Ugonjwa wa figo unaoletwa na kisukari
Idadi ya wagonjwa wa kisukari(diabetes)inaongezeka kwa kasi mno,ulimwenguni kote.Tatizo kuu ni ongezeko la ugonjwa wa figo unaosababishwa na ugonjwa wa kisukari. Ugonjwa wa figo unaoletwa na kisukari ni moja ya matokeo mabaya sana ya kisukari na huleta vifo vingi.
Ugonjwa wa figo wa kisukari ni upi?
vya figo kuharibika.Vinapoharibika, protini hupotea kwenye mkojo. Hali hii nayo husababisha shinikizo la damu (hypertension) , mwili kuvimba na figo kuanza kudhoofika. Mwisho figo hushindwa kufanya kazi (ESKD). Huu ndio ugonjwa wa figo wa kisukari (Diabetic nephropathy).
Kwa nini ni muhimu kujua kuhusu ugonjwa wa figo unaotokana na kisukari?
- Ugonjwa wa kisukari unaongezeka kwa kasi kubwa mno duniani kote.
- Ugonjwa huu ndio chanzo kikuu cha ugonjwa sugu wa figo.
- Wagonjwa kama asilimia arobaini hadi hamsini walio katika kipindi cha mwisho cha ugonjwa wa figo(ESKD) ni wagonjwa wa kisukari.
- Ugonjwa wa figo unahitaji tiba ya gharama kubwa kutibiwa na watu wengi katika nchi zinazoendelea hawawezi kugharamia.
- Utambuzi na matibabu ya mapema yanaweza kuzuia ugonjwa wa figo. Kwa wenye kisukari ambao wana ugonjwa sugu wa figo, matibabu ya mapema huhairisha haja ya dayalisisi au kupatiwa figo.
- Ugonjwa wa figo wa kisukari huongeza hatari ya kufa kutokana na matatizo ya moyo.
- Hivyo utambuzi wa mapema wa ugonjwa huu wa figo unaotokana na kisukari ni muhimu sana.
Ugonjwa wa kisukari ndio mara nyingi husababisha ugonjwa sugu wa figo.
Ni wagonjwa wangapi wa kisukari hupata ugonjwa wa figo?
Ugonjwa wa kisukari ni wa aina mbili. Lakini kila aina ina hatari yake ya kusababisha ugonjwa wa figo.
Aina ya ugonjwa wa kisukari unaohitaji dawa ya insulin (Aina 1)
Aina ya kwanza (Type -1) huanza mtu akiwa na umri mdogo na huhitaji dawa ili kuuthibiti . Aslimia 30 - 35 ya walio na aina hii hupata ugonjwa wa figo.
Aina ya ugonjwa wa kisukari usiotegemea insulin (Aina 2)
Aina ya -2 ya kisukari sana sana huwapata watu wazima na mara nyingine huweza kuthibitiwa bila insulin. Asilimia 10- 40 ya wagonjwa wa aina hii ya kisukari huenda wakapata ugonjwa wa figo.Aina hii ya pili ndio chanzo kikuu cha ugonjwa wa figo usiopona. Mtu mmoja kati ya wagonjwa wapya watatu hupata shida hii.
Ni mgonjwa yupi wa kisukari anaweza kupata ugonjwa wa figo?
Ni vigumu kujua mgonjwa yupi aliye katika hatari zaidi ya kuupata ugonjwa wa figo,ingawaje kuna ishara zinazoashiria kama:
Kisukari ni chanzo kikuu cha ugonjwa wa figo ulio katika hatua ya mwisho, mgonjwa mmoja kati ya watatu huwa na shida hiyo.
- Mtu kapata aina ya kwanza ya kisukari kabla ya kufikisha umri
wa miaka ishirini.
- Ugonjwa wa kisukari usiotibiwa vizuri.( kiasi cha juu cha HbA1c)
- Shinikizo la damu lisilotibiwa/lisilodhibitiwa vizuri.
- Historia ya kisukari kwenye familia na hasa ikiambatana na ugonjwa
sugu wa figo.
- Matatizo ya macho.(diabetic retinopathy), au uaribifu /tatizo la neve
kwa sababu ya kisukari (diabetic neuropathy).
- Protini kwenye mkojo,uzito mkubwa,uvutaji wa sigara na ongezeko
la mafuta kwenye damu.
Ugonjwa wa figo huanza lini kwa mgonjwa wa kisukari?
Ugonjwa sugu wa figo huchukua muda mrefu kwa hiyo ni vigumu
kuupata katika miaka kumi ya kwanza ya kisukari. Dalili huonekana
kama miaka kumi na mitano hadi ishirini baada ya aina ya kwanza
ya kisukari kuanza.
Iwapo mgonjwa wa kisukari hajapata ugonjwa wa figo baada ya
miaka ishirini na mitano,basi hatari ya kuupata hupungua.
Je ni lini mgonjwa wa kisukari anaweza kuwa na ugonjwa
wa figo:
- Anapokojoa mkojo wenye povu au kuna protini kwenye mkojo
akipimwa.
- Anapopata shinikizo la damu au kama alikuwa na shinikizo la damu
basi hali hiyo kuzidi kuwa mbaya.
- Vifundo vya miguu, miguu na uso kuvimba, mkojo kupungua na uzito
wa mwili kuongezeka.
Dalili za madhara ya kisukari huwa ni protini kwenye
mkojo unapopimwa, shinikizo la damu na kuvimba mwili.
- Kupungua mahitaji ya dawa ya insulin na dawa nyingine zinazotumika kutibu kisukari.
- Mgonjwa ambaye ghafla anakuwa na historia ya kuhitaji kipimo cha dawa kidogo kuiweka sukari yake kuwa chini.
- Historia ya mgonjwa kuwa na matukio ya kisukari mwilini kushuka. Aidha kusaidiwa na dawa za kisukari ambazo hapo awali zilikuwa hazimsaidii.
- Mgonjwa kujihisi vyema hata bila kutumia dawa.Wagonjwa wengi hufurahi kupona kisukari lakini ukweli ni kwamba figo za mgonjwa sasa huwa zinazidi kudhoofika.
- Dalili za ugonjwa sugu wa figo huanza kuonekana; kama vile uchovu/kuchoka, kukosa hamu ya chakula, kichefuchefu, kutapika, kujikuna, kuonekana mgonjwa mgonjwa, na kushindwa kupumua.Hizi ni dalili ambazo huonekana ugonjwa ukiwa umeendelea zaidi.
- Vipimo vya kreatinini na yurea huwa juu katika damu.
Je,ugonjwa wa figo unaoletwa na kisukari hujulikanaje na ni uchunguzi upi unaweza kuutambua mapema?
Vipimo viwili ambavyo ni muhimu sana ni kile cha protini kwenye mkojo na kreatinini kwenye damu. Kipimo cha kwanza ambacho huweza kutambua ugonjwa huu wa figo,mapema ni kile kinachoweza kuonyesha kiasi kidogo kabisa cha albumin kwenye mkojo. Albumini ni aina ya protini kama ile inayopatikana katika uteyai.
Kipimo kingine ni kile cha kawaida kinachoonyesha uwepo wa albumin nyingi kwenye mkojo.
Kipimo cha kreatinini ndicho huonyesha kazi inayofanywa na figo. Kiasi cha kreatinini huongezeka kwenye damu katika kipindi cha mwisho, yaani ugonjwa ukiwa umekomaa sana.
ONYO:Kama sukari katika damu inashuka mara kwa mara au kisukari kinajidhibiti bila dawa, ni muhimu ufikirie uwepo wa ugonjwa wa figo.
Je kiasi kidogo na kikubwa cha albumin kwenye mkojo (micro/ macroalbuminuria) maana yake ni nini?
Albuminuria maana yake kuwepo kwa albumin kwenye mkojo. Kiasi cha albumin kinaweza kuwa kidogo (30 – 300mg/siku) ambayo ni vigumu kutambuliwa katika vipimo vya kawaida. Hutambulika tu kwa vipimo maalumu. Albumin ikiwa zaidi ya 300mg/siku huweza kupimika na njia ya kawaida (urine dipstick test).
Kwa nini kipimo kinachoonyesha kiasi kidogo kabisa cha albumin huwa bora zaidi?
- Huwa bora zaidi kwani huweza kutambua mapema ugonjwa wa figo unaoletwa na ugonjwa wa kisukari,—kwa hiyo ugonjwa huweza kutambulika, kuzuiwa mapema na hata kuponywa kama matibabu bora yakizingatiwa.
- Kipimo hiki huweza kuutambua ugonjwa huu miaka mitano mapema zaidi kuliko kile kipimo cha kawaida.pia,miaka mingi kabla ya ugonjwa kuwa hatari na kuonyesha dalili kama zile za ongezeko la kreatinini kwenye damu.
- Zaidi ya kuhashiria tatizo kubwa kwenye figo, lakini kiasi hiki kidogo cha albumin ni ishara kubwa ya hatari ya mgonjwa huyu kupata shida kwenye mfumo wa damu na moyo.
- Kutambua hatari ya magonjwa ya mfumo wa damu na moyo humsaidia madaktari kuwa na nafasi ya kuwatibu wagonjwa hawa kwa bidii na uangalifu zaidi(more vigorously).
Vipimo viwili muhimu vya ugonjwa wa figo unaoletwa na kisukari ni kupima mkojo kama una protini na kreatinini kwenye maji maji ya damu (serami).
Wagonjwa wanafaa kupimwa mara ngapi?
Kwa wagonjwa wa aina ya kwanza(Aina 1)ya kisukari,vipimo hufanywa miaka mitano baada ya ugonjwa kuanza,halafu kila mwaka baada ya hapo.
Wagonjwa wa Aina 2, vipimo hufanywa ugonjwa unapotambuliwa na kila mwaka baada ya hapo.
Mkojo hupimwaje?
Kwanza hupimwa kwa kipimo kile cha kawaida iwapo hakuna protini inapatikana,kipimo kingine hufanywa ambacho kinaweza kuonyesha hata kiasi kidogo sana cha protini ya albumini.Ikiwa vipimo viwili kati ya vitatu vilivyofanywa katika kipindi cha miezi mitatu hadi sita vinaonyesha albumin,basi ugonjwa wa figo huwa umedhibitishwa.Lazima mtu awe hana maambukizi ya njia ya mkojo anapopimwa.
Mkojo hupimwa kwa njia tofauti:
- Kwa kutumia mkojo kidogo tu unaomwagwa kwenye kidonge / tembe au kitu chenye kemikali na kuangaliwa (strip au tablet).
- Kwa kupima albumin na kreatinini katika mkojo wa asubuhi.(Albumin – To – Creatinine Ratio).
- kwa kupima mkojo wa siku nzima. (mkojo wa saa 24).
Kupimwa mkojo kila mwaka ndiyo njia bora ya kuutambua ugonjwa wa figo mapema kwa wagonjwa wa kisukari.
Kipimo cha kawaida cha mkojo kinaweza kusaidiaje kutambua ugonjwa wa figo?
Kwa wagonjwa wa kisukari ,kipimo cha mkojo ndiyo njia rahisi na ya haraka ya kuonyesha uwepo wa protini ya uteyai (albumini). Inapopatikana kwa wingi basi humaanisha kwamba ugonjwa wa kisukari umezidi-yaani uko katika hatua yanne na hufuatwa na ugonjwa sugu wa figo.
Kwa sababu kipimo kinachoweza kuonyesha kiasi kidogo kabisa cha albumin huwa ghali sana,basi kile cha kawaida hutumika kwa wagonjwa wa kisukari.Hii ni njia rahisi na hupatikana kwenye vituo vingi vya afya.
Matibabu bora yakianzishwa,husaidia kuahirisha haja ya dayalisisi au kupatiwa figo.
Njia nzuri na ambayo hutumika sana ni kutumia “dip stick” inayopima protini kwenye mkojo. Kwa mgonjwa wa kisukari pakiwa na albumin zaidi ya 300mg/siku hii si dalili nzuri. Hii uambatana na dalili nyingine za “nephritic syndrome”na kuongezeka kwa kreatinini kwenye damu, hii ni kwa sababu ya ugonjwa sugu wa figo.
Kipimo cha dip-stick cha mkojo ni njia rahisi na isyoghali na ingeweza kuwepo hata kwenye vituo vya chini vya afya. Kipimo hiki kingeweza kutumika kwa kupima watu wengi kama wana ugonjwa wa figo wa kisukari. Kuutambua ugonjwa hata mapema hivi ina tija zaidi kuliko kungojea hadi mgonjwa ahitaji dayalisisi au kupandikizwa figo.
Ugonjwa wa figo wa kisukari hutambuliwaje?
Njia bora: Wagonjwa wa kisukari wapimwe mkojo kila mwaka kujua iwapo una protini na kupima damu na kuona kiwango cha kreatinini. Njia nyingine nzuri ni kila miezi mitatu kupima shinikizo la damu , kupimwa mkojo na damu pia si ghali.
Kipimo cha kijiti cha kubaini protini nyingi kwenye mkojo ni kipimo pekee na muhimu cha kubaini shida hii katika nchi zinazoendelea.
Kuzuia ugonjwa wa figo unaoletwa na kisukari. Fanya yafuatayo:-
- Mwone daktari wako mara kwa mara. Dhibiti kisukari isipite kipimo cha saba cha HBAIC.
- Shinikizo au msukumo wa damu usizidi kipimo cha 130/80 mmHg na kutumia dawa zinazofaa.
- Usile sukari na chumvi nyingi na kula chakula ambacho hakina protini nyingi wala mafuta mengi.
- Pima figo lako walao mara moja kwa mwaka. Pima kiasi cha albumin kwenye mkojo na kiasi cha kreatinini kwenye damu (na eGFR).
- Mambo mengine: Fanya mazoezi, uwe na uzito unaokufaa,usivute sigara wala kunywa pombe,pia jizuie matumizi mabaya ya dawa nyingine za maumivu.
Kuzuia ugonjwa wa figo unaoletwa na ugonjwa wa kisukari. Fanya yafuatayo:-
- Mwone daktari wako mara kwa mara.
- Dhibiti kisukari (iwe chini ya HbA1C ya 7 au chini).
- Dhibiti shinikizo la damu, iwe chini ya 130/80mmHg.
- Tumia dawa za kuzuia shinikizo la damu mapema ili kuzuia ugonjwa kuendelea.
- Tumia dawa za kukojoa ili kuzuia kuvimba na pia jizuie matumizi ya chumvi na vinywaji.
- Zingatia matibabu ya ugonjwa sugu wa figo yaliyozungumzwa katika sura ya 12.
- Kupimwa na kuzuia hatari ya ugonjwa wa moyo kwa kutokuvuta sigara,kula mafuta mengi, sukari nyingi na kuzuia shinikizo la damu.
- Kubadilisha dawa ili kuhakikisha sukari haizidi mwilini.
- Ugonjwa ukizidi basi huhitaji dayalisisi au kupatiwa figo.
Zuia shinikizo la damu lisizidi 130/80 na utumie dawa zinazofaa mapema.
Ni lini mgonjwa inafaa amwona daktari?
- Mgonjwa anapoongezeka uzito ghafla, mkojo ukipungua, kuzidi
kuvimba au kushindwa kupumua.
- Maumivu ya kifua, shinikizo la damu kuzidi au moyo kupiga polepole
au mbio kuliko kawaida.
- Uchovu, kukosa hamu ya chakula,ngozi kukwajuka na kutapika.
- Homa isiyoisha, kibaridi, maumivu au kuwashwa unapokojoa, mkojo
unaonuka au damu kwenye mkojo.
- Kiwango cha sukari kuwa chini kila mara na pia kutohitaji dawa ya
insulin au dawa nyingine za ugonjwa wa kisukari.
- kuchanganyikiwa, kusinzia au kuzimia.
Kutibu hatari za magonjwa wa moyo ni muhimu katika
kukabiliana na ugonjwa wa figo aosababishwa na kisukari.