Figo  kushindwa  kufanya   kazi  ina maana  gani ? 
Kazi  kuu  ya  figo  ni  kuchuja  na  kutoa  uchafu,kutoa maji  yasiyohitajika na  kuhifadhi  asidi  kwa  kiasi  kinachohitajika  mwilini. Kupungua  kwa uwezo  wa  figo  kufanya   mojawapo  ya  kazi  hizi ndiko   kunasemekana ni  kushindwa  kwa figo  kufanya  kazi   au  kufeli  kwa  figo.
Kutambua ugonjwa  wa figo
Kiwango  cha kreatinini na yurea  kwenye  damu  ndicho  huonyesha hali  ya  figo. Kuongezeka  kwa  vitu  hivi  viwili  huonyesha  kuwa  figo hazifanyi  kazi   vyema. Kuongezeka  kwa  kreatinini kwenye damu, hata  kwa  kiwango   kidogo  mno,  kunaweza  kuashiria  kupungua kwa   kiwango  kikubwa  cha  kazi  ya  figo. Kwa  mfano  kama kiwango cha kreatinine  ni  1.6 mg/dl, basi  inaashiria  kuwa   figo hazifanyi kwa asili mia 50%  au  hata  zaidi ya  kazi  zake.
Je,figo  moja  ikishindwa  kufanya  kazi  ina maana  zote mbili zimefeli ? 
La! kufeli  au  kuondolewa  figo  moja  hakuathiri  kazi  ya figo kwa sababu  figo  iliyobaki hufanya  kazi  ya figo zote mbili.
Aina  mbili  za  ugonjwa  wa   figo 
    - Ugonjwa  sugu  wa  figo
 
    - Ugonjwa  wa  figo wa  muda
 
Inaposemekana Figo kufeli inamaanisha kuwa figo zote mbili zimeshindwa kufanya kazi.
                         
                    
                       
                            
                            Ugonjwa  wa  figo  wa  muda
Katika  ugonjwa  huu  figo  hudhoofika  katika  muda  mfupi  kwa sababu  ya  mwili  kutumiwa  vibaya. Ugonjwa  huu  huweza  kupona iwapo  matibabu  sahihi  yatazingatiwa.  Kwa  wagonjwa  wengi  figo hurudi  kufanya  kazi  yake  kama  kawaida.
Ugonjwa  sugu  wa  figo
Katika  ugonjwa  huu,  figo  hudhoofika  polepole  kwa muda wa miezi au hata kwa  miaka mingi. Katika ugonjwa huu, utendaji  kazi  wa figo huendelea  kupungua  polepole.Baada  ya muda  mrefu kazi  hupungua kabisa hadi  kiwango  ambacho  ni  kama figo hazifanyi  chochote. Kipindi  hiki  ambapo mgonjwa huwa mahututi  huitwa  kipindi  cha mwisho  cha  ugonjwa  wa figo (ESRD).
Kufeli  kwa figo  kunatambulika wakati asilimia hamsini (50%) ya kazi  zake  huwa  zimekoma.