /nyingi (juu) – Zaidi ya 200mg/100gms ya chakula
Potasi ya wastani – 100 hadi 200mg /100gms ya chakula
Potasi ya chini _ Chini ya 100mg /100gms ya chakula

Vyakula vyenye viwango vya juu vya potasi

  • Matunda : Amla, apricot, chiken tufaha, embe bivu, forsadi, mapera, machungwa, mapapai, ndizi mbivu, nazi, tunda la kiwi, komamanga, tikitiki maski, plum na sapota.
  • Mboga : Amararith, brinjals, brocooli colocasia, coriander, cumia, kabeji, maharagwe, nyanya, uyoga, papaya kijani, pumpkin, viazi, viazi vitamu, mchicha na viazi vikuu.
  • Matunda makavu: Korosho, lozi, tende, tini kavu na raisini.
  • Nafaka: Bajra, ragi na unga wa ngano.
  • Pulses: Gramdal nyeusi, Bengal gram dal, whole Bengal, chanadal, gramdal kibichi,lentil dal,masoor dal,ndengu nyekundu tur dal.
  • Masala: Mbegu za kumini, mbegu za coriander, pilipili nyekundu iliyokaushwa na mbegu za fenugreek.
  • Vyakula visivyo vya mboga mboga: Samaki kama anchary, mackerel, rohe, pomfret nyeupe, prawas, lobster, na nyama ya ngombe.
  • Vinywaji: Bounvita, maji ya nazi, maziwa yaliyoganda, chokoleti, maji ya matunda, rasam, supu, tembo, nyati maziwa, maziwa ya ng'ombe, divai na vinywaji vingine yenye hewa.
  • Vinginevyo: Chokoleti, kadbari, keki ya chokoleti, aiskrimu ya chokoleti, chumvi ya lona, viambata vya viazi, na mchuzi wa nyanya.

Vyakula vyenye viwango wastani vya potasi

  • Matunda: Lichee, ndimu tamu, mbivu cherry, pear, zabibu na tikiti maji.
  • Mboga mboga: Mzili wa biti, ndizi mbichi, buyu chungu, kabeji, karoti, cauliflower, maharagwe ya kifaransa, bamia (okra), mbichi maembe, mbaazi za kijani, kitunguu, boga, nafaka tamu, majani ya sunflower na.
  • Nafaka: Unga wa kawaida, maida, jowar, tambi za unga ngano, fleki za mchele, na ngano vemiseli.
  • Vyakula visivyo vya mboga: Cital, hisla, katla, magup, ini.
  • Vinywaji: Maziwa ya ng’ombe.

Vyakula vyenye viwango vya chini vya potasi

  • Matunda : Tufahaa, zababu, lemon, tunda la jambu, nanasi.
  • Mboga mboga: Buyu la chupa (dudhi), maharagwe pana (papdi) kapsikam, akra ya kichina (turayi), kokiumba, majani ya fenugreek, lectuce, methi, parvar, tinda.

  • Nafaka:Wali, rava na ngano ya semolina.
  • Pulses:Kunde ya kijani.
  • Vyakula visivyo na mboga mboga: Nyama ya ngo’mbe, kondoo nguruwe, kuku na mayai.
  • Vinywaji: Coca-cola, kahawa, fanta, lemonade, maji ya ndimu, Limka na soda.
  • Vinginevyo: TTangawizi iliyokaushwa, asali majani ya minti haradali, pilipili, karafuu, kungumanga na siki.

Pata ushauri wa daktari wako kuhusu vyakula vilivyopo sehemu yako

Vidokezo vya kupunguza potasi kwenye damu

  1. Kula tunda moja kila siku, hasa lenye kiwango cha chini cha potasi.
  2. Kunywa kikombe kimoja cha chai au kahawa kila siku.
  3. Mboga zenye potasi zinafaa kuliwa baada ya kupunguza kiwango cha potasi.
  4. Epuka maji ya nazi/madafu, maji ya matunda na vyakula vyenye kiwango cha juu cha potasi (vilivyo orodheshwa hapo juu).
  5. Karibu vyakula vyote vina potasi kwa hiyo chagua vyenye kiwango cha chini, ikiwezekana.
  6. Udhibiti wa potasi ni muhimu sio tu kwa wagonjwa wa ugonjwa sugu wa figo (CKD) lakini ni muhimu hata baada ya kuanza dayalisisi.

Namna ya kupunguza kiwango cha potasi kwenye mboga?

  • Menya, kata vipande vidogo na uweke mboga kwenye chungu kikubwa cha maji.
  • Osha vipande hivyo na maji moto kiasi.
  • Jaza chungu na maji moto (kiasi cha maji kiwe mara nne hadi tano ya kiwango cha mboga.) na loweka kwa walao saa moja.
  • Baada ya kuloweka kwa saa 2-3 suuza mara tatu na maji yenye moto kadiri.
  • Chemsha mboga kwenye maji zaidi baada ya kumwaga maji ya kwanza na pika jinsi upendavyo.
  • Kwa njia hii unaweza kupunguza kiwango cha potasi kwenye mboga lakini si kabisa. Kwa hiyo ni bora kujiepusha na mboga zenye potasi nyingi au kula kwa kiasi kidogo.
  • Kwa kuwa vitamin hupotezwa wakati wa kuchemsha mboga Unaweza kunywa vitamin kadri utakavyoshauriwa na daktari.

Vidokezo maalum vya kuchuja potasi kutoka kwenye viazi

  • Kuchonga au kukata viazi vipande vidogo vidogo ni muhimu.
  • Hali ya joto la maji yanayotumiwa ama kuloweka au kuchemsha viazi huleta tofauti.
  • Matumizi ya maji mengi ya kuloweka au kuchemsha viazi ni muhimu na inasaidia.

Kudhibiti fosfera kwenye lishe

7. Kudhibiti fosfera kwenye lishe

Kwa nini wagonjwa wa CKD wale lishe yenye kiwango cha chini cha fosfera?

  • Fosfera ni madini muhimu ya kuweka mifupa imara na yenye afya. Fosfera ya ziada kwenye chakula hutolewa kwenye mkojo na hivyo kiwango cha fosfera kwenye damu kinadumishwa.
  • Kiwango cha kawaida cha fosfera kwenye damu ni 4.0 hadi 5.5 mg/dl.
  • Kwa wagonjwa wa CKD fosfera zaidi inayoliwa kwenye chakula haitolewi kwenye mkojo, kwa hiyo kiwango cha fosfera kwenye damu huongezeka. Ongezeko hili la fosfera huondoa kalisi kutoka kwenye mifupa na kuifanya kuwa dhaifu.
  • Ongezeko la fosfera huweza kusababisha matatizo mengi kama vile kuwashwa, udhaifu wa misuli na mifupa, maumivu ya mifupa, maumivu kwenye mifupa na maumivu ya viungo. Kukakamaa kwa mifupa husababisha urahisi wa kuvunjika kwa mifupa.

Ulaji wa vyakula vipi vyenye viwango vya juu vya fosfera unafaa kupunguzwa na kukomeshwa?

Vyakula vyenye viwango vya juu vya fosfera ni :

  • Maziwa na mazao yake: Siagi.cheese, chokoleti, maziwa yaliyoganda, aiskrimu, sharubati (milk shake), paneer.
  • Matunda makavu: korosho, almonds, pistachios, nazi kavu, Walnut.
  • Vinywaji baridi : Dark colas, fanta, mazza, frooti n.k.
  • Karoti, majani ya kalakasi, mahindi, njugu, viazi vitamu.
  • Protini ya wanyama: Nyama, kuku, samaki na mayai.

Ulaji wa juu wa vitamin na nyuzi

8. Ulaji wa juu wa vitamin na nyuzi (vitamin na fiber intake)

Wagonjwa wa CKD huugua kutokana na ulaji usio tosha wa vitamin kabla ya wakati wa dayalisisi, kwa sababu ya upungufu wa ulaji wa chakula, mbinu maalumu ya upishi ya kuondoa potasi nyingi na ukosefu wa hamu ya kula. Baadhi ya vitamin hasa vitamin B na C inayoyeyuka kwa maji, folic acid n.k hupotea wakati wa dayalisisi. Ulaji wa nyuzi ni muhimu kwa CKD. Kwa hiyo wagonjwa wanashauriwa kula mboga mboga nyingi na matunda yenye vitamin na chakula chenye nyuzi nyuzi.

Kielelezo cha vyakula vya kila siku

Kanuni za kawaida za mpangilio wa lishe ni:

1. Unywaji wa maji na chakula rojorojo : Unywaji wa maji na udhibiti wake unafaa ufuatwe na ushauri wa daktari. Upimaji wa uzito wa kila siku ni vema ufuatwe pia. Ongezeko lolote la ajabu la uzito huashiria ongezeko la unywaji wa maji.

2. Kabohaidreti : Ili kuhakikisha kuwa mwili unapata kaloria zakutosha pamoja na nafaka, mgonjwa anastahili kula vyakula vya sukari na glucose, vinavyotolewa, mradi yeye mgonjwa hasiwe na kisukari.

3. Protini: Maziwa, nafaka, mayai, kuku ndio asili kuu ya protini. Wagonjwa wa CKD ambao bado hawako katika dayalisisi wanashauriwa kupunguza protini kwenye lishe. Wanashauriwa kula grammu 0.8 kwa kila gramu ya uzito wa mwili, kwa siku. Dayalisisi ikianzishwa, mgonjwa huhitaji kiwango cha juu cha protini kwenye mlo, hasa wagonjwa walio kwenye peritoneum – dayalisisi. Jihadhari sana kula protini ya wanyama kama nyama yenyewe, kuku na samaki ambazo zina protini nyingi, potasi na fosfera. Zote hizi zaweza kuwa hatari kwa wagonjwa wa CKD.

4. Mafuta: Kiwango cha mafuta kwenye mlo kinafaa kupunguzwa lakini kukatisha kabisa kwa siagi, samli… n.k. kwenye mlo kunaweza kuwa hatari. Kwa jumla, mafuta ya soya, njugu ni muhimu kwa mwili kuvila Lakini muhimu zaidi ni kula vyakula kwa kiwango vinavyokadiriwa na kushauriwa na daktari wako.

5. Chumvi: Wagonjwa wengi wanashauriwa kula kiwango cha chini cha chumvi.Usiongeze chumvi mezani. Usile chakula kilichopikiwa magadi (na poda ya kula), dhibiti au acha kutumia chumvi mbadala, ina potasi nyingi.

6. Nafaka: Mchele na mazao yake kama, kurmura huweza kuliwa. Ili kuepuka na aina moja tu ya chakula, unaweza kula ngano, wali, poha, saga, semolina, cornflakes* kwa mzunguko. Shayiri, bajra na mahindi yanaweza kuliwa lakini kwa kiwango cha chini.

7. Pulses : Dali mbalimbali inafaa kuliwa kwa mzunguko ufaao ili kuleta mabadiliko kwa ladha na yanaweza kufanya chakula kiliwe na mgonjwa. Ni vyema kufanya dali kuwa nzito kuliko kuwa na maji mengi. Kiwango cha dali kinafaa kiliwe kulingana na ushauri wa daktari.

8. Ili kupunguza potasi kwenye dali ni vyema baada ya kuosha, inafaa kulowekwa kwenye maji moto kisha kumwaga maji hayo. Endelea kuichemsha na maji huku ukimwaga maji hayo baada ya kuchemsha. Pia badala ya dali na mchele mtu anaweza kula khichadi au dosa.

9. Mboga: Mboga zenye kiwango cha chini cha potasi zinaweza kuliwa kama mgonjwa anavyotaka. lakini zenye kiwango cha juu zinaweza kutengenezwa kuondoa potasi kuliko kuliwa kabla. Kuongeza ladha, maji ya limau huweza kuongezwa.

10. Matunda: Matunda yenye viwango vya chini vya potasi kama vile tufaha, papaya, zabibu huweza kuliwa mara moja kwa siku. Siku ya dayalisisi, mgonjwa anaweza kula tunda lolote moja. Maji ya matunda na nazi yasitumiwe.

11. Maziwa na mazao yake: 300-350ml ya maziwa au mazao yake kama kheer, aiskrimu, curd, maththa huweza kunywewa. Dhibiti kiwango cha mazao hayo ili uzuie maji mengi mwilini.

12. Vinywaji baridi: Usinywe Pepsi, fanta, frooti lazima zisitumiwe. Usinywe maji ya matunda na maji ya nazi/madafu.

13. Matunda makavu: Matunda makavu, njugu, karanga, mbegu za ufuta (sesame), nazi bichi au kavu lazima iepukwe.