Wazo Potofu:Magonjwa yote ya figo ni hatari.
Ukweli: La, magonjwa yote ya figo si hatari. Yakitambuliwa na kutibiwa mapema, magonjwa mengi ya figo yanaweza kuponywa. Kwa mengi, utambuzi na matibabu hupunguza au kusimamisha kuendelea kwa magonjwa hayo.
Wazo Potofu: Hitilafu ya figo huweza kutokea iwapo figo moja linahitilafu.
Ukweli: La, hitilafu ya figo hutokea iwapo figo zote mbili zimefeli. Watu hawahisi shida yoyote ikiwa figo moja imefeli kabisa,na kwa hali kama hiyo, kiwango cha yurea na kreatinini ya serami katika damu huwa kawaida. Lakini ikiwa figo zote zimefeli,uchafu hukusanyika mwilini na ongezeko la kiwango cha yurea na kreatinini ya serami katika damu huonyesha kiwango cha juu. Kuongezeka kwa kiwango cha yurea na kreatinini katika damu huonyesha kufeli kwa figo.
Wazo Potofu: Katika magonjwa ya figo, kuwepo kwa edema huonyesha kufeli kwa figo.
Ukweli: La, katika magonjwa ya figo mengine, kuna edema, lakini kazi ya figo ni kawaida (K.m uvimbe wa figo – Nephrotic Syndrome).
Wazo Potofu: Edema hupatikana kwa wagonjwa wote wenye hitilafu ya figo.
Ukweli : La, edema hupatikana kwa wagonjwa wengi wenye hitilafu ya figo, lakini si kwa wote . Wagonjwa wachache huwa hawana edema hata katika hatua ya mwisho ya hitilafu ya figo kwa hiyo ukosefu wa edema si uthibitisho kuwa mgonjwa unayemwona hana hitilafu ya figo.
Wazo Potofu: Wagonja wote wa ugonjwa wa figo wanapaswa kunywa maji mengi.
Ukweli:
La, upungufu wa utoaji wa mkojo hupelekea kwa mgonjwa
kuvimba. Hii ni sifa muhimu kwa magonjwa mengi ya figo. Kwa hiyo
kudhibiti kunywa maji ni muhimu/ lazima ili kudhibiti usawazishaji wa
maji kwa wagonjwa kama hao. Hata hivyo, wagonjwa wanaoumwa
ugonjwa wa mawe na maambukizi ya mfumo wa mkojo, wenye figo
zinazofanya kazi sawa sawa wanashauriwa kunywa maji mengi.
Wazo Potofu:
Najiona niko mzima, kwa hiyo sidhani nina shida ya
figo.
Ukweli:
Wagonjwa wengi hawaonyeshi dalili zozote katika hatua za
mwanzo za ugonjwa sugu wa figo. Uchunguzi wa kimaabara ndio
thibitisho pekee la kuwepo kwa shida ya figo.
Wazo Potofu:
Ninajihisi vyema, kwa hiyo sihitaji kuendelea na
matibabu ya tatizo langu la figo.
Ukweli:
Wagonjwa wengi wenye ugonjwa sugu wa figo (CKD) hujihisi
vyema, kwa hiyo huacha kuendelea na matibabu na lishe maalumu.
Kutoendelea na matibabu ya CKD huweza kuwa hatari. Inaweza
kusababisha kuzorota ghafla kwa hitilafu ya figo na kwa muda mfupi
wagonjwa kama hao wanaweza kufika hatua inayohitaji dayalisisi au
kubadilisha figo.
Wazo Potofu:
Kreatinini ya serami yangu iko juu kidogo tu ya ile ya
kawaida .Lakini niko salama kwa hiyo sina haja ya kuwa na wasi wasi.
Ukweli:
Hata ongezeko dogo tu ya kreatinini ya serami ni ishara ya
kulemaa kwa figo na uhitaji uchunguzi. Magonjwa mengi ya figo
yanaweza kuharibu figo, kwa hivyo mwone mtaalamu wa nefrolojia
bila kuchelewa. Hebu tuelewe umuhimu wa ongezeko la kiwango cha
kreatinini ya serami (hata kidogo) katika hatua na wakati tofauti wa
ugonjwa sugu wa figo.
Hatua za mwanzo za ugonjwa sugu wa figo huwa hazina dalili na
ongezeko la kiwango cha kreatinini ya serami linaweza kuwa kidokezo/
kithibitisho cha pekee la ugonjwa. Kiwango cha kreatinini ya serami
cha 1.6 mg/dl kina maana kuwa zaidi ya asili mia 50% ya kazi ya figo
imepotea tayari, taarifa hii ni muhimu sana. Ugunduzi wa ugonjwa sugu
wa figo na kuanzisha tiba sahihi katika hatua hii hutoa matokeo mazuri.
Matibabu chini ya mtaalamu wa nefrolojia katika hatua hii husaidia
kuhifadhi kazi ya figo kwa muda mrefu sana.
Ikiwa kiwango cha kreatinini ya serami ni 5.0 mg/dl, hii ina maana asili
mia 80% ya kazi ya figo imepotea. Kiwango hiki kinaonyesha kulemaa
sana kwa kazi za figo. Uchunguzi na matibabu sahihi katika hatua hii ni
ya manufaa ili kuhifadhi kazi za figo. Lakini ni muhimu kukumbuka kuwa
hatua hii ni ya mwisho ya ugonjwa sugu wa figo na nafasi pekee ya
kupata matokeo bora ya matibabu huwa imekwishapotea.
Ikiwa kiwango cha kreatinini ya serami ni 10.0 mg/dl ina maana asili
mia 90% ya kazi ya figo imepotea na kiwango hiki kinaonyesha hatua
ya mwisho ya ugonjwa wa figo. Katika hatua hii nafasi ya kumtibu
mgonjwa kwa kutumia dawa haupo tena. Wengi wa wagonjwa huhitaji
dayalisisi katika hatua hii.
Wazo Potofu:
Wagonjwa wenye hitilafu ya figo, wakifanyiwa dayalisisi
mara moja ina maana dayalisisi inakuwa hitaji la kudumu.
Ukweli:
La, muda anaohitaji mgonjwa wa hitilafu ya figo kufanyiwa
dayalisisi hutegemea aina ya hitilafu ya figo.
Hitilafu kali ya figo hudumu kwa muda na ni aina inayoweza kurekebishwa
kwenye hali yake ya awali. (reversible). Wagonjwa wachache wenye
hitilafu kali ya figo huitaji usaidizi wa dayalisisi kwa kipindi kifupi. Kwa
matibabu machache ya dayalisisi (few dialysis sessions),figo hupona
kabisa katika hitilafu hii. Kuchelewa kumfanyia dialysis mgonjwa, kwa
woga kwamba mgonjwa atahitaji dayalisisi ya muda mrefu/ya kudumu
kunaweza kuhatarisha maisha ya mgonjwa.
Hitilafu sugu ya figo huwa mbaya zaidi kila kukicha na hairudi nyuma.
Hitilafu sugu ya figo, ikifikia hatua ya mwisho (End Stage Kidney
Disease), mgonjwa huyu atahitaji dayalisisi maisha yake yote.
Wazo Potofu:
Dayalisisi hutibu hitilafu ya figo.
Ukweli:
La, dayalisisi haitibu hitilafu ya figo. Dayalisisi ni tiba maalumu
ya kuokoa maisha katika hitilafu ya figo ambalo limeshindwa kutoa
uchafu, maji mengi na kusahihisha elektro- laiti na pia usumbufu wa
acid base.Dayalisisi hufanya kazi ambayo figo haiwezi tena kufanya.
Dayalisisi huweka mgonjwa kutokuwa na dalili, sawa na mtu mwenye
afya hata akiwa na hitilafu kubwa ya figo.
Wazo Potofu:
Katika kubadilisha figo, mtu jinsi ya kiume na wa kike
hawawezi kuchangia figo zao kwa jinsia tofauti.
Ukweli:
Wanaume na wanawake wanaweza kuchangia figo zao kwa
jinsia tofauti kwa kuwa muundo na kazi ya figo zao ni sawa.
Wazo Potofu:
Mchango wa figo huathiri afya na kazi ya uzazi.
Ukweli:
Kuchangia figo ni salama sana na haina athari kwa afya na kazi
ya uzazi. Wachangiaji wa figo huishi maisha ya kawaida yanayo jumuisha
ndoa na kuzalisha watoto.
Wazo Potofu:
Kwa kubadilisha figo, inawezekana kununua figo.
Ukweli:
Kununua au kuuza figo ni hatia. Kumbuka kuwa figo
linalopandikizwa hutoka kwa figo hai isiyo na uhusiano na figo ya
mchangiaji. Figo inayopandikizwa huwa na hatari ya kukataliwa
ikilinganishwa na figo yenye uhusiano.
Wazo Potofu Sasa, msukumo wangu wa damu ni kawaida kwa hiyo
sihitaji tembe za kurekebisha msukumo wa juu wa damu yangu..Mimi
huhisi vyema hata nisipomeza tembe hizi kwa hiyo kwa nini niendelee
kuzitumia?
Ukweli :
Wagonjwa wengi wa msukumo wa damu husita kutumia dawa
baada ya hali hii kudhibitiwa ,kwa kuwa hawana dalili zozote tena,
wanahisi kuwa sawa,bila dawa. Lakini msukumo wa damu usiodhibitiwa
huuwa kimya kimya. Baada ya muda mrefu, huweza kusababisha shida
kubwa kama shambulio la moyo, hitilafu ya figo na kupooza . Kwa
hiyo ili kulinda viungo muhimu vya mwili, ni vyema kumeza dawa hata
kama hakuna dalili za msukumo wa damu ambao umetambulika na mtu
kuhisi vyema.
Wazo Potofu:
Wanaume pekee ndio wana figo ambazo zimo kwenye
mfuko kati ya miguu.
Ukweli :
Kwa wanaume na wanawake wote figo zao zipo kwenye
sehemu ya juu na nyuma ya tumbo na ni za ukubwa, umbo na kazi
sawa.
Kwa wanaume, kiungo muhimu cha uzalishaji, kende, kipo kwenye
kifuko kati ya miguu.