8: Kushindwa kwa Figo ni Nini?

Figo kushindwa kufanya kazi ina maana gani ?

Kazi kuu ya figo ni kuchuja na kutoa uchafu,kutoa maji yasiyohitajika na kuhifadhi asidi kwa kiasi kinachohitajika mwilini. Kupungua kwa uwezo wa figo kufanya mojawapo ya kazi hizi ndiko kunasemekana ni kushindwa kwa figo kufanya kazi au kufeli kwa figo.

Kutambua ugonjwa wa figo
Kiwango cha kreatinini na yurea kwenye damu ndicho huonyesha hali ya figo. Kuongezeka kwa vitu hivi viwili huonyesha kuwa figo hazifanyi kazi vyema. Kuongezeka kwa kreatinini kwenye damu, hata kwa kiwango kidogo mno, kunaweza kuashiria kupungua kwa kiwango kikubwa cha kazi ya figo. Kwa mfano kama kiwango cha kreatinine ni 1.6 mg/dl, basi inaashiria kuwa figo hazifanyi kwa asili mia 50% au hata zaidi ya kazi zake.

Je,figo moja ikishindwa kufanya kazi ina maana zote mbili zimefeli ?

La! kufeli au kuondolewa figo moja hakuathiri kazi ya figo kwa sababu figo iliyobaki hufanya kazi ya figo zote mbili.

Aina mbili za ugonjwa wa figo

  1. Ugonjwa sugu wa figo
  2. Ugonjwa wa figo wa muda
Inaposemekana Figo kufeli inamaanisha kuwa figo zote mbili zimeshindwa kufanya kazi.

Ugonjwa wa figo wa muda

Katika ugonjwa huu figo hudhoofika katika muda mfupi kwa sababu ya mwili kutumiwa vibaya. Ugonjwa huu huweza kupona iwapo matibabu sahihi yatazingatiwa. Kwa wagonjwa wengi figo hurudi kufanya kazi yake kama kawaida.

Ugonjwa sugu wa figo

Katika ugonjwa huu, figo hudhoofika polepole kwa muda wa miezi au hata kwa miaka mingi. Katika ugonjwa huu, utendaji kazi wa figo huendelea kupungua polepole.Baada ya muda mrefu kazi hupungua kabisa hadi kiwango ambacho ni kama figo hazifanyi chochote. Kipindi hiki ambapo mgonjwa huwa mahututi huitwa kipindi cha mwisho cha ugonjwa wa figo (ESRD).

Kufeli kwa figo kunatambulika wakati asilimia hamsini (50%) ya kazi zake huwa zimekoma.