Kati ya magonjwa tofauti ya figo, ugonjwa huu wa figo huogopwa sana kwani sayansi ya matibabu haina tiba yake.Magonjwa ya kudhoofisha figo yanaongezeka kwa haraka sana duniani kote. Mtu mmoja kwa kila watu kumi ana aina fulani ya ugonjwa wa figo usiopona. Kuongezeka kwa kisukari, matatizo ya shinikizo la damu,unene zaidi,uvutaji wa tumbaku na mafuta mengi mwilini(cholesterol) ndizo sababu kuu za ongezeko la ugonjwa huu usiopona wa figo.
Ugonjwa sugu wa figo ni upi?
Figo kudhoofika kwa muda mrefu wa miezi hata miaka,na kushindwa kufanya kazi zake . Hali hii ndio ugonjwa sugu usiopona wa figo.Ishara kuu za ugonjwa huu ni ongezeko la umajimaji wa kreatinini katika damu na figo kupungua kwa ukubwa /kusinyaa. Kwa wagonjwa wengi ne huwa hazishindwi kufanya kazi yake kabisa, bali uwezo wake hupungua kiasi. Kwa hivyo kufeli haina maana ya kushindwa kabisa na kazi zake.
Kipindi cha mwisho cha ugonjwa wa figo ni kipi?
Kipindi hiki cha tano cha ugonjwa wa figo ndio husemekana kuwa figo zimefeli.Kazi yake hupungua sana, karibu kukoma kabisa. Ugonjwa huu unapozidi, kazi za figo hupungua hadi asili mia kumi (10%) ya zile za kawaida. Figo zinapofikisha kiasi hiki, huwa haziponi kwa kutumia matibabu yake ya msingi na huhitaji dayalisisi au kupatiwa figo ili kuendelea na uhai /maisha.
Ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu ndizo sababu kuu za ugonjwa wa figo usiokwisha.
Chanzo cha ugonjwa sugu wa figo ni nini?
Mambo kadha yanaweza kusababisha madhara yasiyotibika kwa figo lakini vyanzo vikuu ni ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu.Hali hizi mbili husababisha asilimia sabini na tano ya ugonjwa sugu wa figo usiopona.
Sababu kuu za ugonjwa wa figo usiopona ni:
1. Kisukari:
Kisukari ndicho sana sana husababisha ugonjwa wa figo.Asilimia 35- 40 ya magonjwa ya figo yasiyopona yote huletwa na kisukari. Tuseme kwa kila watu watatu walio na ugonjwa wa kisukari, mmoja wao anaweza kupata ugonjwa sugu wa figo.
2. Shinikizo la damu:
Hali hii isipotibiwa au isipothibitiwa kwa njia ifaayo,huwa ni chanzo kikubwa cha ugonjwa wa figo. Asili mia 30 ya magonjwa ya figo yasiyopona huletwa na shinikizo la damu. Hata kama ugonjwa wa figo umesababishwa na hali nyingine, shinikizo la damu hudhuru figo zaidi.
3. Ugonjwa wa uvimbe kwenye figo (Glomerulonephritis)
Ugonjwa huu ni wa tatu katika kuchangia magonjwa yote yanayoleta magonjwa sugu ya figo.
4. Polycycystic Kidney Disease
Shida hii ya uvimbe kwenye figo zote mbili ni ugonjwa unaoweza kurithiwa (toka kwa wazazi).Hali hii husababisha ugonjwa wa figo kutokana na uvimbe (cysts)kwenye figo zote.
5. Sababu nyingine:
Figo kuzeeka, kufunga kwa mishipa iendayo kwenye figo (renal artery stenosis), mkojo kuzuiwa na mawe ya figo au tezi dume iliyo karibu na kibofu kuvimba,figo kuharibiwa na dawa Fulani fulani, maambukizo ya figo ya mara kwa mara kwa watoto na pia kupunguka kwa ukubwa wa figo na mwisho mkojo kurudi nyuma.