Maelezo

Maelezo

Hitilafu kali ya figo (jeraha): Katika hali hii kuna upotevu wa ghafla wa kazi za figo. Hali hii si ya kudumu,bali ni ya muda na hurekebishika. Anemia : Ni hali ya kiafya ambayo himoglobini inapungua kwenye damu. Anemia husababisha udhaifu, uchovu na kushindwa kupumua akiwa mtu anatumia nguvu kufanya jambo fulani. Anemia ni jambo la kawaida kwenye CKD na hutokea kutokana na utoaji hafifu wa erithroprotini na figo.

Dayalisisi ya peritonia ya kujiendesha (APD): Tazama CCPD.
Fistula ya ateri na veni ( AV fistula ):
Inamaanisha kuunganishwa kwa ateri na veni kwa upasuaji, hasa kwenye mkono. Kwa kutumia fistula hii, damu nyingi yenye presha nyingi huingia kwenye veni na kusababisha upanuzi wa veni. Veni hii basi huruhusu kwa urahisi, uingizaji wa sindano kama inavyotakiwa kwa himodayalisisi. Fistula hii ndiyo maarufu sana na mbinu bora ya upatikanaji wa mishipa ya damu kwa kipindi kirefu cha himodayalisisi.

Figo bandia: Tazama dayalaiza.

Tezi dume kupanuka: Hii ni hali ya kawaida kwa tezi dume kupanuka kadri mwanaume anavyozeeka. Kupanuka kwa tezi dume si saratani, bali ongezeko hili hubana mshipa wa kukojolea na mkojo usipite.

Msukomo wa damu/ Shinikizo la damu: Ni nguvu inayosukuma damu inayotiririrka kwenye mishipa ya damu, moyo ukisukuma damu. Msukumo wa damu ni mojawapo ya ishara kuu muhimu ya kuishi na upimaji wake hujumuisha nambari mbili. Ya kwanza huashiria msukumo wa juu (sistoliki) ambayo hupima presha /msukumo wa juu zaidi inayoshuhudiwa wakati moyo ukifupika (contract).

Nambari ya pili ni presha (msukumo) wakati moyo umepumzika.(diastoli) Namba hizi mbili huamua kama mgonjwa ana shinikizo la damu au la.

Kifo cha ubongo : “ Kifo cha ubongo “ ni uharibifu mkali na wa kudumu wa ubongo ambayo hautakuwa na nafuu kwa matibabu yoyote ya dawa au upasuaji . Kwa kifo cha ubongo, upumuaji na mzunguko wa damu mwilini hudumishwa kwa mashine.

Kubadilishwa figo wa kadaveriki: Tazama ubadilishaji wa figo za mfu.

Kalisi (calcium) : Ni madini ipatikanayo mwilini kwa wingi mno. Ni muhimu kwa ustawishaji na udumishaji wa meno na mifupa kuwa yenye nguvu . Kalisi hupatikana kwenye maziwa na mazao yake.

Katheta ya himodayalisisi: Ni mrija mrefu, mwororo na ulio na uwazi wa lumeni mbili. Damu huondolewa kutoka kwenye lumeni moja, inaingia kwenye mkondo wa dayalisisi ili kusafishwa, na kurudishwa mwilini kupitia lumeni nyingine. Uingizaji wa katheta yenye lumeni mbili ndiyo mbinu ya kawaida na bora ya himodayalisisi ya dharura na ya muda.

Dayalisisi Ya Wakati Wote (CAPD): CAPD ni aina ya dayalisisi inayoweza kufanywa nyumbani bila matumizi ya mashine/mtambo. Katika dayalisisi ya aina hii maji hubadilishwa kwa vipindi maalumu wakati wote yaani saa 24 kwa siku, siku saba kwa wiki.

Dayalisisi inayojiendesha (CCPD, au Dayalisisi ya peritonia ya kujiendesha (APD) ni aina ya Dayalisisi inayofanywa nyumbani kila siku na mashine unayojizungusha . Katika CCPD, mashine hubadilisha maji wakati mgonjwa analala usiku. Mashine hujaza na kuondoa myeyusho wa dayalisisi kutoka tumboni.

Kreatinini na yurea: Huu ni uchafu unaotokana na protini zinazotolewa na figo. Kiwango cha kawaida cha kreatinini ya serami ni 0.8 hadi 1.4 mg% na ile ya yurea ni 2 hadi 4 mg %. Katika hitilafu ya figo, kiwango cha yurea na kreatinini kwenye damu huongezeka.

Ugonjwa sugu wa figo (CKD ) : Muendelezo wa polepole usiojirejesha wa upotevu wa kazi ya figo kwa miezi hadi miaka huitwa CKD . Katika

ugonjwa huu usiotibika, kazi za figo zinapungua polepole na baada ya muda kazi za figo husimama kabisa. Hatua hii ya mwisho huitwa hatua ya mwisho ya ugonjwa wa figo (End Stage Kidney Disease – ESKD).

Sistoskopi: Ni kipimo cha utambuzi ambapo daktari hutazama ndani ya kipofu na urethra kwa kutumia kifaa chembamba, chenye mwanga na chepesi kiitwacho sistoskopi.

Ubadilishaji wa figo ya mfu : Ni upasuaji ambao figo yenye afya iliyotolewa kutoka kwa mtu mwenye kifo cha ubongo, inabadilishwa kwa mgonjwa wa CKD (ugonjwa sugu wa figo).

Ugonjwa wa figo wa kisukari (nefopathi) : Kisukari cha muda mrefu husababisha uharibifu wa mishiba midogo ya damu ya figo. Uharibifu huu husababisha upotevu wa protini kwenye mkojo. Baadae husababisha shinikizo la juu la damu, kuvimba, kisha uharibifu wa polepole wa figo, Hatimaye, hali hii ikiendelea husababisha hitilafu hatari ya figo yaani ESKD.

Ugonjwa wa figo wa kisukari ndio maarufu sana kusababisha ugonjwa sugu wa figo, unaoleta asilimia 40-45% ya wagonjwa wapya wa CKD. Dayalisisi: Ni njia bandia ya kuchuja damu na kutoa uchafu na maji mengi ya ziada kutoka mwilini wakati wa himodayalisisi.

Dialyzer: Ni figo bandia ambalo huchuja damu ili kuondoa uchafu na maji ya ziada kutoka mwilini wakati wa himodayalisisi.

Dawa za kusaidia kukojoa (diuretics) : Dawa hizi huongeza uzalishaji wa mkojo pia utoaji wa maji huongezeka kama mkojo na hivyo kupunguza maji mwilini. Dawa hizi ujulikana pia kama “water pills”.

Uzito mkavu: Ni uzito wa mtu baada ya maji yote ya ziada yametolewa kwa kutumia dayalisisi.

Wakati wa kukaa: Wakati wa dayalisisi ya peritonia, kipindi ambapo maji ya PD hubaki kwenye tumbo huitwa wakati wa kukaa. (dwell time). Wakati huu, hatua za usafishaji hufanyika.

eGFR(estimated Glomerular Filtration Rate) : Ni nambari inayopatikana kutokana na hesabu ya kiwango cha kreatinini ya damu na taarifa nyingine . eGFR hupima jinsi figo zinavyofanya kazi vyema na thamani/kiwango cha kawaida ni 90 au zaidi. Upimaji wa e GFR ni muhimu kwa utambuzi, kuweka katika madaraja na hatua za uchunguzi wa maendelezo ya CKD.

Elektrolaiti : Kuna madini mengi kama vile sodiamu,potasi,kalisi kwenye mkondo wa damu ambayo hudhibiti kazi muhimu za mwili. Hizi kemikali zinaitwa elektrolaiti. Figo huweka kiwango cha elektrolaiti kwa kiwango kimoja kwenye damu, wagonjwa wa magonjwa ya figo, figo hupimwa kujua viwango vya elektrolaiti ili kuona ufanisi wa utendaji kazi wa figo.

Hatua ya mwisho ya ugonjwa wa figo (ESKD): Hii ni hatua ya mwisho ya ugonjwa wa figo. Katika hatua hii ya CKD, kuna hitilafu kubwa katika figo. Wagonjwa wanahitaji matibabu kama dayalisisi au kubadilisha figo ili waweze kuishi maisha ya kawaida.

Erithropoitini ( EPO ) : Hii ni homoni inayotolewa na figo ili kuwezesha ukuaji wa chembe chembe nyekundu za damu kwenye uboho wa mfupa (bonemarrow)* Iwapo figo zimeharibika, haziwezi kutoa erithropoitini ya kutosha na kusababisha upungufu wa ukuaji wa chembe chembe nyekundu za damu, inayosababisha anemia.

Ubadilishanaji: Inamaanisha hatua moja ya mzunguko wa dayalisisi ya peritonia inayojumuisha hatua tatu. Hatua ya kwanza ni mtiririko wa maji ya dayalisisi kwenye tumbo. Hatua ya pili, maji huwa kwenye tumbo kwa saa nyingi ili kuruhusu maji mengi ya ziada na sumu kutoka kwenye damu hadi kwenye maji ya dayalisisi. Hatua ya tatu ni kuyatoa yale maji ya dayalisisi kutoka tumboni.

Kuyavunja mawe kwa mashine (ESWL): Hii ni njia ambayo mawimbi maalumu yanayotengenezwa na mashine (Lithotriptor machine) yana uwezo wa kuyavunja vunja mawe katika vipande vidogo vidogo ili kuyawezesha kupita kwenye mfumo wa mkojo. ESWL ni njia bora ya matibabu ambayo inatumika sana sasa kwa matibabu ya mawe kwenye figo.

Nasuri : Anglia – Nasuri ya Arterio – venous (nasuri ya AV).

Kiunganishi/ Kipandikizi : Hiki ni kipande cha tyubu fupi ya mpira inayounganisha ateri na veni mkononi. Kipandikizo / Kiunganishi hiki huwekwa ili kuwezesha dayalisisi ya damu ya muda mrefu.Sindano huingizwa kwenye kipandikizi hiki wakati wa matibabu ya himodayalisisi.

Himodayalisisi : Hii ndiyo njia inayopendwa sana kutibu figo iliyofeli. Katika himodayalisisi damu husafishwa kwa kutumia mashine ya dayalisisi na figo la bandia (dialyzer)

Himoglobini : Himoglobin ni protini iliyo katika chembechembe ya damu nyekundu, Kazi yake kubwa ni kuchukua oksijeni kutoka kwenye mapafu hadi sehemu mbalimbali za mwili; na wakati huo huo hurudisha kaboni dioksidi kutoka sehemu mbalimbali za mwili kwenda kwenye mapafu. Himoglobini hupimwa kwenye damu na ikipungua huwa ni anemia.

Potasiamu ya hali ya juu (hyperkalemia) : Kiasi cha kawaida cha potasiamu kwenye damu ni kati ya 3.5 hadi 5.0 mEq/LPotasiamu huhesabika iko juu wakati kipimo huonyesha potasiamu iko zaidi ya 5.0mEq/L.Hali hii ni hatari kwa maisha na hujitokeza mgonjwa akiwa na figo zilizofeli na uhitaji matibabu ya haraka.

Shinikizo la damu (hypertension): Hutumika wakati shinikizo la damu liko juu.

Dawa zinazobadili kinga ya mwili : Dawa hizi hupunguza nguvu ya mwili kutambua chake na kisicho chake. Kwa sababu hiyo basi dawa hizi hutumika wakati wa kupandikiza figo ….nk ili mwili usikatae (rejection).kile kilichopandikizwa.

Picha Ya Mishipa ya Veni (IVU): Hiki ni kipimo ambapo picha hupigwa kwa mpangilio fulani baada ya kuchoma dawa kwenye veni. Kwa kuwa dawa hii hatimae hupita kwenye mfumo wa mkojo hivyo daktari huona jinsi figo zinavyofanya kazi na mfumo wote wa mkojo.

Kutoa kipande cha figo (kidney biopsy): Huu ni utaratibu wa kupata kipande kidogo cha figo kwa kutumia sindano. Kipande hiki kitakachopatikana huchunguzwa na utambuzi wa ugonjwa hufanyika.

Figo kushindwa (kidney failure): Hii ni hali ambapo utendaji kazi wa figo huendelea kushuka mpaka kiasi kwamba huondowaji wa sumu na takataka kutoka kwenye damu haufanyiki kabisa. Hali hii utambulika kwa ongezeko la yurea na kreatinini kwenye damu.

Albumini kwenye mkojo (Microalbuminuria) : Hii inahusu uwepo wa albumin ambayo si ya kawaida kwenye mkojo. Uwepo wa albumin unahashiria tatizo la kisukari kuathiri figo.

Mkojo Kurudi Nyuma : (Micturating cystourethrogram – angalia – voiding cystourethrogram).

Nephron: Hii ndiyo kitu ndani ya figo ambacho kinahusika hasa na kasafisha na kutakasisha damu. Kila figo lina takriban nephron milioni moja.

Mtaalamu wa figo (Nephrologist) : Huyu ni Mtaalamu bingwa wa magonjwa ya figo.

Ugonjwa wa figo unaosababisha kuvimba mwili (Nephrotic Syndrome): Huu ni ugonjwa wa figo unaojitokeza sana kwa watoto. Ugonjwa huu utambuliwa kwa kupoteza protini kwenye mkojo (zaidi ya gramu 3.5 kwa siku), kiasi cha protini huwa chini kwenye damu, kiasi cha mafuta ( kolesterol) huwa juu na uvimbe wa mwili.

Kutoa figo kwa kushirikiana (Paired kidney transplantation) : Wagonjwa wengi wenye ugonjwa wa figo hatua ya mwisho (ESKD) wanao watu wangalioweza kuwapa figo tatizo huwa aina ya kundi la damu au kuhusiana kwa figo zenyewe (Cross match incompatibility). Kutoa figo kwa kushirikiana huruhusu kubadilishana figo baina ya mtoaji na mpokeaji wote wakiwa hai na kuwezesha figo kupandikizwa.

Dayalisisi ya fumbatio (Peritoneal dialysis) : Hii ni njia bora ya matibabu ya figo iliyoshindwa.Katika njia hii ya matibabu, maji ya dialisisi huingizwa tumboni kupitia katheta maalumu. Maji haya huondoa takataka na maji ya ziada kutoka kwenye damu. Baada ya maji haya kuwepo tumboni kwa muda huondolewa . Yanapoondolewa hutoka na taka na hutupwa.

Uvimbe wa ngozi ya fumbatio (Peritonitis) : Haya ni maambukizo ndani ya tumbo. Maambukizo haya hutokea mara nyingi kwenye dialisisi ya fumbatio. Huatarisha maisha kama hayakutibiwa vizuri.

Fosforasi (Phosphorus) : fosforasi ni madini ya pili kwa wingi mwilini ikifuatana na kalsium. Hufanya kazi na kalsium kujenga mifupa na meno yenye nguvu. Nyama, njugu, maziwa, mayai, na nafaka ni chanzo kikubwa cha fosforasi.

Ugonjwa wa Vimbe Za Figo (Polycystic Kidney Disease - PKD) : Huu ni ugonjwa wa kurithi na unawaathiri watu wengi sana. Hutambulika kwa figo kuwa na uvimbe uvimbe mwingi, kila kiuvimbe kikiwa kimejaa maji maji. Tatizo hili ni la nne kwa kuleta ugonjwa sugu wa figo.

Potasiumu (Potassium): Ni madini muhimu sana mwilini yanayohitajika kwa ufanyaji kazi wa neva, moyo na musuli. Matunda (fresh), juisi za matunda, maji ya madafu, matunda yaliyokaushwa; vyote vina potasiumu nyingi.

Kupandikizwa figo kabla ya dayalisisi (Pre – emptive kidney transplant): Kwa kawaida upandikizwaji wa figo hufanywa baada ya matibabu ya dayalisisi yameendelea kwa muda. Ikiwa upandikizwaji wa figo uumefanyika kabla ya matibabu ya dayalisisi kama ilivyoelezwa kabla matibabu hayo yanahesabika kama kupandikizwa figo kabla ya dayalisisi.

Protini (Protein) : Protini ni moja ya aina tatu za vyakula vinavyojenga, vinavyofanya marekebisho na vinavyodumisha mwili. Chakula aina ya kunde, maziwa, mayai, chakula kitokanacho na nyama vyote vina kiasi kikubwa cha protini.

Protini kwenye mkojo (Proteinuria) : Uwepo wa kiasi cha juu cha protini kwenye mkojo.

Kukataliwa (Rejection) : Mwili wakati umepandikizwa kitu ambacho siyo chake hujaribu kukiharibu na hivyo kukikataa. Hali hii inaitwa kukataliwa.

Utando unaopenyeza vitu fulani fulani (semi permeable membrane): Utando huchagua kuruhusu maji na vitu fulani fulani

vilivyoyeyushwa kupita wakati huo huo huzuia vitu vingine kupita. Utando huu mwembamba unaweza kuwa wa asili au wa bandia.

Sodiamu (sodium): Haya ni madini mwilini yanayoweka sawa kiasi cha damu (volume) na shinikizo la damu. Aina inayopatikana sana ya sodiam ni ile iliyo katika chmvi ya kawaida tutumiayo mezani.

Upasuaji wa tezi dume kupitia urethra (TURP) : Hii ni njia inayotumika sana sasa ya kutibu tezi dume lililovimba. Operesheni inayofanywa na Madaktari Bingwa wa mfumo wa mkojo. Katika operesheni hii, mashine mashine maalumu inayoitwa sistoskopi (cystoscope) huingizwa kwenye urethra hadi sehemu ya tezi dume inayozuia mkojo. Sehemu hii ya tezi dume huondolewa ili kuruhusu mkojo kupita.

Picha zaUltrasound : Hiki ni kipimo ambacho hakina maumivu. Hutumia mawimbi ya sauti (high frequency). Mawimbi haya huweza kubaini maumbo na viungo vya mwili (ogani) ndani ya mwili. Kipimo hiki ni rahisi, chenye manufaa, na ni salama kinachotoa taarifa muhimu kama ukubwa wa figo, kizuizi kwenye mfumo wa mkojo, uwepo wa uvimbe uvimbe (cysts), mawe na saratani.(tumours).

Daktari Bingwa wa figo (urologist) : Huyu ni Daktari bingwa mpasuaji wa magonjwa ya figo.

Mkojo kurudi nyuma (vesicoureteral reflux – VUR) : Hii ni hali isiyo ya kawaida kwa mkojo kurudi nyuma kutoka kwenye kibofu kuelekea ureta na wakati mwingine hadi kwenye figo moja au zote mbili. Tatizo hili ni la kimaumbile (anatomical) na huweza kutokea upande mmoja au pande zote mbili za mwili. Kurudi mkojo nyuma ni tatizo kubwa liletalo maambukizo kwenye mfumo wa mkojo, shinikizo la damu, na figo kushindwa kufanya kazi hasa kwa watoto.

Kipimo cha kukojoa na kupima kwa picha – Voiding cystourethrogram (VUR) : Kipimo hiki hutumika kuangalia maumbile ya kibofu na urethra. Hufanyika kwa kuingiza dawa inayoweza kuonekana kwa eksrei. Baada ya kuwekwa dawa hii mgonjwa anaombwa kwenda kukojoa na picha za eksrei huchukuliwa.