Heri kukinga kukiko kutibu ni ukweli katika matibabu ya magonjwa ya figo. Magonjwa kama ugonjwa sugu wa figo (CKD) hautibiki na gharama ya matibabu ya ugonjwa wa figo hatua ya mwisho (ESKD) ni ghali mno. Mtu ambaye ana ugonjwa unaoogofya kama huo anaweza asionyeshe dalili mbaya za ugonjwa huu. Iwapo utambuzi wa ugonjwa wa figo unafanywa mapema, unaweza kutibiwa kwa urahisi kwa dawa. Kwa hivyo kama unahisi una shida ya figo, inashauriwa uende kufanyiwa uchunguzi na utambuzi haraka na mapema.
Ni nani anafaa kupata uchunguzi wafigo zao?
Ni nani yuko katika hatari kubwa ya kupata shida ya figo?
Mtu yeyote anaweza kupata shida ya figo, lakini hatari ni zaidi iwapo:
- Mtu aliye na dalili za ugonjwa wa figo.
- Mtu aliye na ugonjwa wa kisukari.
- Mtu aliye na msukumo wa damu usio dhibitika.(shinikizo la damu).
- Historia ya kifamilia ya ugonjwa wa figo, Kisukari na msukumo wa damu.(Shinikizo la damu).
- Mtu ambaye ni mvutaji tumbaku, mnene kupita kiasi na/au mwenye umri unaozidi miaka 60.
- Mtu aliyetumia matibabu ya muda mrefu ya vitulizo vya maumivu.
- Historia ya kuzaliwa nayo hitilafu ya mfumo wa mishipa ya mkojo.
- Uchunguzi kwa watu hawa ambao wana hatari kubwa, husaidia katika utambuzi mapema wa ugonjwa wa figo.
Namna ya kutambua shida za figo? Ni Vipimo vipi hufanywa?
Kutambua shida za figo tofauti tofauti daktari huchukua historia kamili, humchunguza muathirika kikamilifu, hupima presha ya damu kisha humshauri kuhusu upimaji unaofaa. Vipimo vinavyofanywa mara kwa mara ni uchunguzi wa mkojo, damu, na radiologia.
Hatua za mwanzo za ugonjwa sugu wa figo huwa hazibainiki, upimaji wa kimaabara ndio njia pekee za utambuzi.
1. Upimaji wa mkojo
Upimaji tofauti wa mkojo hutoa vidokezo muhimu vya utambuzi wa magonjwa mbalimbali ya figo.
Upimaji wa kawaida wa mkojo
- Ni rahisi, wenye gharama ya chini lakini ni uchunguzi wa utambuzi wa awali muhimu sana.
- Kisicho kawaida kinachoonekana kwenye upimaji wa mkojo hutoa vidokezo muhimu vya utambuzi, hata hivyo ripoti ya kawaida ya mkojo haiondoi shida za figo.
- Kuwepo kwa protini kwenye mkojo (protinuria) huonekana katika magonjwa mbali mbali ya figo haifai kupuuzwa.Kuweko kwa protini kwenye mkojo ni dalili ya tahadhari ya kwanza, na mapema hata pekee ya ugonjwa sugu wa figo (na hata ya ugonjwa wa moyo). Kwa mfano protinuriani ni dalili ya mwanzo kabisa ya figo kuathirika katika kisukari.
- Kuwepo kwa chembe chembe za usaha kwenye mkojo kunaonyesha kuambukizwa kwa mishipa ya mkojo (UTI).
- Kuwepo kwa protini na chembe chembe nyekundu za damu hutoa vidokezo (dalili) ya ugonjwa wa uvimbe wa figo (yaani glomerulonephiritis).
Upimaji wa mkojo ni muhimu sana kwa utambuzi wa mapema wa magonjwa ya figo.
Maikroalbuminuriya
Maikroalbuminuriya inamaanisha kiwango kidogo sana cha protini kwenye mkojo. Upimaji huu hutoa kidokezo (dalili) cha kwanza na mapema cha utambuzi wa figo kuhusika na kisukari. Katika hatua hii ugonjwa huu unaweza kupona kwa matibabu.Protini (albumin) haipo katika upimaji wa kawaida wa mkojo katika hatua hii.
Upimaji mwingine wa mkojo
- Ukusanyaji wa mkojo kwa saa 24 kwa kupima albumin
Kwa mgonjwa mwenye protini kwenye mkojo, upimaji huu ni muhimu ili kubaini kiwango cha jumla cha protini kinachopotezwa kwa saa 24 Upimaji huu ni muhimu kuchunguza ukali wa ugonjwa huu (severity) na pia athari ya matibabu katika kupotezwa kwa protini.
- Upimaji wa kukuza wadudu na kuona mwelekeo wao wa kuuwawa na dawa:(culture and sensitivity test)
Upimaji huu huchukua takriban muda wa kati ya saa 48 na 72 na hutoa habari muhimu kuhusu aina ya bacteria inayosababisha maambukizi na uchunguzi wa aina ya dawa ya matibabu.
- Upimaji wa vidudu vya basili
Upimaji huu nu mihumu kwa utambuzi wa magonjwa ya kifua kikuu cha mishipa ya mkojo.
Kreatinini ya serami (serum) ni uchunguzi maalumu wa damu unaotumiwa kila mara kuchunguza na kuchanganua hitilafu ya figo.
2. Upimaji wa damu
Upimaji mbali mbali wa damu unahitajika ili kufahamu utambuzi wa magonjwa tofauti tofauti ya figo.
- Kreatini na Yurea
Viwango vya damu vya kreatini na yurea huoyesha kazi ya figo Kreatinin na yurea ni uchafu unaotolewa kutoka kwenye damu na figo. Ikiwa kazi ya figo imerudi chini,/imeathirika viwango vya damu vya kreatini na yurea hupanda zaidi ya viwango vya kawaida. Kiwango cha kawaida ya kreatini ya serami (Serum) 0..9 hadi 1.4 mg/dl na kiwango cha kawaida ya yurea ya damu ni 20 hadi 40mg/dl.. Viwango vya juu hudhihirisaha uharibifu mkubwa wa figo. Kiwango cha creatini ni mwongozo bora wa kazi ya figo kuliko kiwango cha yurea ya damu.
- Himoglobini
Figo zenye afya husaidia katika uzalishaji wa chembe chembe nyekundu za damu (RBCS) inayobeba himoglobini. Katika upimaji wa damu, iwapo himoglabini iko chini, hali hii inaitwa anemia. Anemia ni dalili muhimu ya ugonjwa sugu ya figo.
Hata hivyo, mara nyingi anemia inaweza kutokea katika maradhi mengine. Na kwa hiyo anemia si dalili maksusi ya ugonjwa wa figo.
- Upimaji mwingine wa damu
Upimaji tofauti tofauti wa damu unaofanywa kwa wagonjwa wa figoni: Sukari ya damu, Protini ya serami, holesCtral, electrolytes/(Sodiamu potasi na kloridi), Kalsiamu, fofostera, bicarbonate, ASO titer, kitimizonk..
Picha ya Ultra sound ya figo ni upimaji rahisi na salama unatumiwa kukadiria ukubwa, umbo na sehemu ambayo figo zipo.
3. Upimaji wa upigaji picha ( vipimo vya rediolojia)
- Upigaji picha ya ultrasound ya figo.
Ultrasound ni upimaji rahisi, muhimu, upesi na salama ambao hutoa maelezo muhimu kama vile ukubwa wa figo na kuwepo kwa uvimbe wa maji maji (cysts), mawe na uvimbe mwingine (tumors). Upimaji huu unaweza kugundua kuziba kwenye mtiririko wa mkojo popote kwenye figo, ureta au kibofu. Katika hitilafu sugu ya figo, figo zote mbili huwa ni ndogo kuliko kawaida .
- Eksirei ya tumbo
kwa utambuzi wa mawe kwenye mfumo wa mkojo, upimaji huu ni muhimu.
- Picha ya mishipa ya veni (Intra Venous Urography) (IVU)
Upimaji huu pia unajulikana kama (pyelografia) na ni upimaji maalumu wa eksirei. Katika upimaji huu, dawa maalumu inayoweza kuonekana kwenye picha za eksrei, inadungwa kwenye mshipa wa damu wa veni kwenye mkono. Dawa hii inayo dungwa kwenje njia ya damu inapitia figo na utoka mwilini kupitia mkojo. Kwa kutumia njia hii ya uchunguzi, mfumo wote wa mkojo unaweza kuonekana kwa eksrei, ( figo, ureta, kibofu cha mkojo). Picha hizi za eksrei huonyesha mfumo mzima wa mkojo.na kwa hiyo zinaweza kuonyesha shida ya jiwe, kizuizi chochote kinachofanya mkojo usipite (obstruction), uvimbe (tumors). Picha hizi uweza kuonyesha pia kama kuna maumbile yasiyo ya kawaida na utendaji usioridhisha wa figo (abnormalities in structure and function ).
Kama mgonjwa ana ugonjwa sugu wa figo, kipimo cha IVU HAKISHAURIWI. Hii ni kwa sababu dawa inayochomwa kwenye veni inaweza kuharibu zaidi figo ambalo halifanyi kazi vizuri. Dawa haitaweza kuondoka mwilini vizuri kwa hiyo nia ya kuona mfumo wa mkojo haitakuwa na maana. IVU isitumike pia kama mgonjwa ni mja mzito. Kama inabidi kufanya kipimo cha namna hii, basi tumia ultrasound au/na CT Scan.
Upimaji a uchunguzi muhimu sana wa magonjwa ya figo ni upimaji wa mkojo, kreatinini ya serami, na picha ya ultrasound ya figo.
- Sistoetrogramu tupu (VCUG)
Awali kipimo hiki kilijulikana kama upimaji wa . Kipimo hiki huhitajika sana kwa kuthamini maambukizi ya mfumo wa mkojo kwa watoto.
Katika kipimo hiki maalumu cha eksirei, kibofu kinajazwa na dawa maalumu kwa kutumia katheta kwa tahadhari za usafi. Baada ya kibofu kujazwa, katheta inatolewa, na mgonjwa anaombwa kukojoa wakati eksirei zinapigwa kila baada ya muda fulani. Upimaji huu ni muhimu kutambua kama kuna shida inayorudisha mkojo kwenye ureta hadi kwenye figo (ijulikanayo kama vesicoureteral reflux) na huonyesha mfumo usio wa kawaida wa kibofu cha mkojo na urethra.
- Upimaji mwingine wa rediolojia
Kwa utambuaji wa baadhi za shida za figo, upimaji maalum kama vile “ CT scan “ ya figo na mfumo mzima wa mkojo, dopla ya hitilafu ya figo, uchunguzi wa redionuklei , enjiografia ya hitilafu ya figo, antegrade na retrograde pyelografian k ni muhimu sana.
Bayopsia ya figo hufanywa na sindano jembamba wakati mgonjwa yuko macho.
4. Upimaji mwingine maalum
Bayopsia ya figo, sistoskopia na urodinamikia ni upimaji maalum /spesheli ambazo zinafaa kwa utambuzi kamili wa shida fulani fulani za figo.
Bayopsia ya figo
Bayopsia ya figo ni upimaji muhimu unaosaidia katika utambuzi wa magonjwa fulani ya figo.
Bayopsia ya figo ni nini?
Katika bayopsia ya figo, kipande kidogo cha figo hutolewa kwa sindano na kuchunguzwa kwa hadubini. Bayopsia ya figo hutekelezwa ili kutambua maumbile kamili ya magonjwa fulani ya figo.
Ni lini bayopsia ya figo inashauriwa?
Katika magonjwa fulani fulani ya figo, historia pana, uchunguzi na upimaji hauwezi kuleta utambuzi kamili. Kwa wagonjwa hao, bayopsia ya figo ndiyo inaweza kuwa upimaji wa pekee unaoweza kutoa utambuzi kamili.
Uchukuaji wa kipande kidogo cha figo ni kipimo kinachofanywa ili kuweka bayana utambuzi wa magonjwa fulani fulani ya figo.
Ni vipi bayopsia ya figo husaidia?
Bayopsia ya figo hubainisha utambuzi dhahiri wa magonjwa ya figo yasiyoelezeka /yasiyo fafanuliwa. Kwa taarifa hii, mtaalamu wa nefrolojia anaweza kupanga mkakati mwafaka wa matibabu na kuongoza wagonjwa na familia zao kuhusu ukali na aina ya ugonjwa wa figo.
Kwa mbinu zipi bayopsia ya figo hutekelezwa?
Mbinu maarufu zaidi ni bayopsia ya sindano.ambapo sindano inachomwa kupita ngozi hadi kwenye figo. Mbinu nyingine, isiyotumika sana,ni bayopsia inayohitaji upasuaji.
Je, bayopsia ya figo hutekelezwa vipi?
Mgonjwa analazwa hospitalini na kupata idhini ya mgonjwa ni muhimu..
- Kabla ya bayopsia, hakikisha msukumo wa damu/ shinikizo la damu ni wa kawaida na kwamba upimaji wa damu unaonyesha kuganda kwa damu ni kwa kawaida.
- Dawa zinazotumiwa kuzuia kuganda kwa damu, kama asprini, zinasitishwa kama wiki 1-2 kabla ya bayopsia.
- Ultrasound inafanywa ili eneo la figo lijulikane na pia kutambua sehemu kamili ya bayopsia. Sehemu ya bayopsia ni mgongoni, chini ya ubavu, sehemu ya juu ya kiuno, karibu na misuli ya nyuma/ mgongoni.
- Mgonjwa anaombwa kulala kifudi fudi, na tumbo likiegemea mto au taulo. Mgonjwa awe macho wakati wote operesheni hii inapofanyika. Kwa mtoto, bayopsia ya figo inafanywa akiwa amelazwa.
- Baada ya kusafisha ngozi sawasawa, sehemu ya bayopsia inalemazwa (local anaesthesia) kupunguza uchungu/ maumivu.
Uchukuaji wa kipande kidogo cha figo kwa kawaida hufanywa kwa kutumia sindano nyembamba wakati mgonjwa yuko macho kabisa.
- Kwa usaidizi wa sindano ya bayopsia, vipande vidogo vidogo vya nyama (2 au 3) zinatolewa kutoka kwenye figo. Vipande hivi vinatumwa kwa mtaalamu maalumu kwa ukaguzi / uchunguzi wa kihistopatholojia.
- Baada ya bayopsia, presha inawekwa kwenye sehemu ya baopsia ili kuzuia damu kuvuja. Mgonjwa anahimizwa kuwa na mapumziko ya saa 6 - 12 kisha aruhusiwe kuondoka siku inayofuatia.
- Mgonjwa anashauriwa kuepuka kazi nzito au zoezi/kazi nzito kwa takriban wiki 2- 4 baada ya bayopsia.
Je, kuna hatari zozote katika Bayopsia ya figo?
Kama hatua yoyote ya upasuji ,tatizo linaweza kutokea kwa wagonjwa wachache baada ya bayopsia ya uchunguzi. Maumivu kwa mbali na mkojo mwekundu mara moja au mbili hutokea lakini baadaye hukoma wenyewe .
Mara chache uvujaji wa damu unaendelea na upewaji wa damu huhitajika. Mara chache sana, uvujaji mwingi wa damu huendelea na utowaji wa figo kwa dharura kwa upasuaji hauwezi kuepukika.
Wakati mwingine, vijipande vya figo vilivyotolewa havitoshelezi kwa utambuzi wa kihistopatholojia. Hii hutokea kwa nadra (Kati ya 1 kwa 20) na kulazimu kurudia bayopsia.