12: Ugonjwa Sugu wa Figo: Matibabu

Aina tatu zamatibabu ya ugonjwa sugu wa figo ni:

 1. Dawa.
 2. Dayalisisi, yaani mashine kufanya kazi inayofanywa na figo.
 3. Kuwekwa figo la mtu mwingine.
 • Mwanzoni,kila mgonjwa hutibiwa kwa dawa,ushauri wa vyakula na kufuatiliwa mara kwa mara.
 • Figo zinapodhoofika zaidi na kufikia hatua ya mwisho ya ugonjwa,lazima kazi yake ifanywe kwa mashine(dayalisisi)au figo ibadilishwe / ipandikizwe nyingine.

Matibabu ya kutumia dawa

Umuhimu
Hakuna tiba ya ugonjwa sugu wa figo. Ukizidi, lazima dayalisisi itumiwe au figo ibadilishwe ili mgonjwa aendelee kuishi . Kwa sababu gharama ya matibabu haya ni ghali na ni nadra, wagonjwa kati ya asilimia 5 hadi 10 (5 - 10%) wanaopata matibabu haya ya dayalisisi au kuwekewa figo jingine,ilhali wagonjwa wengi wengine hufa bila ya kupata matibabu yoyote yanayofaa.

Kwa hivyo kutambulika mapema na kutibiwa vizuri kwa dawa ndiyo njia rahisi na ya pekee ya kutibu ugonjwa sugu wa figo na huhairisha haja ya dayalisisi au figo nyingine .

Matibabu ya mapema humwezesha mtu kuishi maisha marefu.
Kwa nini wagonjwa wengi hawafaidiki na dawa?

Kuanza dawa mapema husaidia sana.Wagonjwa wengi huwa hawaonyeshi dalili zozote au hujihisi vyema kabisa kwa hiyo hawaoni umuhimu wa kuanza matibabu mapema.Kwa sababu hii,wagonjwa wengi na familia zao huwa hawatambui hatari ya ugonjwa huu na huacha kuzingatia dawa na maagizo ya vyakula.Kuacha kuzingatia matibabu huzorotesha zaidi figo kwa haraka na kwa muda mfupi . Wagonjwa hawa huenda wakahitaji njia hizo ghali za matibabu kama dayalisisi au kubadilishwa figo.

Malengo ya matibabu ya kutumia dawa ni nini katika ugonjwa sugu wa figo?

Ugonjwa huu sugu wa figo huwa ni hali inayoendelea na hauna tiba. Kwa hiyo,kukabiliana nao kwa kutumia dawa unalenga:

 1. Kupunguza makali/kukua kwa ugonjwa.
 2. Kutibu vyanzo vya ugonjwa na vihashiria vingine vinavyochangia.
 3. Kupunguza makali ya ugonjwa na kutibu matatizo mengine/ nyemelezi ya ugonjwa huu.
 4. Kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo.
 5. kuahirisha haja ya dayalisisi au figo nyingine.
Njia za kutibu ugonjwa sugu wa figo usiokwisha kulingana na vipindi vyake mbali mbali ni zipi?

Njia mbalimbali za matibabu zinazopendekezwa katika hatua tofauti za ugonjwa sugu wa figo zimeonyeshwa kwa kifupi hapo chini.

Ugonjwa huu hauponi lakini matibabu ya mapema husaidia sana.

Hatua Hatua mwafaka
Wakati wote
 • Kupimwa mara kwa mara. Kuzingatia ushauri wa daktari na kubadilisha mwenendo wa maisha(life style).
1
 • Kutambua na kutibu ili kupunguza kukua kwa ugonjwa.Kuwafunza / kuwaelimisha wagonjwa jinsi ya kukabiliana na ugonjwa huu. Kutibu magonjwa yanayoambatana na ugonjwa wa figo, kupunguza hathari ya ugonjwa huu kwenye moyo.
2
 • Kutathmini kukua kwa ugonjwa na kutibu magonjwa yanayohusiana.(Co morbid conditions)
3
 • Kutathmini na kutibu matatizo yanayotokana na ugonjwa sugu wa figo, na mgonjwa ashauriwe kumwona daktari bingwa wa figo.
4
 • Kuwafunza wagonjwa kuhusu njia za kubadili sha figo. Mgonjwa atayarishwe kwa matibabu ya kubadili figo.
5
 • Mashine kufanya kazi ya figo (dyalisisi) au kuwekewa figo nyingine.

Hatua tisa za kukabiliana na ugonjwa sugu wa figo usiokwisha
1. Kukabiliana na chanzo cha ugonjwa

kutambua na kutibu hali zilizo tajwa hapa chini husaidia. Hii inaweza kusaidia,kuzuia na hata kupunguza kukua kwa ugonjwa huu sugu wa figo.

 • Kisukari na shinikizo la damu
 • Maambukizo ya njia ya mkojo au kuziba kwa mfumo huo ugonjwa wa kuvimba mishipa midogo ya figo (glomerulonephritis),au shida za mishipa ya damu kwenye figo, Figo kujeruhiwa na dawa za kutuliza maumivu (analgesic nephropathy).
Kutibu chanzo cha CKD huahirisha kukua kwa ugonjwa huu sugu wa figo.

2. Njia za kupunguza kukua kwa ugonjwa sugu wa figo

Njia muhimu na yenye manufaa ya kupunguza makali ya ugonjwa sugu wa figo ni:

 • Kuzuia shinikizo la damu
 • Kuzuia protini
 • Kupunguza mafuta na kutibu anaemia

3. Kutibu dalili za ugonjwa wa figo na hatua nyingine zinazosaidia

 • Dawa za kumfanya mgonjwa akojoe ili kuongeza mkojo na kupunguza mwili kuvimba.
 • Dawa za kuzuia kichefuchefu,kutapika na matatizo ya tumbo.
 • Kumpa vitamin/dawa zenye kalsiamu,fosfati, na dawa muhimu ili kurekebisha ugonjwa wa mifupa unaohusiana na ugonjwa sugu wa figo na mifupa.
 • Kurekebisha ukosefu wa himoglobini ( anemia) , kwa vitamini , dawa zenye asili ya chuma au sindano maalum ya kuongeza chembechembe za damu (erythropoietin).
 • Kuzuia magonjwa ya moyo kwa kumeza dawa ya aspirini kila siku iwapo haijakatazwa na daktari.
Kutibu maambukizi na kupunguza maji mwilini husaidia sana katika ugonjwa sugu wa figo.

4. Kukabiliana na hali zinazoweza kurekebishwa

Chunguza na utibu magonjwa yaliyochangia au kuzidisha ugonjwa.Unapotibu magonjwa haya,figo huenda ikapata nafuu na kurudia kazi yake kidogo kidogo. Mambo kadhaa yanayochangia ugonjwa sugu wa figo ni pamoja na.

 • Figo kubwa na kupunguka
 • Figo kudhoofika kwa sababu ya dawa zenye sumu (kwa mfano non steroidal anti – inflammatory drugs, NSAIDs, antibioticsnk)
 • Maambukizi na ugonjwa wa moyo

5. Chunguza na utibu matatizo ya ugonjwa sugu wa figo

Matatizo haya huhitaji kutambuliwa na kutibiwa mapema na mara moja. Matatizo yaliyo hatari ni kama kreatinini kuzidi zaidi mwilini,potasimu nyingi kwenye damu ( potassium zaidi ya 6.0mEq/L) ,kuadhirika sana kwa figo, moyo, ubongo na mapafu.

6. Kubadilika kimaisha na hatua za jumla zifaazo

Hatua hizi ni muhimu kwa kupunguza hatari ya magonjwa ya figo kwa ujumla:

 • Acha kuvuta sigara.
 • Uwe na uzito unaofaa,fanya mazoezi na shughuli mbalimbali.
 • Jizuie kunywa pombe.
 • Zingatia mpango wa vyakula bora na punguza chumvi.
 • Kunywa dawa kama ulivyoagizwa,kulingana na ukali wa ugonjwa.
 • Kapimwe na chukua dawa zako kama utakavyoelekezwa na daktari wako bingwa wa figo.
Kuzingatia ushauri wa vyakula huzuia ugonjwa kukua haraka na huzuia matatizo.

7. Ushauri wa vyakula

Ni lazima vyakula vinavyofaa vizingatiwe. Hii hutegemea aina na ukali wa ugonjwa.

 • Chumvi: Ili kuzuia shinikizo la damu na kuvimba mwili,lazima chumvi izuiwe.Usiongeze chumvi kwenye vyakula vilivyopakuliwa na jizuie vyakula vyenye chumvi nyingi.
 • Vinywaji: wagonjwa waliovimba mwili wanashauriwa kuzuia vinywaji. Kupungua kwa mkojo husababisha kuvimba na kushidwa kupumua. Wagonjwa wote walio na uvimbe na CKD wasinjwe maji mengi.
 • Potasiamu: Hili ni tatizo kwa wagonjwa wengi wa figo. Potasium ina hatari kubwa kwa moyo kuzuia vyakula vyenye potasiamu kama maji ya nazi /madafu,viazi,machungwa,ndizi, nyanya n.k, kulingana na ushauri wa daktari.
 • Protini: Wagonjwa wa CKD wazuiwe kula protini nyingi kwani huweza kuzidisha kudhoofika kwa figo.

8. Matayarisho ya kubadili figo

 • Kinga mishipa ya mkono wa kushoto(au mkono ule ambao hautumiki sana) punde tu ugonjwa utambulikapo.
 • Mishipa ya mkono wa kushoto isitumiwe kutolewa damu wala kuwekwa dawa.
 • Wagonjwa na jamaa zao wafunzwe mambo muhimu na wagonjwa watayarishwe kwa.
 • Dayalisisi, kwa kupanua mishipa ya mkono ili dawa iweze kupitishiwa hapo. Ni vizuri.
 • Upasuaji huu ufanywe miezi sita hadi kumi na miwili kabla ya kuanza dayalisisi.
 • Kupewa chanjo ya homa ya maini (hepatitis B) mwanzoni mwa ugonjwa huzuia hatari ya kupata homa ya maini (hepatitis B) dayalisi inapoendelea au figo inapobadilishwa. Dozi nne (miezi 0,1,2,na 6}za chanjo ya homa ya ini zinafaa kupatiwa mgonjwa kwa kudungwa sindano kwenye msuli.
 • Mgonjwa aelimishwe na atayarishwe kwa dayalisisi au/na kubadilishwa figo.Fikiria faida za kupatiwa figo na mtu aliye mzima kabla ya kuanza dayalisisi.
Matibabu muhimu sana ili kupunguza kukua kwa ugonjwa sugu wa figo ni kudhibiti shinikizo la damu: Liwe chini ya 130/80mmHg.

9. Kutumwa kwa daktari wa figo

Mtu mwenye ugonjwa sugu wa figo anafaa kutumwa kwa daktari bingwa wa figo mapema.Hii pamoja na mafunzo kabla ya dayalisisi huzuia kudhoofika na hata kufa.Kumwona daktari mapema huzuia kukua kwa ugonjwa haraka na hata kuahirisha kubadili figo.

Ni hatua gani muhimu sana ya kuzuia ugonjwa wa figo kuzidi?

Haijalishi chanzo cha ugonjwa sugu wa figo,ni jambo la umuhimu mkubwa kudhibiti shinikizo la damu.Shinikizo la damu lisipozuiwa,ugonjwa wa figo huzidi kwa haraka na huenda ukasababisha ugonjwa wa ubongo unaosababisha pigo/shambulizi la moyo au kupooza (kiharusi).

Je,ni dawa gani hutumika kudhibiti shinikizo la damu?

Daktari bingwa atachagua dawa inayofaa pamoja na ile ya kumfanya mgonjwa akojoe.Dawa hizi huzuia kukua kwa ugonjwa wa figo na hivyo kulinda figo.

Lengo la kudhibiti shinikizo la damu ni nini katika ugonjwa sugu wa figo?

Ugonjwa sugu wa figo unaweza kuchangia shinikizo la damu na pia shinikizo la damu nalo huzidisha ugonjwa sugu wa figo. Kwa hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa shinikizo la damu liko chini ya 130/80 mmHg.

Njia gani mwafaka ya kufuatia na kupima shinikizo la damu katika CKD?

Kwenda kwa daktari mara kwa mara ndiyo njia bora ya kujua hali ya shinikizo la damu.Hata hivyo,ni vyema zaidi kununua kifaa cha kujipima nyumbani (kama unaweza).Weka rekodi ya vipimo ili daktari aweze kubadilisha dozi ya dawa na wakati wa dawa kulingana na vipimo hivyo.

Dawa za kumfanya mgonjwa kukojoa humsaidiaje mgonjwa wa figo?

Mkojo unapopungua huenda ukasababisha kuvimba na hata kushindwa kupumua.

Dawa za kumfanya mgonjwa kukojoa husaidia kuongeza mkojo na hivyo kupunguza kuvimba mwili na kushindwa kupumua.Ni muhimu kukumbuka kwamba dawa hizi husaidia kuongeza mkojo lakini si kusaidia figo kufanya kazi.

Matibaba muhimu sana ya kuhairisha ugonjwa wa CKD kuendelea ni kudhibiti kwa makini msukumo wa damu ili uwe chini ya 130/80.

Kwa nini mgonjwa hupata anemia na hali hii hutibiwa vipi?
Anemia ni kupungua kwa chembechembe za damu. Wakati figo zinafanya kazi vizuri,hutengeneza homoni inayoitwa erithropoyetini inayosaidia mifupa kutengeneza chembechembe nyekundu za damu.Mtu anapopata ugonjwa sugu wa figo,Kazi ya figo pia hupungua na kwa hiyo homoni hii hupungua na mgonjwa hupata anemia.

Tembe za madini ya chuma,vitamini na wakati mwingine sindano za madini ya chuma ndizo hatua za kwanza za kutibu anemia inayotokana na ugonjwa wa figo.Anemia kali au isiyosikia dawa huhitaji sindano za homoni ya erithropoyetini ambayo husaidia mifupa kutengeneza chembechembe nyekundu ambazo zina kazi ya kusambaza hewa ya oksijeni.Njia hii ya sindano ya erithropoyetini ni salama na bora zaidi.Kuwekewa damu ni njia ya haraka ya kurekebisha matatizo ya anemia lakini haipendelewi kwa sababu ya hatari yake ya kusambaza maambukizi na mzio (allergic reactions).

Kwa nini ni muhimu kutibu anemia katika ugonjwa wa figo.

Chembechembe nyekundu za damu husambaza oksijeni kutoka kwenye mapafu kwenda sehemu zote za mwili.Oksijeni humpatia mtu uwezo wa kufanya shughuli za kawaida za kila siku na huwezesha moyo kubaki katika hali nzuri.Anemia ni hali ya kupungua kwa chembechembe nyekundu za damu au himoglobini.Husababisha udhaifu,uchovu,kutokuwa na nguvu ya kufanya mazoezi,kushidwa kupumua baada ya kazi kidogo,moyo kupiga kwa haraka,kukosa umakini,kuhisi baridi sana na maumivu ya kifua.Kwa hivyo,huhitaji matibabu yanayofaa,na mapema.